mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Umenifokea kweli Mwengeso !!. Hata umenukuu katiba mbovu lakini pia hamuifuati .
Hivi nikuulize lugha ya Kilwa ilifaa kweli ?!. Unaulizwa mkwamo wa unenzi wa stand , halafu unasema shauri yenu na Bwege wenu !!. Unaombwa maji Bunda halafu unasema mimi siwezi kuwanyima wanangu chakula nikawape wa jirani ?!. Mbona kodi zao unakusanya na kuweka kwenye kapu kubwa (hazina) ?!. Unaombwa barabara moshi halafu unasema safari nyingine mjue namna ya kuchagua ?!.
Ndiyo maana nika refer uongozi wa Mwl Nyerere . Uliwahi kufanyika uchaguzi mdogo huko Arusha , nadhani ni Karatu , pamoja na kuendako yeye kama Rais, amiri Jeshi na mwenyekiti wa Tanu . Lakini bado wananchi walimchagua mgombea binafsi Mr Sarwat . Mwl Nyerere aliwaheshimu wale wananchi na akaichukulia Ile kama challenge ndani ya chama chake na hakuwabagua. Sasa huyu wetu anayewabagua watu kwa sababu wameikataa Ccm Je ??!!.
Lugha ya Lissu ni kali kwa sababu alivyotendewa si kibinaadamu . Alipaswa kuombwa radhi hata kwa mlango wa nyuma.
Mkuu Odhiambo Cairo, sikukulenga wewe kujibu hoja zako.
Kwamba Katiba ni mbovu ni mtazamo wa kila mtu kulingana na Ibara zinazogusa haki na uhuru wake binafsi au kikundi km chama cha siasa.
Kauli/majibu za Rais aliyeko madarakani, uliyotoa mfano nimekwisha yatolewa majibu. Kwamba tangu upinzani uanze 1992 ni mwendo wa kuhujumu juhudi za Serikali za maendeleo. Hivyo basi, nia ovu ya Wabunge/Madiwani wa upinzani kukwamisha shighuli za maendeleo ndio msingi wa kauli hizo. Naam, wanaosababisha wananchi wabaguliwe ni viongozi wa upinzani
Hakuna anayebisha Lissu alitendewa vibaya. Ila tangu apate fahamu amekuwa akihituhumu Serikali kwa shambulio hilo. Je, ukweli utakapowekwa wazi kuwa Rais au viongozi wa Serikali hawahusiki, ataomba msamaha?