cotyledon
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 2,260
- 1,629
Hoja nyingi hapo si za kweli na ambazo zina ukweli zimefanywa kwa manufaa ya taifaJe hoja alizo orodhesha ni za kweli au si kweli?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hoja nyingi hapo si za kweli na ambazo zina ukweli zimefanywa kwa manufaa ya taifaJe hoja alizo orodhesha ni za kweli au si kweli?
28. Kuwanyima pensheni wastaafu wa EAC.Magufuli kauliza katenda dhambi gani asipewe tena miaka 5. kwanza dhambi kubwa sana ni RAMBIRAMBI za tetemeko, kivuko kwa wahusika ziligeuzwa kuwa mali ya serikali na ikafanya kazi ya serikali huku mfuko wa maafa upo na bajeti yake ilipitishwa.
Sasa majibu yake haya hapa:
1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8 .Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika..!! Hakika amelitimiza hilo.[emoji848]
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai kuwajua
Ninachokiona kwako ni kuishi kwa kukariri, kuishi kwa mazoea. Acha nikwambie ndugu, usichojua ni kuwa Kuna magufuli na CCM. Pia usichojua ni kuwa nyakati zinabadirika.Mnachosahau ni kuwa CCM ni taasisi kubwa. Haifanyi siasa kuelekea uchaguzi mkuu halafu ukimalizika eti na yenyewe iache siasa.
Mikutano ya matawi itaendelea kama kawaida mikutano ya mikoa itaendelea kama kawaida.
Huwezi kulinganisha na Chadema ambacho ni chama chenye udhaifu mwingi kwa ngazi za chini, chama chenye kukosa nidhamu ya kudumu ya uendeshaji.
Kuitoa CCM ni lazima chama kingine kiwe na muundo imara wa kitaasisi sio hizi blah blah za jamii forum.
Ipi ambayo si ya kweli?Hoja nyingi hapo si za kweli na ambazo zina ukweli zimefanywa kwa manufaa ya taifa
Mzalendo yuko wapi ?!Magufuli anaweza asifae kwa viwango vya mleta uzi lakini ni mara elfu kumi awe yeye rais kuliko huyo anayetishia watu kuwa tutashtakiwa na wazungu halafu hao hao wakapanda ndege kuja Tanzania ili kushirikiana na serikali.
Magufuli na udhaifu wake wote ni mzalendo kuliko mgombea yoyote mwenye nia iliyojificha ya kumtumikia mtu wa nje.
Wote uliowataja misingi na historia ya mataifa yao huwezi kuifananisha na Tanzania.Ninachokiona kwako ni kuishi kwa kukariri, kuishi kwa mazoea. Acha nikwambie ndugu, usichojua ni kuwa Kuna magufuli na CCM. Pia usichojua ni kuwa nyakati zinabadirika.
Mawazo yako alikuwa nayo Omari Al Bashir Ila nyakati zilimfundisha
Mawazo yako alikuwa nayo Robert Mugabe Ila nyakati zilimfundisha
Mawazo yako alikuwa nayo Col Gadafi ila nyakati zilimfundisha.
Maana halisi za nyakati ni kuwa akili za watu za mwaka 1977 au 1995 sio akili za watu wa mwaka 2020.
Kama ni mgumu kuelewa naomba nikujibu kuwa wewe na magufuli somo la nyakati litawafundisha vizuri mwaka huu 2020
Endelea kuishi kwa kukaririWote uliowataja misingi na historia ya mataifa yao huwezi kuifananisha na Tanzania.
Ni yale yale ya kuombea tajiri kama Bakhresa dua mbaya, unatwanga maji ndani ya kinu.
Yupo kwenye kampeni na jana alimvalisha Diamond kofia.Mzalendo yuko wapi ?!
Endelea kuishi kwa kukariri
Hata wazungu hawakuelewa kwanini Nyerere alitaka tuwe huru. Kwasababu walijenga reli, barbara, shule, haspitali, nk.Binadamu yeyote anapenda sana kuwa kwenye comfort zone, yaani hatakubaliana na Jambo lolote hata liwe jema namna gani litalomuondoa kwenye hali aliyokuwa awali.
Mabadiliko yaliyoletwa na awamu ya tano yametufanya tuwajibike kwa asilimia kubwa katika kulipa Kodi, na kuwajibika katika nyanja nyingine pia za kijamii,
Sasa kwa kuwa kuna watu waliokuwa wakifaidi mfumo uliopita na sasa wamebanwa lazima walalamike,
Ndio hawa mleta mada akiwemo.
Mzalendo hawezi fika mahali, akawambia wananchi kuwa sikuleta maendeleo kwa sababu mlikosea kuchagua !! eg Moshi, Kilwa , Bunda nk .Yupo kwenye kampeni na jana alimvalisha Diamond kofia.
That is just a proverbYou cannot teach an old dog new tricks.
Msege, kifungu kandamizi namna hii ya katiba siyo ya kushangiliwa. Hii ni ya kupingwa kwa jasho na damu.Nyie siyo NECView attachment 1562566
Maovu yaliyotendwa na uongozi wa CUF,Chadema na mjomba wao NCCR Mageuzi.Hongera kwa kuorodhesha matokeo ya Tawala zilizolea:
• ufisadi;
• uzembe; na
• matumiza mabaya ya madaraka.
Hongera kuorodhesha maovu makuu hayo yaliyoshughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Alithubutu akatekeleza. Anastahili kuongezewa muda asafishe kabisa ambao bado wana mawazo ya kuturudisha kwenye tawala za kulea uovu.
Kwahiyo hata waliokosa ajira nao walikuwa wanafuika wa mfumo uliopita?Binadamu yeyote anapenda sana kuwa kwenye comfort zone, yaani hatakubaliana na Jambo lolote hata liwe jema namna gani litalomuondoa kwenye hali aliyokuwa awali.
Mabadiliko yaliyoletwa na awamu ya tano yametufanya tuwajibike kwa asilimia kubwa katika kulipa Kodi, na kuwajibika katika nyanja nyingine pia za kijamii,
Sasa kwa kuwa kuna watu waliokuwa wakifaidi mfumo uliopita na sasa wamebanwa lazima walalamike,
Ndio hawa mleta mada akiwemo.