Kwa kuwa viongozi wa upinzani wanapenda kudai kuwa utawala wa sasa hafuati Katiba, ni dhahiri kuwa hwaijui na hivyo basi wanajidharilisha. Soma Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Katika miaka 5 ya utawala wa Serikali ya CCM, inayomaliza muda wake, tumeshuhudia Wabunge wakisusia vikao vya bunge na kutokupitisha bajeti. Pia tumeshuhudia Wabunge na Madiwani kutokutoa ushirikiano kwa watendaji wa Serikali. Kimsingi, maana vitendo hivyo (kinyume na Katiba) vililenga kukamwisha maendeleo ili wananchi waichukie Serikali.
Serikali, pamoja na nia ovu hiyo ya kukwamisha maendeleo, bila kujali, ilitekeleza miradi ya maendeleo katika Kata na Majimbo ya upinzani. Upinzani kuona hivyo, umebadili nia yao ovu na kudai miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ni ya "vitu" siyo ya "watu".
Je, katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, wameweza kueleza maendeleo ya watu ni yapi na miradi yake itakuwa ipi? Kinachoendelea katika kampeni za Lissu, Mgombea wao wa Urais, ni kumdhihaki na kumkejeli Rais aliyeko madarakani, akiamini ndiyo turufu ya yeye kuchaguliwa. Tunategemea, kama ulivyosema, kiongozi awe na lugha nzuri ya kuwasilisha hoja zake hata kama ni amri, nikinukuu Nimeishi wakati wa Mwl Nyerere . Hakuwahi kuropoka . Hata kama jambo hakulipenda alitafuta lugha nzuri ya kuwakanya.
Pasipo shaka Lissu ni punguani au msomi uchwara. Akili zake zimejaa takataka na wanaomshabikia ni Wapumbavu na Malofa