Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Mwanamke yeyote anahitaji usalama kutoka kwa mwanaume wake, ndicho kitu cha kwanza wanakiangalia kabla ya kuwa kwenye mahusiano, japo huwa halisemwi waziwazi.
Usalama wanaotaka ni usalama wa kiakili, kiroho na kimwili ilii aweze kujiachia kwa mwanaume. Usalama wa kimwili mwanamke huupata pale anapojua mahitaji yake ya kimwili yanaweza kutimizwa, na mahitaji ya mtoto wake yataweza kutimizwa.
Hela inatimiza mahitaji makuu ma 3 ya kimwili. Mwanamke anakua na uhakika anaweza kuvaa, kula na kulala sehemu nzuri na salama, ukiwa na pesa hivyo vitu vinakua rahisi kwako kutimiza. Sehemu pakiwa na uhakika wa kula basi mtu hujisikia salama kuishi, haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
Pia hela inaepusha migogoro midogo midogo, Mfano, unakuta mwanaume anamlalamikia mwanamke anamaliza sabuni ya kuogea, huyo mwanamke atajisikia usalama kuishi na mwanaume anayemuacha ajisafishe kwa amani bila kulalamikiwa kuhusu sabuni.
Hela inawezesha kusafiri na kufurahia sehemu tofauti. Ukiwa na pesa ni rahisi kumtoa mwanamke wako kwenda kutembea (ni jambo muhimu).
Wanawake wanapenda kuweka kumbukumbu tofauti tofauti pamoja na watu wawapendao. Usije ukakaa na mwanamke sehemu moja tu siku zote 365, utachokwa. Panga siku za kutoka. Haijalishi una hela kiasi gani, ila hakikisha mnabadili mazingira angalau mara moja kwa wiki.
Hela inasaidia kupata huduma za kiafya kirahisi. Atajiona yupo salama kwako unapokua na hela ya kumhudumia anapoumwa. Wanawake ni rahisi kukubali kuwa ni wagonjwa (sisi wanaume tunaona kuumwa ni udhaifu) ndo mana mara kwa mara atakuambia anaumwa, sio jambo baya sababu inabidi wawe na afya nzuri ili waweze kuleta uhai mpya wenye afya hapa duniani.
Mahitaji mengine kama vocha, vipodozi na manukato unaweza msaidia kadri uonavyo sawa, hakikisha mwanamke unayetaka kujenga naye maisha anayaweza hayo mahitaji madogo, pia unaweza mfundisha jinsi ya kupangilia matumizi ili asikuelemee kwenye hivyo vitu vidogo.
Ila usije ukadhani ni hela pekee ndio itakuwezesha kumtunza mwanamke wako. Wapo wanaowatimizia wanawake mahitaji ya kifedha na wamewashindwa wanawake, sababu wameshindwa kutimiza mahitaji mengine.
Bali uwezo wako wa kumridhisha kimwili, kiakili na kiroho, na kuwa kiongozi wake mzuri unakuwezesha kumtunza mwanamke unayetaka kujenga naye maisha, ndio maana katika kundi la infinite kiumeni utajifunza kila siku jinsi ya kumvutia na kumtunza mwanamke unayetaka kujenga naye maisha.