Sababu hizi zitatufanya ichukue muda sana kupata viongozi kama Hayati Magufuli na Mwalimu Nyerere

Hizo pesa ziliwekwa china zisharudi ?
Inatosha kujuwa kuwa Magufuli alitengeneza kutengo cha Plea Bargain ili kunyang'anya watu fedha na kuzificha China. Suala la kurudi linategemea na aliyezipokea alikuwa na makubaliano gani na wawekaji.

Hata fedha alizoficha Sani Abacha kwenye mabenki ya Ulaya na America siyo zote zilizorudi.
 
Naomba na Mkapa umuweke kwenye list yako.
Nakubaliana nawe, lakini inafaa umtungie mada ikidadavua yaliyofanyika chini ya uongozi wake.
Ule ubinafsishaji wa mali za umma hovyo hovyo ulimpunguzia heshima ambayo angeistahili.

Alipenda sana kusikiliza hao hao mabepari wa nje na ushauri wao bila ya kupima athari zake kwa nchi anayoongoza.

But all in all, alipenda kuipambania Tanzania na watu wake.
 
Ewe mwenyezi Mungu tuepushie mbali na viongozi dizaini ya yule dikteta uchwara
 
Ewe mwenyezi Mungu tuepushie mbali na viongozi dizaini ya yule dikteta uchwara
Tukitaka tuondoe huu umaskini tulionao tunahitaji dikteta mkuu atulazimishe kufanya kazi kwa bidii,atulazimishe tuwe na nidhamu kazini lakini atulazimishe tuwe wazalendo hata kama hatupendi.Maendeleo kwa wote kama nchi yana misingi yake lakini tukienda hivi watafaidika wachache na wengi wataendelea kulia na umaskini mpaka kiama.
 
Hizo kazi ziko wapi?
 
Daaah...!umezunguka sana aisee kwa hicho unachokisema hapo hatupaswi kupongeza kwenye mazuri wala kukosoa kwenye maovu.
 
Embu niambie dhambi kubwa alizotenda mpaka umwite Shetani na kipimo kipi cha dhambi ulivyotumia kupima wingi wa dhambi zake
Kutunyima haki zetu kama watumishi wa umma for 6yrs.
Huo ni ufedhuli. Alizitesa sana familia zetu shetani yule
 
Lile shetani lenu ni chafu tu
 
Sikutegemea utaandika ajabu kama hii
 
Mwenyezi Mungu atuepushe tusije pata Marais wabovu kama hao wawili.

Magufuli and Nyerere were the worst presidents in the history of Tanzania.
Ni vile walitumia na kufaulu kwenye propaganda + ujinga wa Watanzania. Facts are consistently against their purported legacies, respectively.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…