Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Wanandoa wengi wanafanya mapenzi kama jukumu na siyo starehe ya kufurahishana. Na wanaume wengi wamekuwa wabinafsi kwasababu wanafikiria tu mihemko yao bila kujali unayemtumia anahali gani.
Mwanamke ni mtu anayefanya vitu vyake kwa hisia, kwahiyo kabla hujataka kufanya hicho unachotaka kufanya, swali umemuandaaje?
Na hapa siongelei romance, kuna hii dhana wanaume mnayo mnatoka sehemu zenu za kazi mnadai mmechoka hamtaki stori, mwanamke hata akikuongelesha vizuri unakuwa mkali, au unamuongelesha vibaya, umemdhalau, kumsimanga, unamkaripia, kosa dogo utafoka hata mbele ya watoto.
Ngoja nikusanue mwanaume kama umefanya hata mawili kati ya haya nakusibitishia huyo mwanamke hata kama alikuwa amejipanga kukufurahisha hisia huwa zinapotea na hamu inakata kabisa, ndiyo maana anakataa. Na kama akikupa basi amefanya kukuridhisha wewe au kupunguza shauku yake lakini siyo kafurahia.
Hisia za mwanamke ni dhaifu sana, unaweza kudhani anakufanyia kusudi au anaringa, kumbe mwenzio ukiumiza moyo wake umempotezea hisia kabisa. Lakini nyie wanaume hata mkeshe mnatupiana maneno bado mtahitaji kupiga shoo, haijalishi mwanamke kakukera kiasi gani.
Ushauri wangu kwenu wanaume, ukifika nyumbani kwako hata ukiona makosa yamefanyika nyamaza kwanza kama ni mengi orodhesha pembeni, na ni busara kama mambo yenu mtaongelea chumbani na siyo umfokee mbele ya familia.
Muache akufurahishe kwanza akishamaliza kukuonyesha ufundi wake unaweza kuongea vyote unavyotaka.