Hayo ni mawazo yako but katika hila za marekani mojawapo ni kudhoofu mataifa mengine kiuchumi kisiasa, kijamii na kiteknolojia.
Marekani ni taifa la kibepari au taifa la kibeberu. Mojawapo ya kanuni au azimio la bepari au beberu yoyote yule ni kuhakikisha wanaomzunguka wanakuwa dhaifu kwa kila namna ili wasiweze kumpa challenge yoyote na atafanya kuwa life mission yake miaka yote kuwadhoofu sababu kwake ni threat na akiruhusu wakue na kuimarika ina maana anarisk kutolewa katika nafasi yake kama mbabe au mshika hatamu.
Hili ni kosa alilifanya kwa mchina nadhani hayupo tayari lijirudie. China kwasasa ni jabali wa miraba minne ambaye yupo tayari kumfokea marekani endapo atamletea maneno au chokochoko bila kufyata mkia katikati ya miguu na kuinamisha kichwa akiondoka kwa unyonge. Kumbuka China huyu huyu miaka ya 1950's alikuwa ni mwenzetu kwa namna nyingi kwa maana tulikuwa katika hali za kufanana kihali ila leo miaka kadhaa ametuacha na kufanikiwa kupata siti katika meza kuu ya maamuzi.
Marekani na mataifa menzake ya kibepari wanahofu endapo afrika nayo itaimarika kwa maana ya mataifa ya afrika yakishaanza kusimama kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kitechnology hatua itatakayofuata ni mataifa haya kuanza kushirikiana na kujenga mifumo ya umoja wa kikanda na hatimaye bara hili kuunda umoja wake na kuwa taifa moja kubwa sana. Hii haitazuilika maana ni kanuni ya kisayansi na ni lazima itatokea. Nani atataka kuwa taifa kubwa huku amezungukwa na majirani dhaifu.
Afrika ikiungana tayari kutakuwa na giant meza kuu infact africa anaweza hata akajitenga na kuwa na mambo yake kwa 90% ,wadhani afrika atapata nini kwa marekani kama partner kama atajitegemea kwenye kila eneo maana resources anazo.
Kitakachofuata ni marekani kudaiwa reparations (stahiki) au fidia za madhara yaliyosababishwa na utumwa na siasa zake za kitapeli. Yeye pamoja na wenzake. Sababu vijana wa kiafrika watakuwa wamesoma na wanaelimu ya kila aina ikiwamo sheria ambayo itatumika kupeleka miswaada balaza la kimataifa kuishitaki Marekani na Europe ya Magharibi kwa madhambi yake ya Utumwa na ukoloni na kuigandamiza kibepari Africa kwa karne na karne na kuidhulumu wazi wazi tena kwa mikataba ya kinyonyaji na kuwarudisha nyuma watoto wa bara hili takatifu.
China, Urusi, india, na wengineo watapiga kura ya ndio na kukubali kuisapoti Afrika na marekani na Europe ya Magharibi italazimika kukubali kulipia madhambi ambayo yatawafilisi kiuchumi kwa asilimia kubwa sana na kuwekewa masharti magumu ya kiuchumi ikiwamo kunyimwa rasilimali na kukataliwa kushare mahitaji mbali mbali ya kiuchumi na kutesa raia wao.
Marekani anajua hili litatokea akilegeza macho yake juu ya afrika sababu ndicho kinachofuata miaka kadhaa ijayo. Sasa inabidi aje na mbinu kadha wa kadha kudhoofu ustawi wa jamii ya mataifa ya afrika ili tuvurugwe huku yeye akija na mbinu kadha wa kadha kutumia kila tulichonacho.
Kaleta haki sawa a.k.a 50/50 ili wanawake wasielewane na wanaume washindwe kujenga familia imara ambazo zitaleta ustawi wa jamii.
Anashawishi sana uwekezaji katika wanawake na kuwapa empowerment kiuchumi na siasa ili kumtoa mwanamke nyumbani na kumfanya mwanaume kuwa dhaifu sababu mwanaume ambaye atarudi katika nyumba ambayo haina amani, hakuna mwanamke wa kumpokea na kumfariji na kupanga nae maisha huyu mwanaume hatoona haja ya kutulia sehemu moja na atabakia kutanga tanga na kuishi maisha ya ubabaifu bila direction kama askari aliyerudi vitani na msongo wa mawazo akiwa na kumbukumbu za vita tu kichwani mwake.
Mwanamke akitolewa nyumbani anaacha kuwa mama anabakia kuwa mwanamke, kama vile mkulima hawezi kuwa mkulima bila kuwa shambani kwenye shamba ndivyo mwanamke hawezi kuwa mama akiwa hayupo nyumbani kwake.
Kama vile ndege mpumbavu aachaye makinda yake kwenye kiota bila kuwalinda na kuwapelekea chakula na kuwakinga na baridi ndivyo mwanamke wa sasa ameacha kutazama familia yake yaani mume wake na watoto akiwa nje ya nyumba yake kukimbizana na ndoto ambazo atakapofika kuanzia miaka 50 huwa zinayeyuka zote na anaanza kuface reality ya maisha kuwa si kweli jamii ilimuhitaji kama mchapakazi, mwanamke wa shoka, Supawoman, role model in business, ila kama mama bora kwa watoto na mke bora kwa mume.
Watoto wetu wapo pekee yao kwenye nyumba wakikuzwa na Media zisizozingatia maadili. Marekani na vibaraka wake wanawajia watoto wetu kwa njia hiyo na kuwateka akili na kuwatoa katika ubora wao na kuwashape kwa namna yao. Halafu tunakuja kuulizana why ushoga unakua ila hatuulizani why mama hakai na watoto nyumbani na kwann baba anazidiwa na gharama za uchumi sababu ya uzembe wa serikali kusimamia uchumi ili maisha yawe rahisi kwa baba kuweza kumudu gharama za maisha kwa familia yake na kuishi kwa amani na mkewe bila kumtaka ataoke nje kutafuta.
Jibu ni marekani na vibaraka wake wanamkono mrefu katika siasa,jamii, uchumi wetu na kusababisha gharama za maisha kuwa juu na kucheza na akili za raia wetu.
Umeshawahi jiuliza wale wazungu au raia wa kigeni wa kutoka magharibi huwa wanakuja kwenye vikao vyetu kusikiliza nini na kufuatilia nini?
Kuna mengi sana nita yaandalia Podcast ili tuweze kuongea na kujadili kwa mapana.