Sababu muhimu zinazoifanya hii kuwa Nyumba ya gharama nafuu zaidi ya vyumba vitatu

🙏🏾 Shkrani kwa maoni, ninachokukubali unakuja na maoni yenye logic.
1. Umetoa wazo zuri, ila kwa kawaida moja kati ya kazi muhimu za Septic ni kufanya “skimming” ya maji taka, na maji ya jikoni huwa yakua na skam layer ya mafuta ambayo isipoondolewa inaenda kupunguza ufanisi wa shimo kunyonya maji (mafuta yanatanda kwenye kuta za shimo). So ikilazimu yes yanaweza kuwekwa direct kwenye shimo linalonyonya.
2. Hapa nakubaliana nawewe kwa kiasi kikubwa but still ninachofahamu setbacks huwa zinaangaliwa pia na nimeweka picha hapo uangalie
3. Vitu vingi vinawekwa kwenye makabati ya kikoni siku hizi, mikaa na vingine vinawekwa nje huko, si wote wanataka stoo ya ndani kuna watu nisha wachorea nyumba kubwa na bado hawakutaka store ya ndani
4.ok sawa
5. Hapo kwenye kuondoa dining nafikiri tutaongea yaleyale ni mtazamo wa mtu pia. Ushauri mzuri tho🙏🏾
 

Attachments

  • A925CACC-DF56-4F79-A801-8F1FDB8CF747.png
    58.6 KB · Views: 73
1. Ni kawaida kuunganisha gully trap ya jikoni na septic tank. Makosa yetu ni kuwa tunatumia njia hiyo hiyo ku tupia mafuta ya kupikia. Kufanya hivi kunaleta matatizo ulioyataja. Kinachotakiwa kufanywa ni kukusanya mabaki ya mafuta tunayopikia na kuyatupa nje ya sewage system.
2. Setbacks zinaangaliwa kwa sababu ni mojawapo ya vigezo vya manispaa katika kuhakikisha majengo yana nafasi ya kupumulia na kupata mwanga wa jua. Hamna universal standard. Kila manispaa inaweza kujiamulia. Ukienda nchi nyingine, kuna maeneo setback za pembeni zinakuwa hazihitajiki na watu wanajenga mpaka kwenye party walls.
Hizo standards ulizoziweka sijui ni za manispaa ipi maana kuna vitu vingine havina mantik. Una legislate vipi idadi ya household? Unaruhusu vipi majengo mawili kwenye kiwanja lakini unalazimisha household 1? Ina maana jengo la pili haliwezi kuwa la mfanyakazi au mpangaji? Maximum ni moja tu. Hauwezi kuwa na maximum ghorofa 4 mpaka 6. Ni 4 au 6, basi. Unawekaje vigezo katika eneo halafu unaliita unplanned? Haya ni matatizo ya planning conditions zetu ambazo kiukweli nyingi ni copy and paste.
3. Ni kweli kuwa stoo inategemea matakwa ya mtu. Ubaya wetu tunaiga bila kujua na tunaamini kuwa stoo ni kwa ajili ya mkaa na magunia ya mpunga. Sio kila kitu kinawekwa kwenye makabati ya jikoni. Vitu kama pasi, meza ya kupigia pasi, toilet paper za ziada, tv iliyoharibika lakini hutaki kuitupa, glopu za akiba n.k. vyote vinawekwa kwenye stoo na sio kwenye makabati ya jikoni. Nadhani hao unao wachorea ukiwaambia unawareness pantry badala ya stoo watakubali.
4. Kuondoa dining room ni kutokana na nafasi uliyokuwa nayo ambayo imekufanya uigeuze kuwa korido ya kwenda vyumbani na chooni.
Huu ni ushauri na mawazo yangu tu.

Amandla....
 
Kiongozi nataka kama hii isiyo na mbwembwe ya vyumba vitano(master moja,public toilet moja,sebule iliyounganika na dining hapohapo(11*14),jiko dogo tu(6*6)
Hebu angalia nilivyojaribu kudesign unitekebishe.
 
🙏🏾Shukrani kwa maoni mazuri
 
mm ni Quantity Surveyor ( mkadiliaji majenzi) kwa anayeitaji uduma ya kuandaliwa Boq ya kuonesha garama za ujenzi wa nyumba yake au kwa kuombea mkopo pia kuandaliwa materials ambayo yataonesha nyumba yake inatumia material gan na kias gan na garama kiasi gani pia ata ukitaka kujengewa kwa bei nafuu kabisa bila kusahau kuchorewa raman nzuri na bora nicheki watsap 0753757303 /0677400169/0658400165
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…