Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Mungu anahitaji kusaidiwa na mitume?

Kwani kashindwa kutupa ujumbe mwenyewe moja kwa moja tumuelewe kwa njia ambayo haina utata yupo?
 
Yaani ungefanikiwa ni kueleza ni kwanini nature inanitaka niunge kipindi hiki basi ungepata kura yangu.
 
Mungu anahitaji kusaidiwa na mitume?
Nani amekwambia kwamba kuwatuma waja wake miongoni mwa waja wake ni kusaidiwa ?

Soma Historia ya nabii Musa na Farao,nabii Musa akiwa na ndugu yake Haroun walitumwa kwa Farao wa wakati ule,ila wakaambiwa nendeni mkambainishie haki kwa bayana na kauli laiji huenda akaikubali haki,lakini ikawq kinyume,lakini kilimkuta nini baada ya kukaidi,Mola huyo huyo akampa uwezo mja wake Musa kwa fimbo tu ikapasua bahari na kupita kati kati. Huyu ndiyo muweza wa yote.

Nakukumbusha tu kuhusu kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora,malaika wawili walio tumwa na Allah waliuangamiza mji ule,ila kwa uwezo wa Allah mtukufu. Utendaji wake wa ajabu sana.
Kwani kashindwa kutupa ujumbe mwenyewe moja kwa moja tumuelewe kwa njia ambayo haina utata yupo?
Hilo hajashindwa kwake dogo sana na angetaka ingekuwa hivyo.

Allah mtukufu anasema katika Qur'aan,sura ya 10 aya ya 99 :

99. Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini? (Yunus : 99)

Hili swali limeisha,sitarajii kama utaliuliza tena.
 
Tangu Yesu aondoke zimepita siku 2 huko mbinguni. Tutangoja sana asee.
 
Yani Mungu anauwezo wa kufanya lolote.

Ana uwezo wa kumfanya Farao amkubali kirahisi tu.

Lakini anamnyima Farao uwezo wa kumkubali Mungu.

Anaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu kumkubali Mungu.

Halafu anamhukumu Farao kwa kutokubali maneno ya Mungu?

Unaelewa hapo Mungu wako ndiye yuko responsible, si Farao?

Unaelewa Quran inasema Allah atawafanya watu fulani mioyo hao iwe mizito, macho yao yasimuone na masikio yao yasimsikie.

Yani Allah anawafunga macho watu wasimjue, anawaziba masikio wasimsikie, anaifanya mioyo yao iwe migumu wasimkubali.

Halafu anawahukumu watu hao hao vikqli sana kwa kuwa hawajamkubali.

Huyu Mungu yupo kweli au mnalishana ujinga tu?
 
Tatizo bro hoja zako huwa nzito sana
 
Umeongea ukweli kabisa... Hawa watu wanapotea kwasababu hawajitahidi kijitafutia ukweli kwa kuyasoma maandiko na kuyaelewa

Kwa mfano wanalitukuza jina la Mariamu kuliko Jina la Yesu ambaye ndiye aliyekuja kwaajili yao

Inasikitisha
Inasimuliwa na imeandikwa.
Zote zipo sawa inaweza kusimuliwa ikiwa kwenye maamdishi au kusomwa ikiwa simlizi pia.
Hapa uelewatu.
 
Unaelewa Quran inasema Allah atawafanya watu fulani mioyo hao iwe mizito, macho yao yasimuone na masikio yao yasimsikie.
Safi kabisa,hili litafanyika baada ya nini na nini ?
Yani Mungu anauwezo wa kufanya lolote.

Ana uwezo wa kumfanya Farao amkubali kirahisi tu.
Farao alikuwa huru au hakuwa huru ? Je alilazimishwa kufanya uovu au alifanya kwa hiari yake ? Swali kwanini hakufanya wema na akafanya uovu ?
Lakini anamnyima Farao uwezo wa kumkubali Mungu.
Wapi Farao alinyimwa uwezo wa kumfahamu Mola wakati yeye mwenyewe alikuja kukiri ya kuwa Mola ndiye mkuu,ila baada ya kuona maji yamemfika shingoni,sababu Farao huyo alikuwa ana dai uungu.
Yani Allah anawafunga macho watu wasimjue, anawaziba masikio wasimsikie, anaifanya mioyo yao iwe migumu wasimkubali.
Naomba uniwekee aya ya haada ya hii na moja kabla ya hii. Maana majibu yako wazi.
Hapa ituhumu akili yako na elimu,sababu unavyoandika ni kinyume na maandiko bali kinyume na uhalisia.
 
Nipo ndugu Makaveli, habari ya siku?

Okay nashukuru kwa maelezo marefu, ila kimsingi maelezo yangu yalihusiana na hoja ya mtoa mada ambae alikuwa anajaribu kutuaminisha kuwa faida za kufunga zinapatikana mwezi huu tu kutokana na sababu zake za kiimani kitu ambacho sio kweli hiyo ni moja,

Pili ni kuhusu maelezo yako marefu kwamba nyie mnafunga kwa sababu za kiimani, hilo nalielewa vizuri japo sikubaliani na maelezo yako ambapo umedai kuwa mola wenu ndio aliwaambia mfunge.

Asante rafiki, kitambo sana na nakutakia mfungo mwema!!
 
Mnazingua mara kiarabu na quran lugha mbili tofauti mara tena ni kiarabu wazee wa kupata thawabu mnazingua!
 
Mwaka huu nilifunga mwezi wa ramadhani japo mm mkristu, Asante kwa somo Hili maana sikulijua nilifunga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…