Jibu maswali acha longolongo, hakuna Sheikh wa kuweza kujibu hayo maswali zaidi ya kukuambia elimu ya Quran ni pana sana na wewe huwezi kuielewa kwa sababu huelewi Kiarabu.
Yani hiyo habari ya elimu ya Mungu kuwa complicated na kushushwa kwa lugha fulani tu inaonesha huyo Mungu hayupo, katungwa na hao Waarabu.
Angekuwepo, wala tusingehitaji kitabu kumjua kwa uhakika.
Elimu ya uwepo wake ingekuwa hardcoded kwenye DNA kwa kiasi ambacho asingeweza kupingika na mtu yeyote.
The fact kwamba mnahitaji vitabu kumuelezea Mungu inaonesha huyo Mungu katungwa na watu tu, hayupo kiuhalisi.
Nitaacha shughuli zangu kujibu tu maswali uliyokopi sehemu kaka, mambo ni taratibu nitakuwa nakujibu kadri nioatavyo nafasi, umekusanya vitu tofauti kwa wakati mmoja, sijui nijibu kipi niache lipii
Haya bismillah, naanza na hizi contradictions zako juu ya uumbwaji wetu..
Labda nikusaidie kidogo, kwa hapa ni dhahiri unafata upepo kaka, hujasoma quraan wala kuhangaika kusoma hizo unazoita ww ni contradictions, kwa vike ww ni atheist basi kila unachokiokota ni unaamini 100%...
Tuanze na hizo contradictions chache..
Tuchukulie mfano wa ukuaji wa kipepeo..
Anaanza yai kwenye gamba chorion, kisha kiwavi, kisha pupa halafu ndio kipepeo kamili kama sijakosea,
Je mungu akisema amemuumba kipepeo kutoka kuwa chorion, yai ama buu atakuwa kakosea, hizo ni stages ambazo kipepeo anabadilikia..
Sasa mungu anaposema katuumba kwa udongo, hiyo ndio uhalisia, tumeumbwa kwa udongo, ikisha akajaalia sisi kutokana na manii, kuwa pande la damu, kisha, kijusi na kadhalika, ametaja hatua zoote hizo ni elimu kwetu tujue tulianzia wapi, na hatua zoote zimetajwa katika quraan.
Na anaposema hatukuwa chochote, kwa lugha ya tafsiri unapata tafsir mbili..
Moja, tafsiri ya cheo ama hadhi, mfano mtu anapomsaidia mtu baadae aseme nilimuokota hakuwa na chochote je hakuwa hata na nguo? Hivyo anaposema hatukua chochote kwa bimaana udongo ni dhalili mnoo kulinganisha na matokeo ya kuumbwa kwetu, anatukumbusha sisi tusijione wajanja ni dhalili mnoo na kuna aya ndani ya kuraan kazungumzia hili
Pili, ndio kabla ya kuumbwa hatukuwa chochote, simu kabla ya kutengenezwa ilikiwa ni nini? Cobalt? Lithium? Copper? Gold ama silver, au tulikuwa silicon au lead? La hasha, haikuwa kitu
Umekopi baadhi ya aya hapo juu..
Hizi aya zoote ni kutuonesha hatua zetu za ukuaji, kuwa tulikuwa udongo, tulikuwa manii, kisha pande la damu, baadae kutiwa mifupa nakadhalika
96:2
2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
15:26
26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope meusi yaliyovunda.
3:59
59. Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.
19:67
67. Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla(hali yake hii), na hali hakuwa chochote?
52:35
67. Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?
16:4
4. Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.
Quraan 23 suratul muuminun inakujibu kama nilivyojaribu kukuelezea.. Aya ya 12 mpaka ya 14
12.Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.
13. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika makao yaliyohifadhika(madhubuti)
bila shaka ndio huko tumboni kwenye Uterus
14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji
Nyongeza ukisoma inaweza kukusaidia chief
Suratud dahr 1-3
1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi kirefu katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.(binadamu ndio kiumbe wa mwisho kuletwa duniani) hatukuwa chochote
2. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika(ya mwanaume na ya mwanamke) tumfanyie mtihani(kwa amri zetu na makatazo yetu) Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia na mwenye kuona.
•: hapa mungu anatuongezea kuwa sisi tulipitia katika steji ya kuchanganyika mbegu ya baba na mama
3. Hakika Sisi tumembainishia Njia(mbili, kheri na shari, Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
Hapo ni juu yetu kushukuru ama kufaulu juu ya akili(utambuzi) aliotupa allah
Ama katika sura al qiyama ukianzia aya ya 36-39
36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
(Yaank tusipewe makatazo, tusipewe maamrisho, kwa jinsi tulivyoumbwa ama kuwa kabla)
37. Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?(lililotonwa)
Hapa mungu anaongelea kuwa sisi tulikuwa ni bao, hatua ya kutolewa shahawa ama kukojowa vijana wanasema[emoji13]
38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.(mwanadamu kamili)
39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
Quraan 53:45-46
45. Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa