Who Was the First Muslim? Muhammad [6:14, 163], Moses [7:143], some Egyptians [26:51], or Abraham [2:127-133, 3:67] or Adam, the first man who also received inspiration from Allah [2:37]?
Naanza na hii,kwanza nimecheka kidogo. Kitendo cha kupaste haya yanaonyesha yafuatayo kutoka kwako na kwa yule ambaye ume copy kwake.
1. Hamuijui Qur'aan hata kuisoma.
2. Hamjasoma vitabu vya Tafsiri ya Qur'aan na huenda hamvijui.
Mwanazuoni aitwaye Ahmad bin Ali ash-Shawkaniy alipata kusema maneno yafuatayo "Aya za Qur'aan hazipingani yaani hazigongani kwa zenyewe,ukihisi hali hiyo basi ituhumu akili yako kwa kushindwa kung'amua maana za aya hizo na uituhumu elimu kwa kuwa ni ndogo kuweza kufahamu aya hizo". Huyu ni mwanazuoni wa Tafsiri ya Qur'aan ana kitabu chake kinaitwa "Fat'hu al Qadiir". Kadhalika Imaam Muhammad al Amin ash-Shanqitiy ana kitabu chake maalumu kilichokusanya aya zote ambazo watu wanahizi zinagongana na kuwaonyesha ya kuwa ukweli ni kinyume chake,kitabu hicho akakiita "Daf'u ihaam adh-Dhitiraab 'an ayaat al Kitaab" na ana kitabu chake cha Tafsiri ya Qur'aan kiitwacho "adh-Wau ali Bayani fi idhwah Qur'aan bil Qur'aan". Tafuta vitabu hivyo ili usiendelee kuwa kichekesho.
Narudi katika hizo aya,mitume wote walikuwa Waislamu ndiyo maana ukisoma Qur'aan unakutana na aya hizo zinazo pambanua dini ya mitume na manabii husika. Uislamu umegawanyika sehemu mbili kwa munasaba wa maana yake,migawanyo hiyo ni :
1. Uislamu wa ujumla huu ni ule ambao wanaingia mitume,manabii na wafuasi wao wote walio waamini na kuwafata,ni ule Uislamu wa kukiri ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na hana mshirika,kadhalika kuwapiga vita washirikina kwa hali zao zote.
2. Uislamu khasa (maalumu) yaani huu alio kuja nao mtume,tofauti ya huu na ule ni katika sheria za kihukumu ila itikadi ni moja. Katika ummah huu Muislamu wa kwanza ni Mtume,sababu baada ya kuondoka Yesu kumepita kitambo sana bila kuwepo Mtume,na sababu za kuletwa Mtume katika jamii fulani ni pindi ambapo imani ya usawa hupotea na kuanza kudhihiri ushirikina,na hili ndilo lilikuwepo.Amekuja Mtume kipindi ambacho imani sahihi imepotea na watu wakawa wanaabudu miti,masanamu na mengine,huku mfundisho ya mitume yakipotea taratibu.
Kwahiyo hitimisho ni kuwa kitume wote ni Waislamu na Mtume Muhammad ni Muislamu wa kwanza katika ummah huu.
Sasa,kabla sijaenda nukta nyingine naomna ujibu maswali haya.
1. Ulichukua hatua gani pindi ulipo ona hilo bandiko ulilo copy na kupaste hapa ? Au logic inakufundisha uwe kama sponchi kuchukua chukua mambo mitandaoni bila kuyafanyia utafiti ?
2. Unajua kusoma Qur'aan ?
3. Kuna kitabu chochote cha Tafsiri ya Qur'aan umewahi kukisoma na kama umewahi kukisoma ni kipi ? Je hukuona maelezo na bayana juu ya aya hizo ulizo paste unazo dai zinaonyesha "Contradictions" ?
4. Kama majibu ya maswali hayo matatu hapo juu huna,je unaweza ni kwa sababu gani mimi niendelee kujadiliana na wewe juu ya kadhia na kwa sababu gani mimi nisikuite wewe mjinga tena MPUMBAVU usiye jua kama hujui na hujui kama hujui huku ukidhani unajua ?
Tumalize nukta hii kisha twende nyingine.
Nipo ...