Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Hujathibitisha Mungu yupo, unarukaruka na habari zisizo kichwa wala mguu.Kwanza jibu swali nililo kuuliza.
Kwa misingi ya mantiki huwa mnahitimisha vipi kuhusu Mbwa kwa mfano.
Kwahiyo mbwa si mnyama ? Wale wakubwa zako walio hitimisha hawakujua,hivi hakuna ufanano kati ya ng'ombe na mbwa au mbuzi au kondoo au mbweha ? Huwa naona hii logic huwa huielewi kabisa.
Hakuna anaye amini Mola akasema hajui kiumbe kilicho umba dunia. Sisi tinathibitisha uwepo wa Mola kwa njia nyingi na nimeshakutajia takribani njia tano. Yaani katika dini hakuna mambo ya logic,yaani kwenye dini ni ukweli ulio wazi kabisa. Ndiyo maana katika Qur'aan Allah anawauliza wale wanao mkana,kwa kuwaambia "Hivi wanadhani ya kuwa huu ulimwengu umetokea pasi na chochote au wenyewe ndiyo umejiumba ?" .Sasa logic yenu hapo haina nafasi sababu huo ni kweli.
Wewe tuambie tu imekuwaje mpaka hali ikawa iko hivi ilivyo ? Kwamba imetokana pasi na chochote au ulimwengu umejiumba wenyewe ? Kisha utuelezee mchakato ulikuwaje na kama hujui,sasa kwanini una kanusha juu ya uwepo wa Mola.
Swali la mwisho,hivi wakubwa zenu waliwaambia msiwe mnajibi maswali mkiulizwa ?
Thibitisha Mungu yupo.