Naanzia hapa. Msingi mama wa logic ni akili,yaani huwa mnasema wenyewe ya kuwa elimu ya Mantiki ni elimu kwayo humuepusha mtu kukosea katika kujenga hoja. Hii ndiyo maana ya Mantiki yaani kwa ufupi haishughuliki na dhati ya ukweli. Msingi huu mama unao zalishwa na mawazo na kulinganisha mambo kisha kuhitimisha,kutokana na akili ambayo haijakamilika.Mantiki ambayo husema "Wanyama wana miguu minee,mbwa ana miguu minne,basi mbwa ni mnyama". Hapa huwa mmemalza wenyewe. Sasa nitakuuliza kipi hutangulia ? Sifa au kitu husika ?vizuri umekubali tujadiliane kwenye msingi wa logic (mantiki).
Maana nje ya mantiki, hakuna kujadiliana, ni kelele tu.
Kwa sababu misingi ya kujadiliana inatumia mantiki.
Si kweli kwamba nje ya mantiki ni kelele,bila shaka utakuwa huijui Mantiki. Ndani ya mantiki kumejaa ubishi na ushabiki mtu anashikilia nadharia za kina Aristoto na kuishi nazo,yaani yeye alikosea na nyinyi mnakosea.
Siyo kweli kwamba misingi ya kujadiliana inategemea mantiki,hii ni kwa mujibu wenu,sababu mijadala ilikuwepo hata kabla ya waasisi wa logic walikuwa hawatajiki. Elimu ambayo haina hata uwezo wa kuniambia ya kuwa nikifa naenda wapi huu ni wasi wasi wa Shetani.
Hapa unadhihirisha udhaifu wa elimu ya mantiki.Ukisema Mungu ni mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote, kwa kufuata mantiki, hana tabia wala hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kufanyika.
Swali msingi gani wa mantiki umekupa hitimisho hili ? Lakini swali la msingi umejuaje hilo wakati halina kinyume chake ? Haya ni matumizi mabaya ya akili,kuna muda huwa najiuliza hivi huwa unaelewa unachokiandika au huwa unakitafakari kabla ya kukiandika ?
Naendelea....