Ukisoma katika elimu ya logic (ambayo mimi siikubali,ila nyinyi ndiyo mnaishi katika mapito hayo) inasema anaye kanusha hutangulizwa dhidi ya yule anaye sadikisha,mimi nasadikisha ya kuwa Mola yupo na ushahidi upo,ila wewe unaye kanusha unatakiwa ututhibitishie ya kuwa umejuaje kama Mola hayupo,yaani ilikuwaje mpaka ukafikia hitimisho hilo.
Wewe umejuaje kama unavyodai ya kuwa angekuwepo angeumba kila kitu kizuri ? Unajichanganya sana,yaai hilo umelijuaje wakati unadai kwamba hayupo ?
Ni vizuri umekubali tujadiliane kwenye msingi wa logic (mantiki).
Maana nje ya mantiki, hakuna kujadiliana, ni kelele tu.
Kwa sababu misingi ya kujadiliana inatumia mantiki.
Ukisema Mungu ni mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote, kwa kufuata mantiki, hana tabia wala hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kufanyika.
Ulimwengu huu unaruhusu mabaya kufanyika.
Hivyo, kimantiki, ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Na zaidi, Mungu huyo hayupo.
Kwa sababu, Mungu huyo kuwepo na kuruhusu ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo ni contradiction.
Ni sawa na kusema mama yake mzazi babu mwenye miaka sabini ni binti mdogo mwenye miaka mitano.
Hapa ni kama mimi nimekuambia hakuna binti wa miaka mitano ambaye ana mtoto wa kumzaa wa miaka sabini, kwa sababu hiyo nincontradiction ya kimantiki.
Halafu wewe unaniuliza, wewe ymejuaje huyo binti hayupo? Kama hayupo umejuaje kuwa hayupo?
Nimetumia mantiki. Mama anatakiwa kuwa mkubwa kuliko mtoto wake. Pia anatakiwa awe kafikia umri wa kuzaa. Binti wa miaka mitano hajafikia umri wa kuzaa. Pia, binti wa miaka mitano hata akizaa kwa miujiza keo, mtoti wake hawezi kuwa na miaka sabini. Hivyo hili jambo la binti wa miaka mitano kuwa na mtoto wa miaka sabini haliwezekani.
Nimetumia mantiki kujua hilo.
Hili jambo haliwezekani kufanyika, ni contradiction inayoonesha hili wazo ni kitu cha kufikirika tu.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote naye ni wazo la kufikirika tu, kiuhalisia hayupo.
Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.