Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Mimi nadhani kila mtu afuate sheria na maandiko ya imani yake, na kila mtu pia aheshimu imani ya mwenzie, ila tukisema tulazimishane kufunga ramadhan si sawa
 
Mimi nimeanza kudai uthibitisho wa kwamba Mungu yupo, toa uthibitisho huo, halafu niulize mimi nitoe uthibitisho wangu.

Siyo wewe hujajibu swali langu, unataka mimi nijibu lako.

Hiyo ni tabia mbaya.

Thibitisha Mungu yupo. Jibu swali langu.

Kisha rejea maswali yako nikujibu.
 
Mkuu kumbuka ya sungura sizitaki...........
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi tupu tu za kiimani.
Sababu zipo nyingi sana but nitakuwa nataja sababu moja moja tunaijadili hadi tufikie muafaka tukimaliza tunaendelea na sababu nyingine. Right?

Sababu ya Kwanza Ni : CONSISTENCY : Consistency is always a prove that there is a power behind.. Kuna vitu ambavyo toka dunia imeumbwa havijawahi kubadilika. Mfano. JUA/THE SUN: TOKA DUNIA IMEUMBWA JUA HUWA LINA CHOMOZA MASHARIKI NA KUZAMA MAGHARIBI. HAIJAWAHI KUTOKEA KINYUME CHAKE HATA SIKU MOJA.


Mfano wa pili ni: ALAMA ZA VIDOLE ( FINGER PRINTS) toka dunia imeumbwa Kila mwanadamu anae zaliwa ana finger prints zake yeye Kama yeye. This is a prove that there is an intelligent power behind all this. What have you to say about this?
 
Ur still a learner
 

Mnafunga au mnabadilisha ratiba ya kula.??
 
Thibitisha kwamba hakuna Mungu.
Hili hawezi mpaka anakufa,sababu wakubwa zake mpaka wamekufa hawakuwahi kuweza.

Hawa watu suala la kuthibitisha huwa wanaona ni jukumu la sisi tunao sadikisha uwepo wa Mola,wakati wanasahau katika kanuni za kimjadala yule anaye kanusha ndiyo huwa anatangulizwa kuthibitisha sababu hudhaniwa ya kuwa ana elimu na ujuzi juu ya jambo husika,lakini kichekesho ni kuwa hata wao hawajui kama wanakanusha na kutetea hoja yao hiyo hawawezi.

Sisi huwa tunawauliza tu wamejuaje kama Mola hayupo (hapa ndipo kizaa kinapoanza na hupoteana watu hawa).

Lakini kuna jambo lao lingine la kipuuzi sana,kwamba suala la Uwepo wa Mopa ni hadithi tu,ajabu wanashindwa kututhibitishia juu ya hizi hadithi ilikuwaje zikatungwa na nani wa mwanzo katika hadithi hizi.

Sasa unakuja kuhitimisha ya kuwa watu hawa wana matatizo ya akili,na hawafikirii mambo kiundani. Kwangu mimi baada ya Wanafalsafa kwa ujinga na uzwa zwa wanafata hawa wakana Mungu.

Shukrani,shida umemuuliza swali ambalo limemzidi na hana majibu ya swali hilo.
 
Kijana unatakiwa uwe muelewa,kwanza umeelewa ya kuwa mwezi muandamo ndiyo mahesabu sahihi ya nyakati kuliko ya kalenda ?

Sasa hizi nyingine sisi ndiyo tunaishi nazo.
 
Ukiongelea consistency hivyo, kwanza nitakuuliza, unajua consistency maana yake ni nini?

Nitakuambia Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba dunia ambayo inawezekana kuwa na mabaya, watu wakaumia, wakafa kwa magonjwa, watoto wasio na hatia wakauawa kwa vita na umasikini,kukawa na majanga ya kiasili kama matetemenko ya ardhi na mafuriko yanaua watu sana, si consistency.

Ni kinyume cha consistency, ni contradiction.

Umeongea kitu kizuri sana, consistency. Mungu anatakiwa kuwa na consistency, lakini anaonekana ana contradiction.

Tunaambiwa amejaa upendo na huruma, lakini anaachia watoto wasio na hatia wanakufa kwa njaa na magonjwa na majanga mengi.

Hiyo si consistency, hiyo ni contradiction.

Watu kuwa na fingerprint tofauti si ushahidi kwamba Mungu yupo, ukijua computer programming kidogo tu utajua kwamba unaweza kutengeneza dataset ya vitu bilioni nane kwa kutumia base 24 alphanumeric characters ambazo hazijirudii.

Kama unajua mchezo wa chess, zile squares 64 zinaweza ku produce 10 power 120 unique games as estimated (lower estimate at that) by Claude Shannon.

Sasa aliyebuni mchezo wa chess tu kashabuni chess games (equate that to fingerprints) nyingi zaidi ya mara 15,000 ya watu wote wanaoishi duniani kwa sasa.

Kila mtu anayeishi anaweza kucheza michezo ya chess 15,000 ya chess, kila mchezo ukawa tofauti na mwingine, na michezo ya chess ikawepo mingi tu bado haijachezwa.

Sasa ukielewa mambo kama hayo
 
Mzee baba umekuja kuchafua hali ya hewa hapa😂😂😂
Hapana mimi natoa hoja tu, sasa kushindwa kujibu hoja na kutoa tuhuma za jumlajumla ndiyo kuchafua hewa kwenyewe.

Maana bora hata kama tuhuma zingekuwa za rejareja umeniambia nimechafua hewa hapa na hapa kwa sababu hii na hii ningeweza kukupa nafasi kwamba unaweza kuwa sawa ngoja nichunguze hoja zako kama kweli nimechafua hewa. Kama nimechafua hewa kweli nijifunze usafi, kama wewe umekosea nikuoneshe ulipokosea na wewe ujifunze, ilimradi tunajifunza.

Lakini wewe ndiye mchafuzi wa hewa umekuja na ad hominem attack bila hata kugusa hoja.

Ad hominem attack ni kumshambulia mtu bila kuzungumzia hoja zake.Hii mara nyingi ni silaha ya watu waliokosa hoja, hawana hoja wanaleta viroja.

Umenikumbusha kwenye somo la saikolojia kuna habari moja inaitwa "projection".

Projection ni ile hali ya mtu kusingizia wengine tabia yake mwenyewe iliyo mbaya.

Yani mtu anajijua yeye mwizi, anaiba, halafu anawahi kusema mtu mwingine kaiba.

Yani hapa ulichofanya ndiyo hiyo psychological projection.

Ushuzi umejamba wewe, halafu unanisingizia mimi nimechafua hewa!
 
kisichopo hakithibitishiki kua hakipo, kwasababu hakipo ili kuthibitishwa hakipo!.
 
Nashauri elimu itolewe jinsi ya kufunga, kwani kila mfungo huambatana na vifo, sielewi afya ni mgogoro au ufungaji unaunyima mwili na kuvuruga mifumo yake mpaka wahanga wanafariki kipindi hiki.
Somo ulilolitoa kuhusu umuhimu wa dunia nzima kufunga pindi waislamu wanapofunga, halina mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…