Sababu za kuacha kutazama video za utupu

Sababu za kuacha kutazama video za utupu

Kwa hio we umewezaje yajua ikiwa muhusika hajui😀
Mkuu mimi nimekutana na watu wenye kadhia hiyo ambapo matatizo yao yalikuwa yanatokana na kuangalia hizo video za utupu. Hivyo nimekuja na chapisho hili ili kuwaponya watu wengi wasiangamie
 
Jobless ..hio blog unataka views matangazo yapite huko upate hela ..labda ka una blog ya raha tupu.com i will pay a visit
Ni kweli mkuu. Ukitembelea blog yangu utapata machapisho mengi ya kukujenga ambayo yatakufanya uachane na kuangalia porn. Believe you me
 
Mkuu mimi nimekutana na watu wenye kadhia hiyo ambapo matatizo yao yalikuwa yanatokana na kuangalia hizo video za utupu. Hivyo nimekuja na chapisho hili ili kuwaponya watu wengi wasiangamie
Hao watu ulokutana nao ndo unaamua kusema kuwa jamaa anatatizo yani hao wako ndo majibu ya jamaa
 
Ni kweli mkuu. Ukitembelea blog yangu utapata machapisho mengi ya kukujenga ambayo yatakufanya uachane na kuangalia porn. Believe you me
Kwan porno inabomoa nini,,, kufanya sex 3 times a day na 1 bao of nyeto which is bad🤔
 
Wiki mbili zilizopita niliandika chapisho linaloitwa Madhara na sababu za kuacha kutazama video za utupu/ngono. Chapisho hilo lilisomwa na watu wengi na wengine bado wanaendelea kusoma chapisho hilo.

Wengi waliunga mkono na kukubaliana na chapisho hilo kuwa linasema ukweli na wachache waling'aka na kupinga kuwa hakuna madhara ya kuangalia picha za utupu. Wengi waliokubaliana nami wana sababu za msingi na wale waliopinga wana sababu za msingi pia. Lakini ukweli unabaki kuwa kutazama video za utupu kuna madhara makubwa kwa mtazamaji. Na nikasema bayana kuwa, madhara ya kutazama video hizo yanakuja kwa hatua anazochokua mtu baada ya kutazama video hizo.

Inashangaza kuona watu wengi wanapinga ukweli. Ukienda Google ukatafuta madhara ya kuangalia video za utupu utakutana na taarifa chache mno zinazoeleza madhara ya kuangalia video hizo. Taarifa nyingi zinasapoti kuwa uangaliaji wa video hizo hauna madhara. Hata hivyo hatuhitaji kufuata kila ushauri unapatikana google kuwa ni wa ukweli. Sisi wenyewe tunaweza kufanya utafiti wetu na kuja na majibu sahihi na watu wengine huko duniani wakajifunza kutoka kwetu.

Sasa baada ya kuandika madhara kwenye chapisho lililopita, leo naelezea madhara yale kwa undani. Tuangalie madhara yake kwa undani.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kujichua(masturbation)

Moja ya hatua anazochokua mtu baada ya kutazama video hizo za utupu ni kujichua(masturbation). Hii hutokea kwa sababu akili ya mtu anayetazama video hizo huwa imechochewa kwa hisia na kuishia kufanya kitendo hicho. Hali ambayo kama mtu atajichua kwa siku kadhaa hugeuka na kuwa ulevi. Mtu hushindwa kuacha tabia hiyo kwa sababu akili ya bindamu hupokea kwa haraka tabia yoyote anayoijenga mtu katika mazingira yenye hisia kali.

Uki google madhara ya kujichua kwa lugha ya Kiingereza hutakuna na madhara hayo kwenye website kubwa za afya duniani. Website nyingi kubwa duniani zinataja kuwa kujichua ni afya na hakuna madhara yoyote ya mtu kujichua. Lakini wanasahau kuwa watu wengi wanaojichua huishia kukosa urijali. Visa vingi vya watu wengi kukosa urijali katika zama hizi vinasababishwa na kuangalia video za utupu. Kuna mtu atasema "amina" baada ya kusoma hapa.

Yule anayesema hakuna madhara namshauri aendelee kutazama video hizo. Punde ataona matokeo yake. Hata kama ni kwa uchache

Kuangalia picha za utupu hupelekea akili ya mtu kukosa makali(sharpness) na nguvu

Watu wengi walipinga kuwa akili ya bindamu haina makali. Ukweli ni kwamba akili ya bindamu ina makali (mental sharpness). Kuna sababu zinazopelekea akili iwe na makali imara na kuna sababu zinazopelekea mtu kuwa na akili yenye makali butu. Moja ya sababu kubwa ya kufanya akili iwe na makali butu ni kutazama video za utupu. Ndiyo waangaliaji wengi huishia kuendelea kuangalia video hizo kwa sababu ya kushindwa kudhibiti akili zao kuacha tabia hiyo. Hii ni kwa sababu akili zao zinakuwa tayari zishazoea

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa nguvu za mwili

Baada ya mtu kutazama video hizo hupelekea mtu huyo kujichua. Mtu huyo akijichua hupelekea kukosa nguvu za mwili. Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa kiwango cha mtu kukosa nguvu za mwili kutokana na kujichua ni tofauti na kiwango cha mtu anayekosa nguvu kutokana na kufanya tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu kitendo kimoja ni kinyume na asili ya mwanadamu na kitendo kimoja ni asili kwa binadamu.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa hali ya kujiamini.

Watu wengi wanaotazama video za utupu hukosa hali ya kujiamini kwao wenyewe na kwa jinsia tofauti. Hii ni kwa sababu wengi huwa ni watu wa ndani sana na siyo watu wa kutoka nje, kuchangamana na watu wengine. Hata hivyo uwezo wa kuongea na jinsia tofauti hujawa na wasiwasi mkubwa kwa watu hawa.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa nidhamu binafsi.

Nidhamu binafsi niyuwezo wa mtu kujiamulia kufanya jambo fulani na muda ukifika wa kufanya jambo hilo mtu ana anza kufanya jambo hilo. Ana anza kufanya jambo hilo bila kujali kama anajisikiaje au kuna hali gani. Mtu anaye tazama video hizo hukosa nidhamu ya kuacha kutazama video hizo. Hata kama atapanga kuwa kesho ata acha tabia hiyo, lakini kesho ikifika utakuta ana tazama tena. Hii ni kwa sababu ya kukosa nidhamu. Na mtu akikosa nidhamu kwenye eneo mojawapo, basi na maeneo mengine hukosa nidhamu.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukwepwa na watu wa jinsia tofauti.

Akili ya binadamu huvutia mtu mwenye nishati sawa au zaidi. Mtu aliyemaliza nishati yake kwa kujichua kwa sababu ya kuangalia video za utupu huondoa mvuto wa asili ambao ndiyo humfanya mtu apendwe na jinsia tofauti.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo

Watu wengi
wanaotazama video za utupu hutazama siyo kwa sababu wanapenda kutazama video hizo. Hutamani sana kuacha tabia hiyo ya ulevi wa kutazama video hizo lakini hushindwa kuacha. Hali ambayo hupelekea watu wengi kuwa kwenye msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huja pale ambapo mtu alijiapiza kuwa ataacha kutazama video hizo lakini akaishia kutazama tena.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kuwa na afya dhaifu

Chizi mapenzi(sex madman) huwa na afya dhaifu. Hii ni kwa sababu ya kuendekeza sana. Wengi ya wanao jichua huishia kuwa na afya dhaifu kwa sababu nguvu na nishati nyingi hupotezea kwenye kujichua hali ambayo hupelekea kuwa na afya dhaifu.

Ninacho taka kukuambia ndugu msomaji ni uache kutazama video hizo hazina faida kwako yoyote. Hazina faida kiakili, kimwili na kiroho. Zaidi zina kuharibu kimwili, kiakili na kiroho. Hutajua una nguvu kiasi gani kimwili, kiakili na kiroho mpaka utakapo acha tabia fulani usiyoipenda.
 
Kuna kijana hapo utaskia ngoja nipige ndo nisome hili bandiko😆🤣🤣🤣
BTW Hili janga limefika hadi kwa Bi Mkubwa, si umeskia amewaambia wizara ya Afya "wakalitizame" suala la "Udongo wa Congo", source ni nyeto tuu
 
Back
Top Bottom