Apeche alolo
JF-Expert Member
- Apr 14, 2023
- 2,517
- 5,533
Mtasumbuka sana kwanini sasa kwani kabla ya hapo mlikuwa hamumwoni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unawaza kula tu !Waliomponza ni wasaka tonge
Sio issues za kuvunjika Kwa Plea Bargain Tena?Trial de novo, utuhumiwa wake unaanza upya.View attachment 2691993
Ccm huyounawaza kula tu !
Chadema jipangeni kupiga kampeni vizur mwakani Kwa vijana. Tunieni vijana kuwa fursa hasa kwenye ajira. Sio kuleta blah blah blah za bandari hamtoboiKwani hata kama ni Bandari siyo sehemu ya Tanganyika? Kuuza Kipande cha nchi ni kuuza nchi.
Kumbe yalikuwa ni makosa yake ya nyuma, mwenyewe nikadhani ni maoni yake kuhusu bandariMnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo.
Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu (Anti Money Laundering Act).
Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na Serikali (Pre Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.
Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka.
Baadaye alifungua kesi katika Mahakama Kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Ndipo alifungua shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini Mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano (Plea Bargaining) zilifanyika sawa.
Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo Mahakama ilisikiliza hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.
Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.
UPOTOSHAJI:
Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.
Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa. Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.
Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba Mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.
Pia soma Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP