Sababu za kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo.

Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu (Anti Money Laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na Serikali (Pre Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

Baadaye alifungua kesi katika Mahakama Kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini Mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano (Plea Bargaining) zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo Mahakama ilisikiliza hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa. Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba Mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.

Pia soma Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP
Nashukuru kwa taarifa
 
HISTORIA FUPI

Tarehe 14/05/2020 wakili Peter Madeleka alishitakiwa kwa makosa 10 ya uhujumu uchumi katika Economic Case No 40/2020 Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Aliandika barua kwa DPP akiomba makubaliano ya kukiri kosa (Plea Bargain) ambayo ilikubaliwa hivyo akaingia plea bargain ambapo walikubaliana kuwa atakiri kosa dogo zaidi ili aachiwe.

Baadaye wakili Peter Madeleka alipeleka maombi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga makubaliano ya kukiri aliyoingia akidai kwamba alilazimishwa na yalikuwa yamegubikwa na ukiukwaji mkubwa wa kisheria hivyo akaomba yatenguliwe . Baada ya kusikiliza kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilitupilia mbali maombi hayo na kuamua kuwa makubaliano hayo yalikuwa halali na huru kwa mujibu wa sheria.

Ndiposa Madeleka akakata rufaa kuja Mahakama kuu dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyokataa kutengua makubaliano ya kukiri kosa (Plea Bargain) kati yake na DPP.

MABISHANO YA HOJA MAHAKAMA KUU

Maombi ya msingi ya Peter Madeleka Mahakama kuu yalikuwa Mahakama kuu itengue makubaliano ya kukiri kosa yaani Plea Bargaining na iamuru Peter Madeleka aachwe huru.

1. Hoja ya Kwanza ya Madeleka ni kwamba makubaliano ya kukiri kosa baina yake na DPP yalikiuka sheria inayotaka kuwa kama plea bargaining itahusisha malipo ya fidia kwa serikali basi pesa za fidia zilipwe kwa Treasury Registrar na si vinginevyo. Katika makubaliano yake na DPP Peter Madeleka aliambiwa alipe pesa kwenye akaunti ya DPP iliyopo Benki kuu badala ya kwa Registrar.

Akijibu hoja hii wakili wa serikali alisema akaunti ya DPP pesa zilipowekwa siyo mali yake binafsi bali ni akaunti ya serikali hivyo nayo ipo chini ya Treasury Registrar. Pia haoni ni jinsi gani Madeleka aliathirika kwa kulipa pesa kwa DPP badala ya Treasury Registrar.

2. Hoja nyingine ni kwamba alihukumiwa kwa kosa dogo ambalo hakushtakiwa. Kwa mujibu wa Madeleka baada ya Plea Bargaining DPP alitakiwa kumshitaki kwa kosa dogo ili akiri kosa lakini kilichofanyika ni DPP kuondoa mashitaka bila kumshitaki kwa kosa dogo hivyo kupelekea yeye kukiri na kuhukumiwa kwa kosa asiloshitakiwa nalo.

Akijibu hoja hii wakili wa serikali alisema upande wa mashitaka unao uwezo wa kubadilisha mashitaka na kwamba kama Madeleka hakuridhika na kosa dogo angekataa kukiri na angejitoa kwenye makubaliano hayo.

3. Hoja nyingine ni kwamba hakupatiwa ushahidi wa kosa alilokiri kama sheria inavyotaka.

Akijibu hoja hii wakili wa serikali alisema hoja hii ni mpya kwani haikuwepo kwenye maombi mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi.

4. Hoja nyingine ni kwamba fine na fidia zilipaswa zilipwe kwa waathirika wa uharifu na siyo kwa serikali.

Akijibu hoja hii wakili wa serikali alisema sheria hailazimishi pesa kulipwa kwa waathirika wa kosa hivyo anaweza kulipa kwa Serikali au waathirika.

UAMUZI WA MAHAKAMA

Mahakama kuu imekubaliana na hoja moja tu kwamba mtuhumiwa hakupatiwa ushahidi wa kosa alilokiri hivyo imetengua makubaliano ya kukiri kosa baina ya Madeleka na DPP na kuamuru kesi yake ya uhujumu uchumi isikilizwe upya.

My Take

Kuna utata nauona katika uamuzi wa Jaji kwanza kwa hoja zingine za Peter Madeleka zilizokataliwa.

Pili, kuhusu je nini kinatakiwa kifuate baada ya makubaliano ya kukiri kosa kutenguliwa, Je kesi ya msingi inaendelea au mtuhumiwa anaachiwa huru?
Napendekeza Madeleka akate rufaa ili tupate busara ya Mahakama ya Rufani.
 
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo.

Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu (Anti Money Laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na Serikali (Pre Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

Baadaye alifungua kesi katika Mahakama Kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini Mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano (Plea Bargaining) zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo Mahakama ilisikiliza hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa. Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba Mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.

Pia soma Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP
Nina mashaka na uelewa wako kwahiyo rufaa zote una maana wakili alikuwa anapambania awekwe ndani? Acheni kujitoa ufahamu hayo mambo mnayofanyanya alishafanya Magufuri na sasa hivi Yuko kaburini.
 
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo. Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu ( Anti Money laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na serikali ( Plea Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa mkurugenzi wa mashtaka.

Baadae alifungua kesi katika mahakama kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano ( plea bargaining )zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo mahakama ilisikiliza Hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa.
Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.
 
[emoji28]wewe mkuu unaelekea wapi!
 
cku zote msikamate, ccm muwe na aibu
 
Naunga mkono hoja
 
Taarifa ya sasa kutoka Arusha zinaeleza kwamba Madeleka ambaye amegeuziwa kibao na serikali ya Tanzania na kufunguliwa upya kesi ya uhujumu uchumi , baada ya kujitokeza hadharani kupinga Mkataba unaotia aibu wa Bandari na DP WORLD , ataendelea kusota kwenye gereza la Kisongo hadi tarehe 31/07/2023 kesi yake itakapotajwa tena .

Haya yameelezwa na Wakili wake , Simon Mbwambo alipoongea na Waandishi wa Habari .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
 
Nchi ya mauzauza hii, tutaona mambo mengi sana hasa ktk kipindi hiki cha majadiliano
 
Wanasiasa wamemponza mwenzao,wao wanalala na wakezao yeye anaenda lala na Nyapala
 
Taarifa ya sasa kutoka Arusha zinaeleza kwamba Madeleka ambaye amegeuziwa kibao na serikali ya Tanzania na kufunguliwa upya kesi ya uhujumu uchumi , baada ya kujitokeza hadharani kupinga Mkataba unaotia aibu wa Bandari na DP WORLD , ataendelea kusota kwenye gereza la Kisongo hadi tarehe 31/07/2023 kesi yake itakapotajwa tena .

Haya yameelezwa na Wakili wake , Simon Mbwambo alipoongea na Waandishi wa Habari .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
iT IS A PITY KUWA SAMIA NARUHUSU HAYA!
 
Trial de novo, utuhumiwa wake unaanza upya.
Screenshot_20230718-140022.jpg
 
Back
Top Bottom