Katika hili ninakubaliana na kukamatwa kwake, wasiwasi wangu bado upo kwa serikali na jeshi la polisi kukandamiza watu wanaotaka kufanya maandamano ya amani, kwanini serikali kupitia jeshi la polisi inakataza watu kutumia haki Yao ya kikatiba?.
Serikali yetu imeendelea kuwa kandamizi bila sababu za msingi, Mugufuli aliminya uhuru wa raia na watu wengi Sana waliumizwa katika utawala wake, japo kidogo mambo yamebadilika, lakini kwa kiasi kikubwa vyombo vya Dolla havijabadilika.
Kukamatwa kwa Mbowe na kuwekwa ndani kwa zaidi ya miezi 8, kukamatwa kwa Mdude huko Mbeya, Serikali kupuuza kufuatilia na kuchunguza tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lisu hata baada ya yeye kurudi nchini, ukizingatia kwamba serikali ilikataza watu kufanya mikutano ya kumchangia alipokua amelazwa hospital huko Nairobi, ni dalili za wazi kwamba serikali inahusika na matukio yote hayo.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app