Sababu za Msingi kwanini Bomba la mafuta Uganda lipite Bandari ya Tanga

Sababu za Msingi kwanini Bomba la mafuta Uganda lipite Bandari ya Tanga

kmkm ni kikosi cha jeshi linalotambulika kama ilivyo jkt ilivyo chini ya JW.
Jeshi lina vikosi ndani yake, lakini kikosi hakina jeshi ndani yake. Ndiyo maana kwenye ile kesi kina juma Duni waliambiwa hawawezi kuipindua SMZ kwa kuwa siyo dola, sasa jiulize sifa za dola ni zipi kama mojawapo si kuwa na Jeshi?
 
urasimu ni tatizo kuu sana ,ifike mahali watu wawe na maamuzi ya haraka kwa kujali maslahi ya nchi,urasimu wa mfumo wa utawala na utoaji wa maamuzi ya haraka hapa ndipo kwenye mtego .suala la kutoa maamuzi ndani ya wiki litachukua miezi kadhaa wenzetu hutumia hizi weakness za mfumo kutoa maamuzi ya haraka na kuhamisha miradi mikubwa kwao ,tuna safari kuelekea kwenye upebari na kukabiliana na makabaila hawa wazoefu katika dili kubwa ,
 
Kwahiyo watu wanatoana jasho kwa mradi ambao hautatulipa?? Wakenya mpaka wanashusha propaganda kibao na kutuma mashushushu kwa mradi ambao hauna faida yeyote??? Duuuhh angefanya Lowassa au Ukawa haya yangesifiwa..
Mkuu, dunia ya sasa unapaswa kutumia akili sana kutafakari mambo, swala kwamba kuna propaganda nyingi zinaweza kuwa siasa tu za mganda kuharakisha maamuzi sababu wanatujua sis watanzania tulivyo. Mkenya inasemekana aligundua mafuta, strategically hawezi kukubali bomba lipite kwake labda kama reserve sio kubwa, sababu ya kuhofia price war sababu nae ataexport. Hizo sarakasi inawezakana ziko makusudi kutuhadaa tufanye maamuz bila kujua faida muhimu. Sis tuna advantage hatuihitaji pressure. Tayari tuna bomba la Tazama tunaweza kuanzia kufanya economic analysis, japokuwa lile sio source ya export. Mambo ya ukawa unayaleta wewe na waliokutuma, viongozi wa Tanzania wametuweza sababu wamefanikiwa kutugawa ili tufikirie kwa mlengo wa vyama ili wao waendelee kupiga dili.
 
Tanzania italipwa ushuru wa UD$14 kwa pipa, kwa siku yatapitishwa mapipa laki mbili hivyo kwa mwaka Tanzania itavuna US$ bilioni moja, kumbuka mauzo ya nje ya Tanzania ni US$ bilioni tano, hivyo itaongeza mapato yetu ya kigeni kwa 25% na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Tanzania kutoka katika nchi masikini na kuwa nchi za uchumi wa kati itakopesheka kiurahisi badala ya sasa inapewa misaada kiduchu kama msaada wa vyandarua na dawa za kuua kunguni. Pia kitakuwa kichocheo cha biashara zaidi kumbuka Tayari serikali imetoa offer ya bandari kuwa maalumu kwa mizigo ya Uganda na upo uwezekano wa kutumika hadi sudan ya kusini.
Naomba kuuliza mtaalamu wa uchumi kupitia bandari ya tanga kwa bomba la mafuta kwenda uganda unaweza fika uchumi wa kati yani huo uchumi wa kati unakuaje au ni figure tu tunapanga mana nimesikia kupitia gesi inaweza kutufikisha uchumi wa kati kwa kuuza umeme nje ya nchi au tunatumia akili kudanganya akili nyingine naomba ufafanuzi mana tazama aijatufikisha uko utalii ndo inatupoteza kabs madini ndo yanatuweka gizani je ilo bomba na utaratibu wake itatufikisha wapi sijui vizur uchumi sorry ni shwali mi sio mwanauchumi ndo mana nimekufata kuona kama umeongea interested things uchumi wa kati i like dat mister/miss
 
Bado ni zaidi ya hapo, kama ulimaanisha Domestic revenue, kwa mwezi tu karibia 1.5Tril. Refe (Wazir wa Fedha)Kama ulimaanisha GDP ni karibu Trilion 100. (IMF)
Mkuu unaongelea hii mpya ambayo haijawa audited, mie naongelea kwa refference ya bajeti ya Mkwerre
Mkuu, kuna trip down effect chungu mzima, na buckward linkage za kutosha labda tuanzishe topic nyingine ya kukuelewesha faida ya huu mradi ila najua wakenya wanaweza wakafa kwa kihoro.
Ni kweli mkuu unayoyasema.
Nimesahau pia kuku acknowledge hapo juu kwa mchango wa mawazo yako,knwenye ule uzi mwingine.

Nchii hii tukikaa vizuri tutafika tu aiseeeee
 
Naomba kuuliza mtaalamu wa uchumi kupitia bandari ya tanga kwa bomba la mafuta kwenda uganda unaweza fika uchumi wa kati yani huo uchumi wa kati unakuaje au ni figure tu tunapanga mana nimesikia kupitia gesi inaweza kutufikisha uchumi wa kati kwa kuuza umeme nje ya nchi au tunatumia akili kudanganya akili nyingine naomba ufafanuzi mana tazama aijatufikisha uko utalii ndo inatupoteza kabs madini ndo yanatuweka gizani je ilo bomba na utaratibu wake itatufikisha wapi sijui vizur uchumi sorry ni shwali mi sio mwanauchumi ndo mana nimekufata kuona kama umeongea interested things uchumi wa kati i like dat mister/miss
Kabla ya gesi tulihitaji "per capita" ya us$ 30 tu, sasa ukiunganisha na gesi lazima tuvuke, ni suala la BOT kuiweka vizuri kwenye mahesabu ya uchumi wetu.
 
Mkuu, kuna trip down effect chungu mzima, na buckward linkage za kutosha labda tuanzishe topic nyingine ya kukuelewesha faida ya huu mradi ila najua wakenya wanaweza wakafa kwa kihoro.
Mi nasubir tu nione sina la kusema...hebu waiter lete maji baridiii!
 
Mkuu, dunia ya sasa unapaswa kutumia akili sana kutafakari mambo, swala kwamba kuna propaganda nyingi zinaweza kuwa siasa tu za mganda kuharakisha maamuzi sababu wanatujua sis watanzania tulivyo. Mkenya inasemekana aligundua mafuta, strategically hawezi kukubali bomba lipite kwake labda kama reserve sio kubwa, sababu ya kuhofia price war sababu nae ataexport. Hizo sarakasi inawezakana ziko makusudi kutuhadaa tufanye maamuz bila kujua faida muhimu. Sis tuna advantage hatuihitaji pressure. Tayari tuna bomba la Tazama tunaweza kuanzia kufanya economic analysis, japokuwa lile sio source ya export. Mambo ya ukawa unayaleta wewe na waliokutuma, viongozi wa Tanzania wametuweza sababu wamefanikiwa kutugawa ili tufikirie kwa mlengo wa vyama ili wao waendelee kupiga dili.
hahahahahahahaha MK254 njoo umsome huyu msomi hapa...
 
Kabla ya gesi tulihitaji "per capita" ya us$ 30 tu, sasa ukiunganisha na gesi lazima tuvuke, ni suala la BOT kuiweka vizuri kwenye mahesabu ya uchumi wetu.
Ok naona ukuti ukuti unaendelea mi sio msiasa ni mtanzania mungu bariki kwangu naona itakua imeokoa vifo barabarani na uaribifu wa road zetu ndo faida kubwa naomba kuongeza uchumi tupate izo dola kaka waambie na zambia tanzania iongeze nguvu uchumi uchukue kasi ya ndege au magnetic train mzee salute uchumi wa bongo lets give them a chance tu prove
 
Swala sio technical analysis kwa nin bomba lipite kwetu,issue ni economic benefit gani tutapata kama nchi? hii issue imebebewa bango sana sasa cjui ni kusahaulisha watu mambo ya zanzibar au kuna ukweli wowote.

nenda kasoma press release iliyotolea na gerson msigwa au ile iliyotolewa siku wamekutana magufuli na mseven kule arusha kila kitu kimeelezwa
 
urasimu ni tatizo kuu sana ,ifike mahali watu wawe na maamuzi ya haraka kwa kujali maslahi ya nchi,urasimu wa mfumo wa utawala na utoaji wa maamuzi ya haraka hapa ndipo kwenye mtego .suala la kutoa maamuzi ndani ya wiki litachukua miezi kadhaa wenzetu hutumia hizi weakness za mfumo kutoa maamuzi ya haraka na kuhamisha miradi mikubwa kwao ,tuna safari kuelekea kwenye upebari na kukabiliana na makabaila hawa wazoefu katika dili kubwa ,
Mkuu ukiona sehemu kuna urasimu sana ujue kuna mianya ya rushwa mingi.
Urasimu mwingi huwa ni wa kutengeneza na leongo ni kujenga mazingira ya wakubwa kupiga hela, bahati nzui tumpata Magu hapendi hizi mambo za Rushwa na kujuana juana kimtandao, tunaweza fika mbali sana
 
Jeshi lina vikosi ndani yake, lakini kikosi hakina jeshi ndani yake. Ndiyo maana kwenye ile kesi kina juma Duni waliambiwa hawawezi kuipindua SMZ kwa kuwa siyo dola, sasa jiulize sifa za dola ni zipi kama mojawapo si kuwa na Jeshi?
JF bhana badala wajadili hoja kuu, wamejikita katika majeshi au nia nikumfafanulia nani? iwe ni kikosi, kikundi,jumuiya,shirikisho, nk (Hoja siyo kupata tafsiri) kikubwa uwepo wao uanaongeza usalama wa bandari ya Tanga. KWISHA.
 
Sina tatizo na muhongo toka mwanzo tatizo anaemtumia muhongo bado anaendelea kumtumia sasa ilo tatizo kwan wale wote walioona account ya scrow ni dili na kuunga mkono afukuzwe na leo wanaunga mkono kua jamaa jembe ndo mana wapinzan walisema tatizo ni mfumo mzima ndo mbovu kwa maana kuna watu wako pemben ndo wanachezesha picha na ndo untouchable so we yeyote atachezeshwa kwa nyimbo zao naona sasa yanaendelea inabidi akili ya ziada kutuamsha watanzania naona kizazi cha musa alichokitoa misri ndo kimepitia kwetu kila siku tunchonga miungu ya kuabudu musa akija tunaitupa
 
Nkibali pro muhongo kwa utaifa ni genge dogo sana kwa maslahi yao binafsi ndo waliokuwa wakimsakama kwa kasfa
 
Hongera sana Professor Muhongo, Dr. James Mataragio na timu yako kwa kulitetea taifa na nimepenyezewa ubuyu kuwa mambo sasa safi, Bomba ni confirmed linapita Tanga.

Miongoni mwa hoja mlizozijenga kwa mama Irene Muloni na msafara wake kutembelea bandari ya Tanga ya kwa nini wajenge bomba lao kupitia Tanzania na si Kenya ni hzi.

1. kina cha bandari ya Tanga kina urefu wa zaidi ya mita 40 wakati meli za mafuta zinahitaji mita 18 hivyo kuwa bandari salama zaidi kwa meli za mafuta. tofauti na Lamu ambapo kina chake ni kifupi mno, hivyo inabidi kuongeza kina kwa kuchimba zaidi.

2. Bandari la Lamu ina mawimbi makubwa mno, kutokana na kutokuwa na visiwa vya pembezoni mwake vinavyopakana nayo, upepo toka bahari za mbali unavuma moja kwa moja mpka bandarini, sio salama kwa meli ya mafuta ukilinganisha na bandari ya Tanga iliyoko katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja hivyo haina mawimbi makubwa na kuwa salama zaidi kwa meli za mafuta ambazo huhitaji utulivu wa hali ya juu wakati wa kupakia shehena yake ya mafuta kwani huchukua siku nyingi sana kupakia mzigo na inahitaji utulivu sana.

3. Bandari ya Lamu iko mpakani na Somalia hivyo nirahisi kwa meli za mafuta kutekwa na maharamia ya kisomali wakati Tanga ipo katikati ya Zanzibar na Bara hivyo kuna doria za jeshi la Tanzania na vikosi vya Zanzibar hivyo sio rahisi kuvamiwa na maharamia.

4. Tanga tayari kuna miundombinu ya mafuta tofauti na Lamu inabidi ijengwe. Pia vifaa vya ujenzi vitashuka Tanga na kwenda site moja kwa moja ,tofauti na Kenya vifaa itabidi viteremshwe mombasa na kusombwa kwa maroli kwenda site.

5. Tanzania imetoa ofa ya kutenga bandari ya Tanga kuwa mahususi kwa mizigo ya Uganda na tayari kuna miundombinu ya reli na barabara ambapo Lamu hakuna reli wala barabara ya kwenda huko.

Maelezo haya yaliwaridhisha na Irene Musoni na team yake wameahidi kutuma wataalamu baada ya wiki mbili kukagua njia zitakazotumiwa kupita bomba la mafuta.

Naona katoa muda wa kwenda kumueleza Uhuru kuwa dili limebuma.

>>Much Respect kwako Mukulu kwa "kichwa ngumu" hakuna ile mambo ya kuwa soft soft, ume prove kwa watanzania kuwa wewe ni Ngosha kweli
>>Much respect kwako Silent Killer Professor Muhongo kwa umafia kwa kimya kimya ulioufanya, umelibeba taifa.
>>Much respect kwako balozi Mahiga kwa Economic Diplomacy na Intelligence iliyotukuka.
>>Much Repect kwako Mataragio kwa agressiveness yako kuu kwa hawa manyang'au.
NB:

Nachowaomba serikali yangu sikivu ni kuona namna ya ku-mjoin South Sudan katika bandari ya Tanga awe na ka-portion kake pale maana itamuhakikishia fursa ya kupunguza hustling anazopata kwa sasa, hasa ukizingatia Mkenya hanaga jema kwa mtu zaidi ya kuangalia maslahi yake.
Lakini pia mpige hatua mbele zaidi ya kuangalia namna ya kumuamsha Mganda katika usingizi mzito alio nao wa namna ya kuichangamkia South Sudan ili iwe partner wake kiuchumi kwa kupitisha bomba lake la mafuta Uganda kuja Tanga maana hio itamuongezea mapato Uganda pia tofauti akizubaa bomba likapitia Kenya, Uganda hatapata hata mia
Mawazo tofauti. Utafiti wa bomba la mafuta ulianza kitambo kidogo. Mimi nipeleke pongezi zangu kwa rais JPM kwa msimamo wake wa kiutendaji ambao umefanya waganda wabadili msimamo wao wa awali wa kupitisha bomba Kenya na nadhani hata ule umoja wao utatu uliojengeka wa Kagame, Kenyata na Mseveni ambao uliibagua Tz sasa umesambaratika.
 
  1. Waingereza wanasema "don't count your chickens before they are hatched ". Wengi hapa wanakokotoa na kupanga mapato kana kwamba tumeshawekeana mkataba na Uganda. Kuna uwezekano kwamba bomba litapita kwetu , lakini linaweza bado lisipite kwetu. Uhuru could make Uganda an offer they can't refuse.
  2. Yapo madhara ya mazingira yanayoweza kuletwa na bomba la mafuta. Factor that in. Don't look at the benefit only, consider costs - environmental damage in this case - also.
  3. Kuna uzi humu jukwaani unasema bomba la gesi lilitumia gharama kubwa sana per kilometer, ukilinganisha na ujenzi uliofanyika nchi nyingine kama Pakistani. Sasa si watu walewale wamo kwenye huu mradi wa sasa? Kama wana asili ya kudai asilimia 10 si wataendelea kufanya hivyo?
 
Mkuu inabidi uelewe kuwa tozo ya kupitisha pipa moja kwa katika ardhi ya nchi nyingine ni $14 na Uganda inapitisha mapipa 200,000 kwa siku maana yake kwa mwaka serikali inaingiza zaidi ya Trillioni 2, na hio ni fedha ya kigeni kwa haraka haraka ni US Dollars.
Pia ukumbuke pato la ndani kwa mwaka kwa serikali kwa sasa ni almost Trillioni 4 maana yake pato la ndani litakua limeongezeka kwa 50%, sasa hapo huoni hio faida??

Kumbuka pia kama tukipwa dollar hizo maana yake shillingi ya Tanzania dhidi ya Dollar ya mmarekani itaimarika sana na hivyo kutupa advantage katika maununuzi ya nje.

Kiuchumi hii kitu ina faida sana.
Kama umekokotoa vizuri hesabu zako hilo pato si haba.
 
Back
Top Bottom