Sababu za Simba kushinda Jumamosi ni hizi hapa. Yanga acheni Polimi Lai!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Simba Jumamosi saa 10 jioni itacheza mchezo wake wa Nusu Fainali dhidi ya Wydad. Simba itashinda mechi hiyo kwa sababu zifuatazo.

1. Simba haina cha kupoteza kwenye mechi hiyo kwa ivo itacheza kwa kila njia bila ya kuwa na hofu ya kufungwa.

2. Simba haina tena shinikizo kwenye Ligi ya ndani kwani kwa vyovyote vile mwakani tena itashiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

3. Wachezaji wa Simba wengi sana sasa hivi wana dhamira ya dhati kabisa kupambana kwa ajili ya timu yao.

4. Kucheza uwanja wa Nyumbani kunawapa Simba deni la kuzuia kuaibika mbele ya Mashabiki wake.

5.Kocha wa Simba ameonekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutumia mbinu kucheza kitimu kuliko kumtegemea mchezaji mmoja mmoja.

6. Simba ndiyo Klabu Pekee ya Soka Tanzania ambayo ina rekodi nzuri sana ya kuzishinda timu ngumu za Uarabuni kwenye wakati wa shinikizo. Kadri shinikizo linavyokuwa kubwa ndivyo simba inavyokuwa imara zaidi kupambana na timu toka Afrika ya Kaskazini.
 
Kwenye mpira mambo yasiyotarajiwa hutokea. Nani alijua Yanga ingefungwa na Ihefu kwenye Ligi Kuu Tanzania!?
 
Hawajacheza acha uongo weka kikosi cha morroco World Cup ambacho kina wachezaji tisa wa wydad
 
Kila mwaka robo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…