Sababu za wanafunzi wa kizazi hiki kufeli masomo ni hizi hapa

Suala la umri na lugha ndio huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya mitihani yao. Tukitumia kiswahili kwa ngazi zote za elimu, tutakuwa na mafanikio makubwa
 
Yeap naona sasa shule kibao.
 
Mkuu unahoja nzuri na zenye manufaa kwa wazazi na hata jamii yetu.....ila wengi humu Jukwaani wanasubilia story tu za sisiemu vs chadema....... huwezi kuona kwenye hizi Thread za Ustawi wa jamii
 
Suala la umri na lugha ndio huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya mitihani yao. Tukitumia kiswahili kwa ngazi zote za elimu, tutakuwa na mafanikio makubwa
umri ni kiwango cha kimataifa (miaka 5) na mtoto anakuwa na uelewa mzuri tu wala siyo shida.

Sema lugha ndiyo inasumbua
 
Asante kwa maboresho mkuu. Ni kweli kabisa haya nayo yanachangia kufeli kwa kiasi kikubwa sana.
 
kwa hiyo mkuu ulitaka mahitaji ya shule kama notes yapatikane kwa ugumu? kama zamani
Sikuwa na maana hiyo mkuu. Maana yangu ilikuwa kwamba kila kitu kupatikana kibwerere kunakifanya kikose thamani.
 
Ili mtawaliwe kila his lazima mfanywe wajinga
Lengo la Serikali sio watoto wapate maarifa bali wahitimu, ndo ma'ana vyumba vya madarasa vinajengwa ila Walimu hawahajiriwi, vitabu havinunuliwi, watoto hawana mtihani wa mchuujo

Zamani Shule zilikuwa chache, wanafunzi wachache bali kulikuwa na mitihani ya mchuujo, leo Shule nyingi, wanafunzi wengi, Walimu wachache(students teacher ratio) hakuna mchuujo! Jiongeze
 
umri ni kiwango cha kimataifa (miaka 5) na mtoto anakuwa na uelewa mzuri tu wala siyo shida.

Sema lugha ndiyo inasumbua
Umri ni tatizo kwa namna mbili mkuu:
1. Mtoto anakuwa hatilii maanani masomo kwa sababu bado akili zake ni changa hazijang'amua umuhimu wa elimu.
2. Mtoto akiingia sekondari akili zake bado zinakuwa changa haziwezi kumudu ugumu wa masomo na lugha.
 
Mi nadhani sio lazima wote wanaosoma wafaulu,wengine wanapaswa tu kupewa elimu labda ya balanced diets, kujua umuhimu wa matunda katika mwili ili akitoka hapo aende akawe soko la bidhaa hiyo huko mbele,na maisha yaendelee katika circle hiyo.
Hiyo balanced diet imetumika kama mfano,
Umeongea kitu ambacho only few will understand.
 
Umri ni tatizo kwa namna mbili mkuu:
1. Mtoto anakuwa hatilii maanani masomo kwa sababu bado akili zake ni changa hazijang'amua umuhimu wa elimu.
2. Mtotot akiingia sekondari akili zake bado zinakuwa changa haziwezi kumudu ugumu wa masomo na lugha.
Kuhusu namba 1, mbona watoto nchi za Ulaya wanaanza miaka 5 na baadae wanaendeelea vizuri tu? Kuelewa umuhimu wa elimu inakuwa ni pole pole kila anapojifunza.

Hakuna hicho kitu kuwa akili changa hawezi kumudu ugumu wa masomo na lugha, muhimu mtaala uwe wa kueleweka tu.
 
Hivi mnatambua kwamba mitihani ya kubet hata SUA Chuo kikuu ipo mpaka ngazi ya masters?
 
Ngono ni sababu nambari moja ya wanafunzi kufeli masomo sio shule za chini hata kule vyuoni. Tutalaumiana sana lakini mwisho tutaelewana tu
 
Suala la umri na lugha ndio huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya mitihani yao. Tukitumia kiswahili kwa ngazi zote za elimu, tutakuwa na mafanikio makubwa
Bado unatengeneza tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…