Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeap naona sasa shule kibao.Mimi nadhani wakati wako unaousema( sijajua miaka ipi), nafasi za kujiunga sekondari zilikuwa chache sana.waweza kuta ndani ya wilaya moja ziko shule mbili au tatu.
Kwa hiyo kwa tafsiri ya sasa,waweza kuta kipindi hicho,alama mlizopata,mlifaulu ila nafasi ya kujiunga sekondari zikawa chache,wakaenda wachache
umri ni kiwango cha kimataifa (miaka 5) na mtoto anakuwa na uelewa mzuri tu wala siyo shida.Suala la umri na lugha ndio huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya mitihani yao. Tukitumia kiswahili kwa ngazi zote za elimu, tutakuwa na mafanikio makubwa
Asante kwa maboresho mkuu. Ni kweli kabisa haya nayo yanachangia kufeli kwa kiasi kikubwa sana.Nakubaliana na mtoa maada karibu hoja zote lakini niboreshe na kuongeza sababu.
Kuhusu sababu namba Saba naboresha Kwa kuongeza maneno kuwa wanasiasa kuingilia KAZI na majukumu ya waalimu.
Nyongeza 1. Upungufu wa walimu.
2.Utoro wa Wanafunzi, kuna wanafunzi wanaweza kukaa miezi miwili kuhudhuria shule lkn wanahudhuria kufanya mtihani.
Hizi shule za St Kayumba ni shida sana kwa kweli😀😀😀Sasa kila mtoto anafikiria kukata mauno, kuwa mbongo fleva
Kuna kufaulu kweli...
Vichwa vyao vimejaa mambo ya miziki tu
Ova
View attachment 2477232
Umri ni tatizo kwa namna mbili mkuu:umri ni kiwango cha kimataifa (miaka 5) na mtoto anakuwa na uelewa mzuri tu wala siyo shida.
Sema lugha ndiyo inasumbua
Hiyo balanced diet imetumika kama mfano,Mi nadhani sio lazima wote wanaosoma wafaulu,wengine wanapaswa tu kupewa elimu labda ya balanced diets, kujua umuhimu wa matunda katika mwili ili akitoka hapo aende akawe soko la bidhaa hiyo huko mbele,na maisha yaendelee katika circle hiyo.
Kuhusu namba 1, mbona watoto nchi za Ulaya wanaanza miaka 5 na baadae wanaendeelea vizuri tu? Kuelewa umuhimu wa elimu inakuwa ni pole pole kila anapojifunza.Umri ni tatizo kwa namna mbili mkuu:
1. Mtoto anakuwa hatilii maanani masomo kwa sababu bado akili zake ni changa hazijang'amua umuhimu wa elimu.
2. Mtotot akiingia sekondari akili zake bado zinakuwa changa haziwezi kumudu ugumu wa masomo na lugha.
Hivi mnatambua kwamba mitihani ya kubet hata SUA Chuo kikuu ipo mpaka ngazi ya masters?Mitihani ya kubet
Naishangaa mno serikali kwa kulazimisha kutunga mitihani ya kubahatisha (kubet) inayowawezesha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kupenya kwenda sekondari. Hii hupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wasiokuwa na uwezo kuingia sekondari, hivyo kushindwa kumudu masomo. Na hawa ndio huongeza idadi ya wanaofeli katika mitihani ya kuhitimu sekondari (CSE).
Tatizo kubwa sana hii, na chini ya kapeti "Mtihani ya kubet" wanataka kuleta mpka O-level
Ngono ni sababu nambari moja ya wanafunzi kufeli masomo sio shule za chini hata kule vyuoni. Tutalaumiana sana lakini mwisho tutaelewana tuHabari zenu wadau wa elimu? Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Awali ya yote napenda ku declare interest kuwa mimi ni mwanafunzi wa zamani na mshauri wa masuala ya elimu ninayefanya kazi na kampuni ya Shuledirect kwa hiyo ushauri ninaotoa hapa ni wa kitaalamu na kitafiti.
Kiwango cha elimu na ufaulu wa wanafunzi kimekuwa kikishuka kwa kasi ya kutisha. Hata ukilinganisha uwezo wa wahitimu wa zamani na wa kizazi cha sasa, utagundua tofauti kubwa sana. Ukimlinganisha kijana wa kitanzania aliyehitimu Kidato cha Nne hana tofauti na yule aliyeishia Darasa la Saba na wakati mwingine mhitimu wa Kidato cha Nne anaonekana bomu kuliko yule wa Darasa la Saba. Hili ni tatizo kubwa sana la kielimu ambalo limepaliliwa kwa muda mrefu na sasa limefikia pabaya kiasi hiki.
Tofauti na miaka ya 1980 kurudi nyuma hadi nchi hii ilipopata uhuru, kiwango cha elimu pamoja na ufaulu wa wanafunzi vimeporomoka kwa kasi kubwa. Baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu nimegundua sababu zifuatazo ndizo chanzo ya kuporomoka huku:
1. Mrundikano wa wanafunzi
Zamani darasa moja lilikuwa likichukua wanafunzi 45 tu. Sasa hivi sio ajabu kukuta darasa moja lina wanafunzi zaidi ya 200! Kwa idadi hii ya wanafunzi unategemea mwalimu ataweza kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja na kugundua uwezo wake wa kujifunza ili amsaidie kwa undani? Haiwezekani.
2. Mitihani ya kubet
Naishangaa mno serikali kwa kulazimisha kutunga mitihani ya kubahatisha (kubet) inayowawezesha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kupenya kwenda sekondari. Hii hupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wasiokuwa na uwezo kuingia sekondari, hivyo kushindwa kumudu masomo. Na hawa ndio huongeza idadi ya wanaofeli katika mitihani ya kuhitimu sekondari (CSE).
3. Umri mdogo wa kuanza shule
Kwa makusudi kabisa, serikali imekuwa ikipunguza umri wa watoto kuanza shule kadri miaka inavyoenda mbele. Wanafunzi wa zamani tulianza darasa la kwanza tukiwa na umri wa miaka 9–13. Sasa hivi serikali inashauri watoto kuaanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 5! Madhara ya kuanza shule katika umri mdogo ni makubwa kuliko tunavyodhani. Nitajaribu kuyaeleza kwa ufupi.
Kwanza, mtoto humaliza shule akiwa bado hajitambui na hajui umuhimu wa kutia bidii masomoni yeye binafsi bila kuhimizwa na wazazi. Na kwa kuwa hatii bidii kwenye masomo, ana uwezekano mkubwa wa kutofaulu mitihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE), hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofeli.
Pili, watoto wanaobahatika kwenda sekondari kupitia mitahi ya kubet, wakifika huko hukutana na masomo magumu na yanayofundishwa kwa lugha wasiyoielewa barabara. Hili nalo hupelekea kufeli wanafunzi wengi katika mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari (CSE). Mtiririko huu wa kufeli na kushuka kwa kiwango cha elimu huendelea hadi wanafunzi wanapohitimu kidato cha sita na kuingia vyuo vikuu.
4. Mtindo wa maisha
Mtindo wa maisha tunaoishi haujawaacha wanafunzi salama. Watoto wa siku hizi wanalelewa kwa mtindo wa kudekezwa ukilinganisha na mtindo wa maisha wa zamani ambao watoto waliishi kingangari bila kuwategemea wazazi wao kwa asilimia kubwa. Watoto wa sasa hivi bila kuwapa ahadi ya kuwanunulia zawadi kama vile simu, baiskeli na zawadi nyingine kedekede ikiwa watafaulu, hawatii bidii kwenye masomo ng’o. Na tatizo hili huanza tangu wakiwa wadogo kwa kudekezwa na kufanyiwa homeworks na wazazi.
5. Kukua kwa sayansi na teknolojia
Zamani hakukuwa na TV, movies, games, internet na mambo mengine kama hayo. Tulitarajia kwamba kukua kwa sayansi na teknolojia kungewasaidia wanafunzi kujifunza lakini hali imekuwa tofauti. Wanafunzi wengi wanaomiliki simu badala ya kuzitumia kujisomea huzitumia kutongozana, kuimba singeli, kuangalia video za utupu na kutukana walimu. Hivyo, hujikuta wanapoteza muda mwingi kwenye mtandao kufuatilia mambo ya kijinga na hatimaye kufeli mitihani.
6. Upatikanaji rahisi wa wa mahitaji ya shule
Kama ilivyo kazi ngumu kutafuta na kuchimba madini, vivyo hivyo thamni yake iko juu. Ingekuwa dhahabu inapatikana bwerere wala isingekuwa na thamani kubwa sana.
Sawa na madini, zamani haikuwa rahisi mwanafunzi kupata notisi kibwerere. Ilikulazimu kutembea mamia ya kilometa hadi kijiji cha mbali kuwahi notisi kwa mwanafunzi aliyehitimu masomo kabla wanafunzi wengine hawajakuwahi. Hata walimu walipata notisi kwa shida sana kwa kuwa vitabu vilikuwa vichache. Uchache huu ndio uliwafanya wanafunzi wa zamani kutumia notisi hizi kikamilifu na kuafaulu masomo kwa ufaulu mkubwa.
7. Serikali kuingiza siasa kwenye elimu
Kama ilivyo kwenye mitihani ya kubet serikali pia ina mkono wake kwenye kutunga mitihani rahisi na kuisahihisha kwa urahisi (easy exams and lenient marking of papers).
Siku moja niliongea na mwalimu wa sekondari anayeteuliwa kusahihisha mitihani kila mwaka akaniambia serikali huwapa maelekezo ya kusahihisha mitihani kwa urahisi na endapo mwalimu atakiuka anaweza kushushwa cheo kazini na hatateuliwa kwenda kusahihisha mitihani kamwe!
Yaani serikali inawaelekeza walimu watunge mitihani rahisi ya kubet na inaenda mbali zaidi kuwalazimisha walimu kuisahihisha kwa ulaini, na bado wanafunzi wanafeli. Kama serikali ingekuwa haiingilii kati, basi idadi ya wanafunzi wanaofeli ingekuwa ya kutisha zaidi ya hii tunayoshuhudia
Mjadala
Je, unadhani nini kifanyike ili kuepuka au kupunguza ukubwa wa tatizo hili? Karibu tujadiliane.
Nawasilisha
1. Mrundikano wa wanafunzi
Hizi pekee ndiyo hoja zenye mantiki, zilizobakia zote ni porojo tu.7. Serikali kuingiza siasa kwenye elimu
Bado unatengeneza tatizoSuala la umri na lugha ndio huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya mitihani yao. Tukitumia kiswahili kwa ngazi zote za elimu, tutakuwa na mafanikio makubwa