Mkuu usitafute unafuu wa kutetea hayo madubuwasha, Ngada imeharibu wengi sana kiakili, kiafya na kiuchumi. Hata wewe ulikuwa unaenda kupotea ulipoanza kusahau sahau ungeendelea ungekuwa ndo basi tena, hayo madudu hamna kitu ndio maana mateja wanakwambia zinawafanya wafikirie haraka ila unaweza kumuuliza swali akajibu baada ya muda wakati swali jepesi tu. Ngada inakitengenezea tu uongo kwenye akili uaminj kwamba inakuongezea confidence, kufikiria, n.k kumbe ni kinyume kabisa.
Hizo ngada zenyeww zikifika hapa bongo zimechanganywa na vitu kibao kama fethanyl ambayo ina nguvu mara mia kuliko heroin, supplier anachotaka ni kumgeuza mtumiaji mteja wa milele ili yeye afaidike huku wewe ukiangamia.
Hata cocaine za huko colombia ambazo ni original hazijachanganywa, watu wa huko wanashangaa sana watu wanaozitumia maana kuna documentary niliicheki kuna chemicala kibao sana zinachanganywa na hata sumu ya panya na cement vinawekwa humo wakiamini ya kwamba quality inaongezeka huku wao hawatumii.
Hayo madudu yanaenda kinyume kabisa na utaratibu wa starehe za asili kama pombe, Ngono, chakula, n.k
Kwa ushauri tu kwa vijana starehe zipo kibao hapa tz zisizo na madhara endapo ukitumia kwa kiasi, Kunywa pombe, sikiliza mziki, cheki mpira, kuwa na demu wa kukupumzisha mwili na ukienda mbali basi choma nyasi
KIBAYA NI KIBAYA TU, HAKINA HAJA YA KUTETEWA ILI KIONEKANE NA NAFUU, TUSHAPOTEZA VIJANA KIBAO KWA HAYA MADUDE