Naomba mnitajie movie kali za haya mambo ya spies....
The November Man 2014 - Pierce Brosnan yule jamaa wa movie za James Bond.
Kwenye hii movie yeye anaitwa Peter Devereaux, wakubwa wa CIA wanamuomba atoke kwenye kupokea pensheni ili aingine Russia kumtoa msichana aitwae Natalia ambae yumo Russia akiwa kama mwakilishi wa CIA lakini ni raia wa Russia.
Huyu msichana amepata jina la mtu ambae anataka kumharibia mgombea mtarajiwa wa uraisi wa nchi hiyo.
Ni movie nzuri kwa kuanzia na inafanana na movies za Bourne na zile za 007.
Movie nyingine kali ya spies inaitwa
AWOL-17 ya mwaka 2015, ambapo jamaa mwanajeshi anaitwa Conrad Miller (jina lake halisi Luka Gross) anatuhumiwa kuuza siri za kwa KGB wakati wa vita baridi.
Anapogundua kwamba kimenuka na kuna mwenzie anaitwa Myron (jina lake halisi Bokeem Woodbine) ndie amepewa kazi ya kumsaka na kummaliza.
Lakini Myron anataka kuanza na kumuua mpenzi wa Miller ambae ni mtoto bomba kwelikweli na hilo Miller anaona haiwezi kutokea na ndipo utamu wamovie unaponoga.
Halafu mwaka huu Bruce Willis amekuja na movie kabambe inaitwa The Extraction.
Kwenye movie hii Bruce Willis alicheza kama jasusi aliestaafu anaitwa Leonard Turner anatekwa na kundi la magaidi na wanatoa onyo kali kama madai yao hayatasikilizwa kabla ya kumwachia Turner.
CIA wanaamua kumpa kazi ya kumuokoa Turner kwa mwanamke aitwae Victoria ambae ni mmoja wa majasusi hatari wa kike ambao idara hiyo imewahi kuwa nao.
Victoria anapewa jukumu la kuwatafuta magaidi hao, kumuokoa Turner na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
Ni moja ya movie kiboko kwa mwaka huu.
Ntakushushia zingine nikipata muda.