Sababu zipi zilimfanya Mwl.Nyerere kuiingiza nchi katika ujamaa na chama kimoja?

Sababu zipi zilimfanya Mwl.Nyerere kuiingiza nchi katika ujamaa na chama kimoja?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.

Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
 
timing, wakati ule wote walikuwa communist I mean, waafrika na black people, communism ilijifanya kama ni mtetea wanyonge dhidi ya ukoloni kwa hivyo waliotawaliwa wote walikuwa attracted na communism, nchi karibia zote za Afrika, carribean mpaka India na North Afrika walijiunga communism hivyo siyo Nyerere tu, uislamu wote au niseme nchi za kiislamu kuanzia irak, iran, syria mpaka palestina walifwata communism ndiyo maana kulikuwa na wimbi la black amerika converting to islam, kwa kifupi communism iliwadanganya watu kwamba ni njia ya haki ya kujitawala.

communism looks very good in paper lkn wengi hawajui kwamba communism ni satanic na wanaofund communism ndio hao hao wanaofund capitalism …
 
Kwa kweli yanahitaji maelezo ya kina.

Tukisema kutawaliwa kuna mataifa kadha wa kadha yalitawaliwa na wala hayakuona kabisa umuhimu wa kufagilia siasa za kikomunisti.

Mbaya ni kwamba licha ukomunisti kuanguka na kuvurugika duniani na yeye kung'atuka kwa nchi kumshinda bado aliendelea kuamini kuwa mawazo yake yalikuwa sahihi.

Can you imagine mfadhili wake mkubwa mchina alianza mabadiliko toka miaka ya 70 ya kujiengua zaidi huko katika uchumi akaja yule mzee Deng akazidi kufanya mabadiliko zaidi na zaidi ya kuweka mambo sawa na hawa ni wakomunisti pure kabisa waliofuata mtiririko wote wa kuusimika ukomunisti katika nchi lakini walibadilika ili kuondoa taifa katika shida kubwa lakini yeye Nyerere bado aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa yupo sawa.

Hata alipo mteua mwinyi alimuona wa ajabu kwa kutotilia maanani misimamo yake.
 
Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.

Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Mtu mjinga huwezi mpa uhuru wa kujiamulia kabla hajastaarabika.

Angekosea tuu hapo ,Ardhi ya Nchi hii ingekuwa ya wachache sana
 
Mtu mjinga huwezi mpa uhuru wa kujiamulia kabla hajastaarabika.

Angekosea tuu hapo ,Ardhi ya Nchi hii ingekuwa ya wachache sana
Kama suala ni ardhi tu kwa nini mabadiliko yaligusa mpaka siasa na sheria za nchi ? Kwa nini kusingekuwa na mabadiliko ya sheria kuhusu umiliki wa ardhi ?

Mabadiliko ya kisheria kuhusu umiliki wa ardhi hata Singapore walifanya na wala sio nchi ya kikomunisti
 
Kama suala ni ardhi tu kwa nini mabadiliko yaligusa mpaka sheria za nchi ? Kwa nini kusingekuwa na mabadiliko ya sheria kuhusu umiliki wa ardhi ?

Mabadiliko ya kisheria kuhusu umiliki wa ardhi hata Singapore walifanya na wala sio nchi ya kikomunisti
Kwani Utawala ni aspect Moja tuu?
 
Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.

Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Hakuwa na hoja ya msingi. Alidai anataka kuondoa tabaka la walionacho na wasio nacho,, Nyerere kwa kweli sio mfano wa kuigwa na nchi mpaka leo haiendelei sababu ya kuiga fikra zake zote, hata mambo ya kutekana yalianza huko

Hivo basi, hakuwa na hoja ya msingi. Yeye alidhani kwa kuadopt ujamaa basi masikini hawatokuepo na aliamini ujamaa ndio msingi mzuri wa kuwabana matajiri wasiwanyonye masikini

Lakini kama ambavyo ukienda Hotelini ukaagiza kuku basi inakuja na chips. Nyerere naye alikuwa na agenda yake ya kujihakikishia absolute power kwa kupitia ujamaa. He never liked to be challenged not even by his comrades within CCM
 
Back
Top Bottom