Sabaya na wenzake washinda Rufaa dhidi ya Serikali kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Sabaya na wenzake washinda Rufaa dhidi ya Serikali kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Ukiona wanaopandishwa kuwa Justices of Appeal unaona kabisa kuwa kuna shida sana huko CoA! Ni hao judges kutoka High court ambako ni "mavi" maupu, "mavi" hayo yanapanda kwenda kwenye apex court! Soma hata kiingereza chao, shida tupu! Linganisha hukumu za bold judges kama Mwalusanya na za hawa UPE, utaona clear intellect difference, a very big one


Kwamba?? High court za Tanzania ni mavi matupu??

Hujaumaliza mwendo bado, angalia sana unapokanyaga. Sana.
 
Mahakama ya Rufaa Tanzania, imetupa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.

Leo Ijumaa Novemba 17, 2023 mahakama hiyo imetupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuona umekosekana ushahidi usioacha mashaka wa wajibu rufaa hao kutenda kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha au makundi.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abeesiza Kalegeya.
Kangaroo courts hizi.Hazina jipya.Hakika MAMA anaupiga mwingi hadi anapiga mtu GWALA 5.
 
Mako mwenezi sabaya kashinda rufaa. The team is back!! What we gona do mamen is back around !?
 
Kooo kooo kooo 🤣🤣🤣.


Mama aliacha afanye weeeee anayoweza, na chawa pia wakaachwa wafanye weee wanayoyaweza.

Sasa ipo hivi, Kila chawa ana Faili lake .


Vipi WATU wafikishwe mahakaman, au tukae mezan kwanza, Tim Msoga Vs Tim JPM ?.

Kwakua nanyie mafaili yenu yapo, Nasisi Vijana wetu wawe huru !!!!.


Na Bado... Huku Makonda, kule Sabaya !!.
 
Kwamba hadi wale wananchi waliokatwa masikio na kuingiliwa kinyume kule Hai walikuwa wanamsingizia?
Yule Ustaadh aliyevamiwa dukani kama jambazi, na wale wamiliki wa Hotels na wafanyabiashara je?
Sawa
Wewe mamlaka ya kuhukumu umetoa wapi?

Mahakama imekataa wewe unafosi.

Punguzeni Wivu
 
Dah kwel naamin weng chuki huzima mpaka uwezo wa kufikiri.hiv mnaona mahakama hawajui nyie ndio mnajua na mnataka mtu akutwe na hatia hata kama hana.shida sabaya au kitu ki gine? Kashinda mnaumia au kwa vile sio ndugu yako unataka ateseke
 
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.

Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.
Safi kabisa. Asante Mungu kwa hili. Mungu ni mwema. Hukumu imejieleza.
 
The expected! Mahakama za kishenzi. Kama walitoa hukumu kuwa Wakurugenzi kusimamia kura haina shida kwa vile wameapa kutenda haki, basi ujue hakuna mahakama ni takataka tu mbona wanajeshi wanapindua serikali ingawa wamaepa? chini ya viapo vyao?
Tulijua ni njia za kumsafisha.
Mahakama za Tanzania ni laana toka kuzimu.
Yaani hukumu huandikwa na kitengo wao ni kosoma tuu.
 
Back
Top Bottom