Sabaya ole Lengai dawa ya Mafisadi, karibu tuwatibu wagonjwa wenye ugonjwa wa ufisadi, wizi na wauza madawa ya kulevya

Mw
Huyo ni Kiongozi Mkuu wa Chama kama Zitto vile πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mwalimu alipata kusema Tanzania hatuangalii imani ya MTU katika kuchagua kiongozi !! Tupo tayari kumuapisha kiongozi hata kwa kutumia miti kama yeye atakuwa anaamini miti !!
 
Wengi wao ni maopportunistics na wala sio wazalendo !! Huwa wanavaa ngozi ya uzalendo lakini nyuma ya pazia wanafanya ufisadi wa kutisha !! Hao ndio wabongo !!
Nadhani wanaweza kufika 80 % au zaidi kidogo !!!
 
Aaaaarghhhh!!! 😀
 
Well said. And he is going to pay hayo yote ya kinyama aliyowafanyia watu.Days are coming.
 
Ina maana haya ndiyo maelekezo ya kuangalia namna ya kukabiliana na mfumuko wa bei...
 
NURU IMESHINDA GIZA.
Power Lensabaya Mwanamapinduzi wa zama hizi ndani ya Taifa letu.

Ukiwa na Umri wa miaka 36 tu tayari umekuwa moja ya wanasiasa mashuhuri na shupavu kabisa hapa nchini na katika ukanda wa Africa Mashariki.

Pamoja na madhaifu uliyonayo kama Mwanadamu yeyote lakini mimi na Wanaccm wenzangu tuliyowengi tusiegemea kundi la lolote la siasa ndani ya chama chetu, wanaccm ambao kwao chama ni muhimu kuliko mtu yeyote ndani ya chama, wanachama halisi wa CCM ambao wako CCM bila Mategemeo ya Uteuzi wa nafasi yoyote, Wanachama tunaopenda CCM kwa Imani siyo kwa Fursa, tunaamini kuwa Madhila unayopitia inatokana na msimamo wako wa kukipenda chama na kukipigania hata kwa kutoa Uhai wako.

Jana baada ya hukumu kutoka mahakama kuu ndiyo nikafahamu Upendo wa wanachama wa CCM, hasa vijana wengi kutoka kila pembe ya Tanzania wake kwa Waume waliyonipigia huku wakifurahi sana, Hakika tayari una bond kubwa sana kwa vijana wengi ndani ya CCM.

Nadhani miye nilikuwa mtu wa mwanzo kupata taarifa ya ushindi wa rufaa yako Kutoka kwa moja wa wasaidizi wa wakili wako.
Niendelee kuwatia moyo vijana ndani ya CCM siasa inataka watu wenye ngozi ngumu kama Lengai Ole Sabaya, watu wanaojitoa kupigania maslahi ya chama chao ikibidi hata kupoteza maisha.

Wakati wa kesi yako kuna baadhi ya vijana wenzanko wa CCM walitiwa Rumande tena kwa maelekezo ya baadhi ya viongozi vijana ndani ya CCM kisa tu waliamua kuchangishana pesa kukusaidia kijana mwenzao yote haya ndiyo siasa.
Mimi naamini kabisa Kesi hii ilitokana na vita ya kisiasa ndani ya CCM na nje ya CCM.

Nilishangazwa kuona Ubalozi wa America na European Union ikiwa mstari wa Mbele kushinikiza ili ufungwe nadhani kufungwa kwako walitegemea kumkomoa Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye kimsingi ameshamaliza maisha yake hapa Duniani.

Hali kama hii iliwahi kutokea wakati wa sakata la EPA katika serikali ya awamu ya Nne chini ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ambapo Benki ya Dunia iliingilia kati kuhakikisha akina Rajabu Maranda na Farijala Hussein wanafungwa otherwise wangeondoa mikopo waliyokwisha kuidhinisha kisa tu Rajabu Maranda alikuwa Mwekahazina wa CCM mkoa wa Kigoma.

Hii inanionyesha kuwa sisi wanaccm Adui mkubwa wa Chama chetu ni Taifa la America na European Union tusibweteke tuzidishe mapambano.

Chama pekee cha upinzani inayopambana kuing'oa CCM Madarakani ni Taifa la America na European Union na siyo hawa vikaragosi mnaowaona wakijiita Wapinzani.

Hawa wanaojiita wapinzani ni mawakala tu kama ilivyokuwa enzi ya Utumwa viongozi kama hawa walitengeneza Urafiki na mafashisti wa Dunia ili kuwasafirisha mababu zetu kwenda Utumwani huku wao wakipewa Vijizawadi kama inavyofanyika sasa.

Siku viongozi wa CCM watakapogeuka mawakala wa Mabeberu ndipo wanaccm tutanyuka kila moja kurejesha Taifa letu mikononi mwa Wanamapinduzi wavujajasho wa Taifa ili.

Wakati mwingine nikiona wanaccm wenzangu wakishupalia mambo ambayo yana angamiza wanaccm wenzao ambao wakati mwingine wanajitolea maisha yao kuokoa hata Taifa nabaki kujiuliza huu Unafiki wetu tuliyosomea nchi gani ili na mimi niende.

Ndugu zangu iwapo itampendeza Mungu ndugu yetu akawa Huru tusiache kupigania maslahi ya CCM kokote, tukumbuke hawa wanaccm wenzetu wasiyokuwa na madaraka ndiyo wamekuwa Mstari wa Mbele kumuombea na wengine waliacha shughuli zao kwenda kumtembelea kisongo na wengine waliingia Rumande.

Tena watanzania wema waliyowengi walikesha kukuombea usiangalie nyuma songa Mbele kwa Fahari kubwa nani ajuaye kilichopo Mbele yako.

Kumbuka Mpendwa wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli waliwahi kutaka kummaliza na Sumu akiwa Waziri wa Ujenzi mpaka alitaka kujiuzulu Uwaziri.

Hayati Magufuli akaja kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa mpaka Mungu aliporuhusu Alale usingizi wa Mauti, Mwingine Shaka Hamdu alitaka kujiuzulu Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana Taifa tulimtia moyo alipitia changamoto kubwa akiwa na Umri mdogo ndani ya chama kwasababu tu aliamua kupigania Mali ya Jumuiya iliyoporwa na Wajanja wachache ndani ya CCM wanaojiona hiki chama ni Mali ya Baba zao.
Mwingine ni Dr. Harrison Mwakyembe.

Wakati mwingine unapojitoa muhanga kupigania maslahi ya watu maskini na kutetea Rasimali za Taasisi, unakumbana na Madhila kama aliyopitia Hayati Magufuli waliyetaka kumuua kwa sumu akiwa Waziri wa Ujenzi na Comred Shaka Hamdu Shaka waliyetaka kumsulubu alipokuwa Uvccm Taifa na Dr. Harrison Mwakyembe.

Madhila kama haya yanayompata kijana wetu Lengai Ole Sabaya inawezekana inatokana na wabaya wake Kisiasa kutaka kuzima Nyota yake.

Tumuombee Lengai Ole Sabaya ili hukumu ya mwisho wa mwezi huu Mungu amuepushie mbali kama alivyofanya jana.

Baada ya kumaliza ya Sabaya tuangalie na zile familia ya vijana wa CCM waliyopoteza maisha yao wakati wa Uchaguzi 2020 Kule Tunduma, Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu mkoa wa Iringa aliyeuwawa na Chadema Tanzania Kule Njombe, waliyojeruhiwa na wafuasi wa Chadema Katavi, Rukwa na Tarime mkoani Mara.

Nuru imeshinda giza the Great Lengai Ole Sabaya
 
Mwanamapinduzi wa kuwaangamiza wapinzani wake wa kisiasa?

Unachekesha Sana wewe😁
 
ccm wote wezi
 
Aisee huyu comrade alimnyoosha Mboyer mpaka akalia kabisa na kutamani kufanya matendo ya kigaidi.
 
Naona mlikuwa na wakati mgumu kwenye karakana yenu ya ibilisi. Kiongozi amerudi sijui kama atakubali kuendelea kuwa C.E.O au fundisho alilopata linamtosha
 
Here it is, it speaks for itself.View attachment SABAYA JUDGEMENT - Armed Robbery - MD, Mendez.pdf.PDF
 
Kama ambavyo Jamhuri kutokuendelea na kesi haimuondolei ugaidi... Jinai haifi.
Hakuwa amehukumiwa!! But Sabay alihukumiwa.... Kaachiwa sababu ya technicalities sio kwamba hakutenda hayo makosa!!!

Mfano kesi ya uhujumu uchumi ipo clear kwamba kweli alipora fedha na CCTV footage zilionyeshwa mahakamani so akiachiwa na hii ingine sio kama Hana kosa ila ushahidi ulikuwa wa wazi.

Kwa Mbowe hakuna ushahidi wa kufadhili ugaidi popote ulioletwa mahakamani so usilinganishe haya matukio mawili.
 
Mahakama ilimkuta gaidi na kesi ya kujibu, Jamhuri ikaamua kutoendelea; and as long as jinai haifi, he shouldn't rest assured.

Sabaya ameachiwa huru kwa kuwa hakimu aliyemkuta na hatia mwanzo alijawa hisia zaidi ya haki; hivyo hakutenda kosa lolote.

Kuhusu Uhujumu Uchumi; tuiachie mahakama iamue kama kweli alipora au la, siyo kazi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…