Sadaka kumpa mzazi ni bora kuliko kuipeleka kwenye nyumba za ibada

Nimependa uwezo wako wa kufikiri. Sadaka unapeleka kanisani zinaishiwa kuibiwa na kuhongwa wake za watu au kuneemesha matapeli kama akina Gwajima. Heri hata ununue ulabu ujinywee kama wazazi wako walishakufa kuliko kuwapelekea hao mahabithi wenye roho mtakakitu wamuitaye roho mtakatifu wakati ni mchafu
 
PEngine tunatofautiana imani mkuu.
mimi siamini kama lengo la sadaka ni kumrudishia Mungu, Mungu yeye hanufaiki na sadaka zetu na wala hadhuriki na ubakhili wetu.
Basi, ni kweli mkuu hapo ndipo tunapotofautiana na tukubaliane kutoufautiana. Mimi na wengine wenye imani kama yangu wanaamini sadaka wanayotoa ni kwa ajili ya kufanya kazi ya kueneza neno la Mungu. Watu wengi wanapolijua na kulishika neno la Mungu basi furaha kubwa inakuwapo katika jeshi la Mungu

Luka 15:7-10
7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
 
Yaani hata mimi sikatai na wala sipigi huwezi mwadhibu mzazi kwa mabaya anayoyafanya ni wengi wanafanya, lakini watoto wasilaumiwe moja moja hapana kuna wazazi vichomi, unakuta baba anaoa kabinti [emoji3] nakupata watoto kisha nyie mlioachwa huku msomeshe hao watoto na nilazima kisa mzazi, mmoja anakwambia Mzee anataka watoto aliozaa kwa mchepuko mwanaye mkubwa awapeleke hao shule za private haaa haaa !
 
Duh huo mtihani
 
Mkuu ukimpa mzazi hiyo siyo sadaka ni wajibu wako, ila ukimpa mtu mwingine mwenye uhitaji hapo ndo umekuwa umetoa sadaka..ni hivyo nilimsikiza mwanauzoni mmoja akisema.
 
Ibada njema huanzia nyumbani. Mtu asipompenda wa ndani mwake kumpenda Mungu hakumo ndani mwake
 
Mkuu ukimpa mzazi hiyo siyo sadaka ni wajibu wako, ila ukimpa mtu mwingine mwenye uhitaji hapo ndo umekuwa umetoa sadaka..ni hivyo nilimsikiza mwanauzoni mmoja akisema.
Kwani mzazi hana uhitaji ?

Mwanazuoni gani kasema ?
 
Asante sana Boss. Kuna wajinga bora wapeleke hela zao huko zikanunuliwe ma- VX lakin wazazi wao waliowasimesha wanalala njaa
 
البَقَرَة

وَأَتِمُّواْ ٱلۡحَجَّ وَٱلۡعُمۡرَةَ لِلَّهِۚ فَإِنۡ أُحۡصِرۡتُمۡ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۖ وَلَا تَحۡلِقُواْ رُءُوسَكُمۡ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡهَدۡيُ مَحِلَّهُۥۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ بِهِۦٓ أَذٗى مِّن رَّأۡسِهِۦ فَفِدۡيَةٞ مِّن صِيَامٍ أَوۡ صَدَقَةٍ أَوۡ نُسُكٖۚ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلۡعُمۡرَةِ إِلَى ٱلۡحَجِّ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۚ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖ فِي ٱلۡحَجِّ وَسَبۡعَةٍ إِذَا رَجَعۡتُمۡۗ تِلۡكَ عَشَرَةٞ كَامِلَةٞۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمۡ يَكُنۡ أَهۡلُهُۥ حَاضِرِي ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
 
Unakusudia nini
 
Kuna watu “wameweka heshima” church kwenye kujenga majengo wakati Mama zao wanaishi kwenye vibanda vya mbwa huko vijijini.

Hii laana haiwezi kumuacha mtu salama!
Sadaka kwa wazazi ni jambo kubwa sana
 
Pamojja mkuu nimekusoma vyema
 
Ibada njema huanzia nyumbani. Mtu asipompenda wa ndani mwake kumpenda Mungu hakumo ndani mwake
Kuna kauli ya nabii muhammad inasema "mbora wenu ni yule aliyekuwa mbora kwa watu wa nyumbani kwake(mke,watoto,baba,mama aau familia kwa jumla"
 
Nyumba za ibada zimegeuka mapango ya wanyang'anyi, ni bora nipeleke fedha hiyo kwa wagonjwa hospitalini au niwasaidie wengine wenye shida kuliko kuwapelekea wahuni wanaolitumia jina la mwenyezi Mungu kuwaibia watu hata wale masikini wasioweza kupata mlo mmoja kwa siku, inaumiza sana
 
Wanaoipokea sadaka kwa kisingizio cha utumishi wa Mungu wanatakiwa kutubu na kuungana na wale wanaotoa sadaka hizo kwenda kuhubiri neno la Mungu kwa kujitolea na siyo kuwatoza watu pesa halafu wanazitumia fedha hizo kufanya starehe, anasa na kujenga majumba ya kifahari
 
Kabisa kabisa.

Sio fair home msosi mbovu alafu pesa unawapa wengine
Maneno ya busara kabisa. Na mimi naongeza ni bora uwape watu wenye uhitaji kama yatima, wajane, wagonjwa kuliko kuipeleka kwa watu kama Gwajima.
 
Asante sana. Eti unakuta mtu anapeleka kwa mtu kama mzee wa Upako au Gwajima. Ni bora nimpe ombaomba au yatima. Hata hospitalini kuna wagonjwa wenye uhitaji wengi sana.
 
Jifunze tofauti kati ya sadaka na msaada.
Jifunze tofauti kati ya sadaka na msaada.
Lakini pia jua kutofautisha vinavyomstahili Mungu na vilivyo kwa ajili ya Kaisari( binadamu wenzetu au mamlaka ya kiserikali).
 
Jifunze tofauti kati ya sadaka na msaada.

Jifunze tofauti kati ya sadaka na msaada.
Lakini pia jua kutofautisha vinavyomstahili Mungu na vilivyo kwa ajili ya Kaisari( binadamu wenzetu au mamlaka ya kiserikali).
Sawa nimejifunza ndo mana nikaandika hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…