Saed Kubenea amburuza Paul Makonda Mahakamani, kupanda kizimbani Desemba 3, 2021 kwa makosa ya jinai

'wale ambao wanajiona wana madaraka sana kuliko mimi hamnijui, mimi ni mtu mkubwa kuliko wao' wajuvi tunaomba mtujuze hayo mamlaka aliyokuwa nayo konda boy yanayozidi hadi ya waziri mkuu.........
 
No comment
Itakuwa unampenda weweee,kumbeeee...
Nivema atakuwa amepewa haki ya ama kulisafisha jina lake ama kuwafundisha vijana wanaokurupuka wapewapo uongozi kubwa mwisho wa ubaya aibu!
Wenye ushahidi wajitokeze sasa taifa lipone japo najua sirkali itampambania ashinde
 
Mkubwa Fella😅😅😅
 
Amekwishatuma watu kadhaa anaowaamini, kuomba huo upatanisho. Mzee wa watu kawaambia kuwa alisamehe tangu wakati huo huo ambapo Makonda alikuwa akimnanga. Hivyo haoni na wala hakuna haja ya kuombwa msamaha. Wote jibu wanalopewa ni moja. Lakini amekuwa anayafanya yote hayo ili ikiwezekana arudishwe serikalini, hata kwa nafasi ya uDC.

Sasa naona badala ya kuoewa cheo huku uraiani, huenda akapata cheo cha unyapara gerezani.
 
Hizi kesi mbona sijazielewaaa. Sasa wanampeleka mahakamani kwa kosa lipiii?? Au inaaamaa kila aliyefanya makaosa ya kiutendaji naye apelekwe mahakamaniii? Nani mkamilifu kiutendajii?? Tutakamata wangapiii
 
Mahakama itahitaji Picha tu..wakisema Paulo na Daudi waje..si picha zitalinganishwaa?
 
Clouds walishamkana huyo Mwanasheria wenu uchwara naona anatafuta kick kupitia jina la Makonda na msifikiri Kila mtu anafurahia kuona mtu mwingine anateseka kwa sababu TU ya chuki za kisiasa na kuna maisha mengine nje ya siasa
 
Hiyo ndiyo inayosababisha ugumu wa kupata KATIBA mpya watu wengi wanatamani waliopo madarakani washtakiwe wao wanatafuta Kinga ya kutoshtakiwa.

Binadamu wa kiafrika wanatabia za kipare wanaweza kuuza mbuzi kwa kesi ya kuku.

Wekeni bayana makosa ya Makonda @ Bashite ili tuyalinganishe na makosa yaliyowahi kufanywa na viongozi wengine waliowahikutokea.
 
Clouds walishamkana huyo Mwanasheria wenu uchwara naona anatafuta kick kupitia jina la Makonda na msifikiri Kila mtu anafurahia kuona mtu mwingine anateseka kwa sababu TU ya chuki za kisiasa na kuna maisha mengine nje ya siasa
Makonda ndio alikuwa anafurahia kuons wenzake wakiteseka.


Karma haiwezi kumuacha, na haijawahi kumuacha mtu salama. Vipi wewe ndio wale machawa wake?
 
Makonda ni jambazi kama majambazi wengine, subiri kortini ndio utajuwa kimya kingi kina mshindo.
 
Je vipi na maswahiba wake, Akina mnyeti, hapi, muro tuanze kuwaomba wajiandae na kuanza kupata uzoefu Kwa swahiba wao🤔?
 
Mbona Riziwani Kikwete ndio alikuwa mtu wake wa karibu?

Kitendo cha kumuorodhesha Riziwani kwenye orodha ya wauza unga huyu mjinga kamwe hawawezi kumsamehe, tena asubiri ile nongwa ya kiswahili haswa.
Unakumbuka ile picha anamfunga kamba za viatu R1, baadaye akapewa ukuu wa wilaya.Alafu akamtaja kwenye list ya bwimbi
 
huna akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…