Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Husimuonee p.mselewa ni kwamba sheria za kuingia au kutoka ndani ya nchi ziliwekwa kwa ajili ya usalama wa taifa kwa maana unaweza kuwa mtanzania lakini ukawa unahujumu taifa lako hivyo ndio maana kuna mipaka iliwekwa kisheria ili uweze kuruhusiwa na masharti yake, utashangaa kitu hapa pesa za kigeni hapa ndani zipo ukiitaji unaenda kubadilisha kila pesa hiyo unapotaka kuvuka mpaka lazima ubebe kwa kiwango Fulani na ihalalishwe na wanahusika,unatakiwa ujue kuna sheria zipo kama zimekufa lakini ikitokea umeharibu alafu ni famous inakuumiza,mfano:sheria ya umiliki wa laini tumeambiwa ukitaka kutumia zaidi ya moja omba kila wengi wanazo hadi kumi na hawajaomba siku ukiharibu hizo laini zitakuja kukufunga,zipo sheria nyingi zinaonekana kama mfu ila ukiaribu zinauma.
Sasa nyumba yako ina mlango wa kuingilia, wewe unarudi usiku saa sita unachupa ukuta, umeingia kihalali apo? Au hukufunzwa adabu kwenu?

Halafu kajifunze kitu:

Criminalization of Illegal Entry Around the World
Keshatiwa mbaroni tayari, hiyo ni hatua ya kwanza... hayo unayosema wewe yatajulikana mahakamani.

Swali la msingi, je ni lini kesi hiyo itasomwa na kumalizika?
Mahakama inahitaji ushahidi wa Kubenea kwenda Kenya na kurudi kwa njia ya panya na si vinginevyo.

Kesi ya Zombe Jaji aliwaambia upande wa mashtaka wakawatafute wauwaji wawalete mahakamani, Zombe hakuuwa mtu lakini alishtakiwa kwa kesi ya mauwaji.

Wengi humu bado hamuelewi kwa nini watu wengi hawafungwi mahakamani bado hamjajuwa mahakama hasa huwa inahitaji nini ili kumfunga mtu.
 
å Sometimes sisi wanadamu ni ngumu sana kuacha mazoea yetu hasa ya kuumiza na kubagaza watu wengine....

å Aidha ukiangalia namna mambo yalivyo kwa jicho la kibinadamu, kwa mazoea ya kibinadamu na kwa kusikia kwa sikio la kibinadamu, ni ngumu sana mtu kuamini kuwa mambo yanaweza kubadilika kwa kufumba na kufumbua tu macho...

å Tundu Lissu wiki tatu au nne zilizopita alilisema juu ya hali ya utawala huu chini ya CCM ya Magufuli, kwamba kupitia sanduku la kura kamwe hawawezi kushinda hapo Oktoba 28, 2020....!!

å Alionya kuwa, wao CCM na MAGUFULI wanalijua na kulitambua hili vilivyo, lakini wana advantage moja tu.....wanaongoza serikali na wanaweza kutumia faida hii kujipatia ushindi wa mezani kirahisi kabisa ktk uchaguzi ili kuendeleza mateso ya wananchi....

å Aliendelea kusema, njia rahisi na ya kipekee ni kufanya "systematic pull out" ya wagombea wa vyama vingine kwa njia za kisheria na uhuni mwingine wowote unaowezekana. Naona watu kama Saed Ahmed Kubenea hawakumwelewa Tundu Lissu na sasa yanawatokea...

√• Tazama na sikiliza tahadhari ya TL ktk video hii 👇 👇👇
 
Kubenea amehama Chadema na kuhamia ACT, na kwa uhasama pale Ubungo.

Chadema Ubungo imepasuka sababu ya ishu yake na Boni (mtu wa Mbowe).

ACT Ubungo ndo chama pekee kilichomuwekea Boni pingamizi pamoja na wagombea wote udiwani wa CHADEMA UBUNGO. Hili pingamizi la ACT ndo limemuengua Boni kugombea ubunge Ubungo. Kitu ambacho hakiwezi kufurahisha akina Mbowe.

Kwahiyo sidhani kama Kubenea anashirikiana na Lissu, ili hali akina Mbowe na wenzake wanammind.

Msamaha wake itabidi aamue na kukubali kutumika ipasavyo....
Safi sana.
 
Dah.. hiyo sheria anayosoma Ndugu Mganga ni kali sana jamani..
Hizo hela hazifiki 30M ila balaa lake zito sana...
Mungu akusimamie Kiongozi yataisha
Kosa alilofanya ni kuingia Kenya nakurudi bila kupita njia halali, hilo ni kosa kwa mtu maarufu,
Jambo hilo lilimsumbua sana Ronardinho wa Brazil huko sijui Uruguay au Paraguay mwaka jana kwa kuingia kiujanja ujanja.
 
Hapa ndipo ninapokuona wewe ni wakili kanjanja, inawezekana vipi umkamate raia wa Tanzania ndani ya Tanzania na halafu umshtaki kwa kuingia Tanzania isivyo rasmi? Are you mad?

Hivi huko ccm huwa mnavutishwa bangi gani ya kuwatowa akili?
kosa hapo siyo kuvuka mipaka ,ni kuwa na hizo $8000 za kigeni ,mpakani hutakiwi uvuke na zaidi ya $1000 kutokana na sheria za sasa
 
Ninadhani amekuwa decoyed kama Kagame alivyofanya kwa Paul Rusesabagina (Hotel Rwanda Oscar Award recipient) hivi karibuni.

Pole Camaradie Kubenea utakuwa ulikwenda kusaka pesa za kampeini, ila siku hizi hawa jamaa wameziba na kutuatilia udhibiti wa kila mwanya/njia inayoweza kutoa upenyo kwa upinzani kupata uwezo wa kuendesha kampeini zao, ingawa wao waliisha kuvuna pesa za kampeini kupitia kwa mkataba wa akina Thobias Andengenye na Lugola, pamoja na mkataba wa manunuzi ya mbolea kupitia kwa wizara ya kilimo (Hassunga anahusika).
Hii siyo fedha ya kampeni. Inaonekana pengine ana mkataba wa kampuni ya Kenya kwenye mambo ya habari na huwa wanamlipa. Hapa pengine alikwenda mara moja kuchukuwa mshiko wake.
 
Nina wasiwasi,amount ya pesa on him ni kidogo sana kuwarrant an arrest,,
Kuingia na kutoka njia ya panya,kunataka red handed caughting,,au ushahidi wa video footage
Kimsingi kesi nyepesi kushinda msala ni kupelekwa mahakamani anaweza akawekwa ndani mpaka 2024.
 
Mkuu kwa hili tatizo la Kubenea ni uchoyo na ubinafsi tu.

Ni lini ulisikia Drugs Tycoon amekamatwa airport anasafirisha unga?

Dunia nzima magendo yanasafirishwa na vijana wa kazi au mawakala.

Biashara ya kusafirisha pesa nk Wasomali na wahindi.

Mtu analipa pesa Canada, wewe unakwenda kuipokea kariakoo na pesa haisafirishwi.
Nakubaliana na wewe. Kariakoo kuna vijiwe vingi sana vya kutolea fedha zinazopatikana nje ya nchi kimagumashi. Kama wauza ng'anda wengi hutumia hii njia.
 
Mahakama inahitaji ushahidi wa Kubenea kwenda Kenya na kurudi kwa njia ya panya na si vinginevyo.

Kesi ya Zombe Jaji aliwaambia upande wa mashtaka wakawatafute wauwaji wawalete mahakamani, Zombe hakuuwa mtu lakini alishtakiwa kwa kesi ya mauwaji.

Wengi humu bado hamuelewi kwa nini watu wengi hawafungwi mahakamani bado hamjajuwa mahakama hasa huwa inahitaji nini ili kumfunga mtu.

Maelezo yako ni mazuri sana mkuu, ila yapo too general... hapa ni Kubenea na jinsi atavyopoteza muda wake kipindi hiki muhimu kwake.

Hadi hayo usemayo yadhibitishwe ili aachiwe ni leo!!
 
Hivi sheria inayosimamia na kudhibiti aint money Laundering mfano una mtu nje ya nchi uk nk akatuma pesa kwaajili ya uwekezaji ni taratibu gani unatakiwa kutumia
Tafuta mawakili tukusaidie
 
Raia wa Tanzania kushtakiwa kwa kuingia nchini kinyume cha sheria ? Kabisa mwanasheria uchwara , kesi ya kisiasa Kama kawaida , kwanini alikataa kuunga mkono juhudi ? Aunge mkono juhudi hukohuko rumande kesi itayeyuka mara moja .
 
Sasa nyumba yako ina mlango wa kuingilia, wewe unarudi usiku saa sita unachupa ukuta, umeingia kihalali apo? Au hukufunzwa adabu kwenu?

Halafu kajifunze kitu:

Criminalization of Illegal Entry Around the World
Naona wengi hamjaelewa Matola anasema nini? Walimkamata red handed wakati anavuka? Kinachafanya wahisi kuwa alikuwa Kenya si ni hiyo risiti tu na ticket ya basi? Kama ana rafiki yake Kenya mwenye jina kama hilo na ndiye alimletea mpaka pale Namanga je?
 
Kama Mkurugenzi wa Mashitaka anaandaa mashitaka yenye 'matobo'('loop-holes') hivi basi tuna safari ndefu..


Hao CCM hawajali , Masheikh na waislamu wengine wanaopigania haki wako ndani kwa zaidi ya miaka 7 , na wanafikiri wao wataishi maisha hapa duniani
 
kosa hapo siyo kuvuka mipaka ,ni kuwa na hizo $8000 za kigeni ,mpakani hutakiwi uvuke na zaidi ya $1000 kutokana na sheria za sasa
Kuna ushahidi wowote unaonyesha kavuka mpaka ?
 
Dah.. hiyo sheria anayosoma Ndugu Mganga ni kali sana jamani.

Hizo hela hazifiki 30M ila balaa lake zito sana.

Mungu akusimamie Kiongozi yataisha
Ujinga kama huu angefanya mtu asiejielewa sawa ila Kubenea daah... watu wote wa upinzani wanatakiwa kujua kwamba wanatafutwa kwa kila namna kosa lolote unapotezwa sasa dola elf 8 kwake kitu gani
 
Back
Top Bottom