Safari moja ilivyotaka kunianzishia safari nyingine ya majuto

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
Mwaka jana nilienda mkoa fulani kumsalimia ndugu yangu, vilevile nilitaka nikapumzike nitulize na akili kidogo.

Nilikutana na mwanaume kwenye huo mkoa akaonyesha nia ya kutaka kuanzisha mahusiano yatakayopelekea ndoa kwa maelezo yake ya awali, sikuwa na huo mzuka wa ndoa ila nilihisi ana nia nikasema wacha nitulie hapa huenda nimeandikiwa huyu.

Baada ya muda kidogo nikagundua mambo kadhaa alinificha kwanza umri alinidanganya, aliniambia ana mtoto mmoja baadae akaniambia kuwa anao wawili.

Sasa kuna mipango tulikuwa tumeipanga nikamwambia mimi nataka nirudi kwanza town then baada ya kukamilika hiyo mipango ndiyo tutafanya process za mchakato wa ndoa, 😂heee saa ngapi asinigomee na kuondoka kama kanioa vile, eti oooh! mahusiano yenyewe ndiyo hayana hata muda unataka uondoke mimi nataka ukae kae kwanza nifanye mipango yangu twende wote huko kwenu nikatoe barua na mahali tuanze kuishi wote.

Kwanza ana mawivu akipiga simu usipokee au atume msg dk5 zikipita atakwambia una mambo yako wewe, na atajinunisha na hiyo ni kesi tayari mkikutana utasemwa hadi basi. Kuna hapo kwa ndugu yangu kuna huyo mdada ameolewa na mimba yeye na mumewe wakawa wanatoka akamuomba twende wote maana ni ana mazoea na dada yangu mimi nikakubali tukatoka, tukaenda zetu kujivinjari huko tukarudi saa7 za usiku, na kumbe mchumba alimtumia meseji ya usiku mwema sikuijibu.

Asubuhi nikaja kumtafuta mtu kanuna ananiambia huyo dada jirani kanitafutia mwanaume na nilikuwa naye jana hiyo siku tuliyotoka na akakomalia msimamo wake huo kama haiwezekani tutoke watatu lazima kila mtu alikuwa na wake, akanishtakia hadi kwa dada yaani yule kaka ni mswahili, mlalamishi sijapata kuona, hiyo kesi haikuwahi kuishaga kabisa hadi leo haongei na hiyo dada jirani eti anadai alinitafutia mwanaume na wakati siyo kweli.

Mimi nilifosi niliondoka zangu huo mkoa nilivyofika mjini nikaambiwa nimeondoka bila kumuaga kuna mwanaume nimemfata, akaniambia na niache kazi nisubiri aje alipe mahari niende kule tuanze kuishi huku anitafutia mtaji😂 alihisi nina njaa sana na ndoa sijui.

Kwa kutoa ni mtoaji na mpambanaji sana tu ila hizo changamoto zake ndiyo maana nahisi hakuna mwanamke anayemuweza kuishi naye, hapa nimemwambia aendelee na maisha yake atafute mwanamke mwingine ananitumiaga mameseji kama yote eti ananipenda nimsamehe siwezi kufanya huo upuuzi kwanza nilikuwa sina amani naye kabisa maana ama wivu uliopitiliza, namshukuru Mungu nimemjua mapema kabla hatujafika mbali namuombea tu apate wa kuendana naye.
 
Kweli ulikutana na bumunda la mbeya ,pole aisee natumai bado hamjampata mtu anayeleeweka ,basi ikawe kheri kwako ukianza kumtafuta mtu mwingine
 
Mkuu njaa ya ndoa usikatae wala kubeza, ulikuwa nayo.

Ndiyo nyie hupenda kuelezea mambo kwa kinyume!

Utasikia: ... 'lione sura yake jitu lenyewe bayaa'!

Kumbe kimoyomoyo ushakufa na kuoza kabisa juu yake...'sizitaki mbichi hizi'.

Mbinu hizo niliwahi kuzitumia zamani, lakini wife alikuja kunigundua, nikabadili maujanja ya kuonesha kuumizwa na hisia ama tamaa za mapenzi, ilikuwaga nawaponda sana wapenzi wangu mbele yake.

Mtu ashakulala kwa makubaliano ya kufunga ndoa,utasemaje haukuwa na njaa ya ndoa?
 
Mkuu njaa ya ndoa usikatae wala kubeza, ulikuwa nayo.

Ndiyo nyie hupenda kuelezea mambo kwa kinyume!

Utasikia: ... 'lione sura yake jitu lenyewe bayaa'!

Kumbe kimoyomoyo ushakufa na kuoza kabisa...'sizitaki mbichi hizi'.

Mbinu hizo niliwahi kuzitumia zamani, lakini wife alikuja kunigundua, nikabadili maujanja ya kuonesha kuumizwa na hisia ama tamaa za mapenzi, ilikuwaga nawaponda sana wapenzi wangu mbele yake.

Mtu ashakulala kwa makubaliano ya kufunga ndoa,utasemaje haukuwa na njaa ya ndoa?
Inawezekana hakuwa haja ya ndoa ila alikua na tamaa ya pesa za jamaa ,kwa kuchojoa na kucheza kikubwa ( stripper)
 
Back
Top Bottom