Safari moja ilivyotaka kunianzishia safari nyingine ya majuto

Safari moja ilivyotaka kunianzishia safari nyingine ya majuto

Kwa hiyo umeamua uje unitangaze humu jamii forums? Kwani ungeniacha kimya kimya umeona utapata hasara sana? Jifunze basi kutunza siri,ivi imagine ningetoa siri zako mambo unayonifanyia si ungekuwa ushajinyonga kitambo tu? Jumatatu nakuja kazini kwako.
 
Kwa hiyo umeamua uje unitangaze humu jamii forums? Kwani ungeniacha kimya kimya umeona utapata hasara sana? Jifunze basi kutunza siri,ivi imagine ningetoa siri zako mambo unayonifanyia si ungekuwa ushajinyonga kitambo tu? Jumatatu nakuja kazini kwako.
uzuri ni kwamba huyo mtu hata kwetu hapajui
 
hivi mtu ana miaka 34 ana watoto wawili kwa wanawake tofauti huoni kama ana shida zaidi yangu
Unajuaje kua shida ni yeye na sio hao wanawake anaokutana nao?

Kua na watoto wawili kwa wanawake tofauti haimaanishi kua Mwanaume ana shida,

Hata hao wanawake aliowaacha nao pia watapata wanaume wengine na watazaa nao,kwahiyo na hao Wanawake nao pia wahukumiwe kua wana watoto wawili kwa Wanaume tofauti nao Wana shida?

Lengo lako la kuanzisha huu uzi ni lipi hasa?
 
Hiyo ishu yake mbona ndogo Sana kwanini hukumkalisha chini mkaongea mkasolve?

Afu nikwambie wivu ni kitu cha kawaida Sana kwa wanaume especially kama mwanaume anakupenda Sana.

Ckuiz ndoa zilivyo ngumu mwenzio anataka apeleke mahari kwa wazee akuoe na wewe unaanza kuleta kichwa shauri yako Baki hivyo hivyo na ujeuri wako
 
Mwaka jana nilienda mkoa fulani kumsalimia ndugu yangu, vilevile nilitaka nikapumzike nitulize na akili kidogo.

Nilikutana na mwanaume kwenye huo mkoa akaonyesha nia ya kutaka kuanzisha mahusiano yatakayopelekea ndoa kwa maelezo yake ya awali, sikuwa na huo mzuka wa ndoa ila nilihisi ana nia nikasema wacha nitulie hapa huenda nimeandikiwa huyu.

Baada ya muda kidogo nikagundua mambo kadhaa alinificha kwanza umri alinidanganya, aliniambia ana mtoto mmoja baadae akaniambia kuwa anao wawili.

Sasa kuna mipango tulikuwa tumeipanga nikamwambia mimi nataka nirudi kwanza town then baada ya kukamilika hiyo mipango ndiyo tutafanya process za mchakato wa ndoa, 😂heee saa ngapi asinigomee na kuondoka kama kanioa vile, eti oooh! mahusiano yenyewe ndiyo hayana hata muda unataka uondoke mimi nataka ukae kae kwanza nifanye mipango yangu twende wote huko kwenu nikatoe barua na mahali tuanze kuishi wote.

Kwanza ana mawivu akipiga simu usipokee au atume msg dk5 zikipita atakwambia una mambo yako wewe, na atajinunisha na hiyo ni kesi tayari mkikutana utasemwa hadi basi. Kuna hapo kwa ndugu yangu kuna huyo mdada ameolewa na mimba yeye na mumewe wakawa wanatoka akamuomba twende wote maana ni ana mazoea na dada yangu mimi nikakubali tukatoka, tukaenda zetu kujivinjari huko tukarudi saa7 za usiku, na kumbe mchumba alimtumia meseji ya usiku mwema sikuijibu.

Asubuhi nikaja kumtafuta mtu kanuna ananiambia huyo dada jirani kanitafutia mwanaume na nilikuwa naye jana hiyo siku tuliyotoka na akakomalia msimamo wake huo kama haiwezekani tutoke watatu lazima kila mtu alikuwa na wake, akanishtakia hadi kwa dada yaani yule kaka ni mswahili, mlalamishi sijapata kuona, hiyo kesi haikuwahi kuishaga kabisa hadi leo haongei na hiyo dada jirani eti anadai alinitafutia mwanaume na wakati siyo kweli.

Mimi nilifosi niliondoka zangu huo mkoa nilivyofika mjini nikaambiwa nimeondoka bila kumuaga kuna mwanaume nimemfata, akaniambia na niache kazi nisubiri aje alipe mahari niende kule tuanze kuishi huku anitafutia mtaji😂 alihisi nina njaa sana na ndoa sijui.

Kwa kutoa ni mtoaji na mpambanaji sana tu ila hizo changamoto zake ndiyo maana nahisi hakuna mwanamke anayemuweza kuishi naye, hapa nimemwambia aendelee na maisha yake atafute mwanamke mwingine ananitumiaga mameseji kama yote eti ananipenda nimsamehe siwezi kufanya huo upuuzi kwanza nilikuwa sina amani naye kabisa maana ama wivu uliopitiliza, namshukuru Mungu nimemjua mapema kabla hatujafika mbali namuombea tu apate wa kuendana naye.
Sawa
 
mm ninachojua , wivu ndo msingi wa mapenzi, hakuna mwanaume anae chekea upuuzi na ujinga wakurudi saa 7 hata kama ulikua na rafki ako.

TATHMINI; lakini kama umesema hujawahi mpenda inaonesha hata haya maneno asilimia kubwa ni ya uwongo tu to FEED YOUR EGO 🤔

OK wew ulikua unahitaji ushauri gani binti ??
 
Back
Top Bottom