Safari moja ilivyotaka kunianzishia safari nyingine ya majuto

Umemkataa huyo kisa ana wivu,kila binadamu ana mapungufu yake,hata wewe una mapungufu yako,inaonekana jamaa alikupenda sana,

Kama mwenye wivu umeshindwa kumvumilia,je mwenye tabia ipi ndio utaweza kumvumilia?

Ulifanya vizuri sana kubadili ile ID yako ya Wife matearial.
 
Ndio tatizo la kuwaonjesha wanaume wa mikoani mambo ya daslam mnawachanganya..!! 😹😹😹
Kafinyiwa kwa ndani msukuma wa watu kapagawa, kawa na wivu kama nyegere(honey badger).

Hata jani tu likimgusa shemeji jamaa analinyofolea mbali.

Ila huyo dada nae akumbuke hakuna aliekamilika, atakuja kustuka shkamoo zimekua nyingi na kutongozwa kumepungua.
 
I'd ya wife material utajuaje ni kakipande kidogo ka nyama kwenye mtego wa panya?
 
I'd ya wife material utajuaje ni kakipande kidogo kwenye mtego wa panya?View attachment 3543216
Kumbe ile ID ilikua ni mtego?

Hiki kisa kimenifanya nione jamaa ame epuka makubwa sana huko mbeleni,Mwanamke katoka na watu walio kwenye ndoa,Mume na Mke kisha akarudi saa 7 usiku! Hakuna Mwanaume wa kuivumilia hii sinema.
 
Sema jamaa kuna namna anaonekana katumia pesa zake kumshawishi huyo bi dada awe nae , kuna namna mwamba ni goigoi fulani hivi kwa maelezo ya huyu bibie
 
Sema jamaa kuna namna anaonekana katumia pesa zake kumshawishi huyo bi dada awe nae , kuna namna mwamba ni goigoi fulani hivi kwa maelezo ya huyu bibie
Ni kweli mwamba ni goi goi na huyu Dada alisha anza kumpanda kichwani,hata huo mtoko kisha akarudi saa 7 usiku,inaonekana huyu Dada alifosi kwenda bila ruhusa ya jamaa,

Sasa hivi jamaa ndio anatakiwa akaze asirudi nyuma,atafute Mwanamke mwingine atakaye muheshimu na kumsikiliza.
 
Kwa tabia zake hawezi kupata mwanamke atakayemvumilia kama mimi
 
Mh! hayo mambo ya kulala yanatoka wapi tena, enewei sijawahi kumpenda yule kaka na tabia zake zimefanya nisimpende kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…