Safari ya gari Cape Town, Afrika Kusini mpaka Dar es Salaam, Tanzania

Ataiuza kweli sio poa
 
Ahsante kwa maoni yako. Kuhusu TRA ni mahesabu ya kawaida hakuna tofauti ya uingiza gari kupitia bandari.
 
Mateso yote ya nini mtoa post panda ndege hizo gharama za gari,,border,service na risk, zingine za njiani achana nazo unless kama mko kifamilia zaidi ya 4 people
Asante kwa ushauri. Ila kila mmoja ana matamanio, mipango yake katika maisha. Hata utokapo nyumbani kwenda kazini asubuhi hujui litakalo kukuta barabarani (hiyo ni risk pia) ila unaenda kazini na kurudi.

Kama pesa inaruhusu, hivyo ndivyo kufurahia maisha na kuona mazingira tofauti.
 
Wakuu vp experience ya basi ya abiria kutoka Cape town kuja Tanzania, nauli imekaaje na uchukuwa siku ngap

na kama kuna details zinazohitajika zaid ya Passport, ningependa ufafanuzi kwa anayefaham
Hakuna basi kutoka Capetown hadi Dar.
Hapo itabidi uunge uunge.
Capetown hadi Johburg kisha Johburg hadi Lusaka kisha Lusaka hadi Tunduma/Nakonde.
 
Gari ninayo hapa natumia na sijalipia kodi na ikitoka hapa inaenda Malawi ndio ntalipia kodi mbona unalazimisha vitu visivyokuwepo ni kama navyopita Botswana au Zambia bila kulipia Kodi unaweza kukaa Zambia muda unaotaka na ukaamua kuondoka ili mradi ulipie kibali cha kutumia gari kwa muda pale ila kama gari destination yake ni hapa na nimeamua kulipa nalipa tuu maana kodi yake haijachangamka kama gari za kutoka Japan..
 
Sawa mkuu gari unayo South Africa au Tanzania?
 
Ila msinunue gari mtandaoni SA watu wametapeliwa sana matrekta na gari mnaambiwa sijui bank repo pana utapeli sana hapo siku ntaanzisha uzi wake njia salama ya kununua na kusafirisha gari kutoka ZA...
Mkuu siku ukishusha huu uzi naomba unitag, halafu vipi na kuhusu spare kwa kununua online pia si salama kwa sasa pia?.
 
Mkuu siku ukishusha huu uzi naomba unitag, halafu vipi na kuhusu spare kwa kununua online pia si salama kwa sasa pia?.
SA imeingiliwa ila naweza kukupa address mara ya kwanza ukifika hapo Nugget parts au Bumper to Bumper trip zinazofatia unachukua wanakupa simu zao unawasiliana nao kwa whatsAap tu ukishafanya manunuzi kwa mara moja ni rahisi kufanya nao manunuzi mtandaoni au unaenda trip moja ni kuchukua mawasiliano na truck za kusafirisha mizigo yako...
 
Sawa mkuu mie kwa sasa sina mpango wa kwenda nilikuwa nikitembelea platforms tofauti za huko hivyo nikaona huu usumbufu wa wafanyabiashara wetu kutupiga bei ya ajabu ndio nikaona siku moja nijaribu na huko.

Ila nikiwa sawa nitafata tuu nitaanza na Msumbiji halafu katika na huko.
 
Kwamba una temporary permit ya zaidi mwezi mmoja?
Wewe jamaa unauliza ufundishwe au nina miaka zaidi ya 20 nafanya kazi za magari na vitu vingine SA matakataka yote na sheria nyingi zinabadilika tupo kwenye gemu...humu nipo kuwaeleza wengine wasione ugumu wewe unaleta mambo yenu ya Kitanzania kuwa haiwezekani unafaidika nini wakati gari za Gauteng zipo nyingi Daslm na mikoa mingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…