Madam President ni binadamu mwenye UTU sana na jasiri kweli kweli, we fikiria pamoja na ukali wa kupindukia wa Dk. Magufuri, hakuna kiongozi yeyote Serikalini pamoja na wabunge wa chama tawala walio thubutu kwenda kumjulia hali Tindu Lissu alipokuwa amelazwa Hospitalini Nairobi kutokana na majeraha ya risasi - Mtu pekee aliye onyesha uwanadamu na ujasiri wa kutukuka alikuwa si mwingine bali mama Samia Suluhu Hassan!! Hata anaposema kwamba ana nia ya kujenga umoja wa kitaifa Dunia inamuelewa kwamba si msanii/mbabaishaji - atatekeleza ahadi zake kweli - amekwisha wambia Doubting Thomases kwamba wajitayalishe kisaikokojia kukubali mabadiriko hayo yenye lengo la kujenga umoja wa kitaifa - kuna baadhi ya Watanzania wenzetu hilo hawalipendi kabisa kabisa - wanatamani ikiwezekana Tanzania iwe a one party state, bahati nzuri madam President ana exposure kubwa na vast experience ya kutambuwa Dunia ya hivi sasa inaendaje, binafsi nina uhakika atatuvusha salama.