Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Mboni kawaida tu uzuri wa hio Safari usafiri usiku ndio utaona raha yake, nimetoka Dar saa 2 Asubuhi nimefika Shinyanga saa 12:30 Asubuhi kesho yake halafu safi kabisa Mwadela Mama
 
Mwanaume kabisaa analalamika kusafir kwa bas eti mwanza dar very sad na watu wanampa pole. Na huna hela. Hawa watoto siku hiz sijui ni vip yan....anyways ndio generational evolution i think maana kadir siku ziendavyo kizaz dhaifu sana kinazid ongezeka
Nime mshangaa Sana, naonaga kawaida mno.
halafu one way trip SI ni usd 192 tu!
 
Yule mwamba angekuwepo sasa hivi SGR ingekuwa Mwanza. Masaa 7-8 uko Mwanza.
Mnampa sifa asizostahili kabisa.
Aliyemzaa mtoto na kufariki baada ya miaka 5 na aliyemtoa hapo kwa kumlea kimaadili, kumvisha,kumsomesha,kumuoza,nk nani apewe sifa zaidi?
Magu hata Chalinze angekuwa bado. Srma alikuwa mtu wa kupenda misifa. Sikopiii nje huku anakopa kimya kimyaa
 
Pole sana mkuu, mimi kutoka dar tu mpk moro au dodoma nishaachaga kupanda Bus ni mwendo wa private kwenda mbele bora niongeze nauli asee. Comfortability ni kitu cha msingi sana sikuizi.
 
Bado haiondoi umbali.
Mwanza-Dar siku hizi pamekuwa parefu tofauti hata zamani. Tulikuwa tunafika siku hiyohiyo kwenye saa 1 jioni au saa2 na Zuberi.
Leo hii masaa yameongezeka, mnasafiri njiani hadi unahisi kizunguzungu.
Zimeongezeka kilometa ngapi??
 
Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Ungepanda luxury bus, kuchoka kupo ila afadhali unaweza kujinyoosha.
 
Back
Top Bottom