Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Pole mkuu
umasikini ni mbaya sana
mkuu utakuwa ulipanda lori. basi likitoka mwanza saa 1 angalau saa tatu na nusu linatakiwa liwe shinyanga
mabasi angalau mazuri ni katarama au Allys na Sama
hayo mengine ni shida
 
Polee sana soon
Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Serikali tuta longe safar ya tren utafurah sana SGR oyeeee
 
Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Kuwa mpole, huyo uliyekaa naye hapo ndiyo mduguyo kwa sasa.

Umasikini hautaki hasira!! Kaa kwa kutulia kumbuka ukifika Dodoma tununulie zabibu.
 
Bado haiondoi umbali.
Mwanza-Dar siku hizi pamekuwa parefu tofauti hata zamani. Tulikuwa tunafika siku hiyohiyo kwenye saa 1 jioni au saa2 na Zuberi.
Leo hii masaa yameongezeka, mnasafiri njiani hadi unahisi kizunguzungu.
Kwamba zamani kilometa zilikuwa chache na leo zimeongezeka?
Kwanza zamani kwenda Mwanza tulikuwa tunapitia Nairobi !
Mtu unasafiri hadi unajishangaa. Siku hizi naona ni raha sana tuu.
 
Uzuri au ubaya ni kuwa tafsiri ya umaskini inabadilika kwa jinsi maendeleo yanavyokuja. Kuna wakati waliokuwa wanasafiri na basi walionekana matajiri, leo hii hao ndiyo wanaonekana maskini wa kutupwa.

Ila kiukweli gharama za ndege haziendani kabisa na uhalisia wa maisha ya Watanzania wengi. Sijui tumekwama wapi kuweka bei rafiki au ni lobbying ya wenye mabasi? Mbona kwenye huduma zingine tumeweza kuweka uwiano mzuri ili kila mtu aweze kutumia huduma?
 
Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Panda SGR hadi Dodoma na Dodoma hadi Mwanza chukua basi
 
Mkuu mbona nakuonea wivu , naona unakula raha.

Ungekuwa na Safar ya moja Kwa moja Mwanza- Mbeya nadhan ungemwaga chozi.

Kuna hii kutoka mwanza Hadi mbeya, ukifika Dodoma safari inaanza upya kuitafta mbeya.
Mmenikumbusha kuna siku nilikuwa Arusha nikakutana na watu wanajiandaa kurudi Mbeya. Nikapiga hesabu ya ile trip nikawaonea huruma saana.

Ila kama hauna haraka usafiri wa barabarani ni mzuri mno ukifuatiwa na wa treni.
 
Back
Top Bottom