Safari ya wanawake sio fupi kwa kiasi hicho

Ni vizuri na naheshimu msimamo wako japo siwezi kuufata hata robo.
Poa, lakini watoto wa aina hii ninayowlea mm ni vigumu sana kurubuniwa na wanaume, ni rahisi sana kwake kujifunza michezo kama Carate, football, boxing, riadha, nk. Confidence Yao Iko juu sana eye contact unapoongea nao Iko juu sana, hatazami chini Wala kung'ata vidole.
 
Hivi ni kwanini matumizi ya ziada ya mtoto wa kike mnasema ni pedi pekee??
Vipi nguo za ndani mkuu, hao wote ni sawa kwenye angle hiyo?? Mtoto wa kike atahitaji sidiria na chupi nyingi kuliko huyo kaka yake.
Hizo mambo ulizosema sijui kuchafua nguo sana, kula sana aisee mkuu mbona hayaingii akilini kabisa kwamba mroto wa kiume akienda mgahawani atakula sahani zaidi ya moja na wa kike moja tu itamtosha sio??

Tusiwe wabishi bna labda uongelee wale watoro ambao hawajavunja ungo lakini hawa ambao hadi matiti yamewaota, vishawishi kila kona aisee em tuwahurumia sio kufananisha matumizi yao sawa na wa kiume.

Hiyo 200,000 kwa wa kiume ni kubwa, kuhonga sio hitaji la lazima lakini pedi ni lazima. Unafananishaje hitaji la lazima na la hiari kaka??

Umeanza kwa kusema hitaji la ziada tusiongelee pedi pekee, lakini bado ukahitimisha kwa kutoa mfano wa hiyo hiyo pedi kusisitiza utofauti wa KE na ME.!

Kuhusu nguo za ndani ukisema mmoja anahitaji nyingi kuliko mwingine ndo ubaguzi wenyewe, hata hivyo boksa 1 ya kiume ni chupi 3 hadi 5 za kike kwa mujibu wa bei.

Hivyo basi, watoto wote wakielimishwa vizuri wanao uwezo wa kutumia bajeti sawa kwa mahitaji tofauti.
 
Kakaaa, tofauti kubwa sana iliyoko kati ya mwanaume na mwanamke iko kwenye viungo vyao vya uzazi tu ( uke, uume, korodani, ovale, uterus, nk) basi na wote wanazaliwa wakiwa uchi, hizi nguo, bangili, heleni, magauni, suluali na mishono ya nguo waliwapa sisi (social constructions). Wazazi ndio wanaowanunulia watoto wa kiume matoi ya bastola na magari na watoto wa kike midoli ya mwana sesele, vitu vya kujipikilisha na vitambaa vya kuvalisha watoto. Mimi watoto wangu wote niliwanunulia midoli inayofanana (bastola, magari, mwanasesele, nk) wachezee wote. Watoto wangu wa kike ndo walikuwa wa kwanza kuendesha magari yangu, na wote walikuwa na uwezo wa kukamua ng'ombe na kulisha na kufunga mbwa bandani. wote walijisikia wako sawa ila wote walijua kwanini wanatofautiana kwenye namna kukojoa; kuchuchumaa na kukojoa wima.

Kwenye mavazi natofautiana na wewe pamoja na hicho ulichokiita social construction, kama unaona sawa kwa KE kuvaa mavazi ya ME…. usitake niwaze kuwa unaona sawa pia kwa ME kuvaa mavazi ya KE kama hoja yako ni USAWA.

Nimechagua kutofautiana nawe kimtazamo tu lakini siwajibiki kubadilisha malezi yako, kwa maana hata mtaani tunaona ME wenye mavazi ya kike ambao bila shaka ni matokeo ya malezi ya namna yako.

Torati 22:5
Mtu mume asivae mavazi yampasayo mtu mke wala mtu mke asivae mavazi yampasayo mtu mume.
 
Wanaume kuendelea kuwa-favor wanawake ili hali tunaonekana si kitu ni shobo... Na mwisho wa shobo ni aibu na Kifo sasa endeleeni kuwahonga.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye mavazi natofautiana na wewe pamoja na hicho ulichokiita social construction, kama unaona sawa kwa KE kuvaa mavazi ya ME…. usitake niwaze kuwa unaona sawa pia kwa ME kuvaa mavazi ya KE kama hoja yako ni USAWA.

Nimechagua kutofautiana nawe kimtazamo tu lakini siwajibiki kubadilisha malezi yako, kwa maana hata mtaani tunaona ME wenye mavazi ya kike ambao bila shaka ni matokeo ya malezi ya namna yako.

Torati 22:5
Mtu mume asivae mavazi yampasayo mtu mke wala mtu mke asivae mavazi yampasayo mtu mume.
Hapo me naona kuwa wanaume tupo special sana na hii ni kwa kuwa ata uumbwaji wetu ulitofautiana na ke' so, namaanisha kwa Mimi mwanamke namuona ni mtu asiejua wapi asimame so hata kutenda dhambi kwake ni rahisi hivyo basi kama ke' anapokosea hatupaswi nasi kukosea Bali sisi tusimame katika njia iliyo sahihi..... Mwanamke akivaa Nguo ya kiume me hutikisa tu kichwa na kuondoka zangu hiyo haitafanya Mimi nikavae za kike.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Umeanza kwa kusema hitaji la ziada tusiongelee pedi pekee, lakini bado ukahitimisha kwa kutoa mfano wa hiyo hiyo pedi kusisitiza utofauti wa KE na ME.!

Kuhusu nguo za ndani ukisema mmoja anahitaji nyingi kuliko mwingine ndo ubaguzi wenyewe, hata hivyo boksa 1 ya kiume ni chupi 3 hadi 5 za kike kwa mujibu wa bei.

Hivyo basi, watoto wote wakielimishwa vizuri wanao uwezo wa kutumia bajeti sawa kwa mahitaji tofauti.
Sio chupi tu kuna sidiria pia ndgu.
Na hata hivo watoto wa kike wanajitahidi mno kwenye matumizi zaidi ya wakiume.

Pamoja na yote hayo bado wa kike wanahitaji pesa zaidi ya wa kiume hicho ndicho ninachokiamini na kukifanya.
 
Poa, lakini watoto wa aina hii ninayowlea mm ni vigumu sana kurubuniwa na wanaume, ni rahisi sana kwake kujifunza michezo kama Carate, football, boxing, riadha, nk. Confidence Yao Iko juu sana eye contact unapoongea nao Iko juu sana, hatazami chini Wala kung'ata vidole.
Wewe mkuu ni jasusi?? Unajua kuna ule irojorojo mtoto wa kike anao, kwahiyo hao wako ni nga nga nga.
 
Umeanza kwa kusema hitaji la ziada tusiongelee pedi pekee, lakini bado ukahitimisha kwa kutoa mfano wa hiyo hiyo pedi kusisitiza utofauti wa KE na ME.!

Kuhusu nguo za ndani ukisema mmoja anahitaji nyingi kuliko mwingine ndo ubaguzi wenyewe, hata hivyo boksa 1 ya kiume ni chupi 3 hadi 5 za kike kwa mujibu wa bei.

Hivyo basi, watoto wote wakielimishwa vizuri wanao uwezo wa kutumia bajeti sawa kwa mahitaji tofauti.
Exactly, wewe ndo umeilewa mada vizuri. Wasichana sio viunbe vinavyohotaji huruma za wanaume Wala makongamano mlimani city, huruma pekee wanayohitaji ni wakati wakiwa na mimba, kujifungua na kunyonyesha watoto. Hiki Kinachofanyika ni kuzidi kuwanyong'onyeza wanawake. Ukomnozi wao lazima uanzie nyumbani kwa wazazi wao wakati wa kuwalea, Kisha jamii Kisha serikali.

Ni vema kuanzia Sasa waziri apige marufuku uvaaji wa sketi na magauni shuleni kwa wasichana kama vile polisi wa kike walivyoruhusiwa kuvaa suruali ambazo zinawaongezea uimara kwenye kazi zao badala ya zile sketi ambazo zilikuwa zikifunuliwa na upepo.
 
Chupi na sidiria haviwezi kuwa sehemu ya pocket money yake. Hivi huwa ananuniliwa nyumbani TU na mama yake kabla ya kwenda shuleni. hata watoto wa kiume wanahitaji singileti, socks nyingi pia maana wanachafuka na kutoka jasho jingi sana. Kaka watoto wa kiume ni tabu sana kuwalea kuliko wasichana. The bottom line hapa ni kuwa watoto wote wanahitaji kutunzwa na Wana gharama zinazokaribiana.
Hapo nimekupata vilivyo mkuu. Kama ni kwa hilo basi nakubaliana na wewe kua ni kweli wanapaswa kupewa pocket money sawa. Maana mi concern yangu ni hivyo vitu vidogo vidogo ambapo mwanamke anavyo vingi kuliko mwanaume, so kama vinanunuliwa mapema hata wakipewa 20/20 kila mtu hapo basi haki sawa. 🤝
 
Kwenye mavazi natofautiana na wewe pamoja na hicho ulichokiita social construction, kama unaona sawa kwa KE kuvaa mavazi ya ME…. usitake niwaze kuwa unaona sawa pia kwa ME kuvaa mavazi ya KE kama hoja yako ni USAWA.

Nimechagua kutofautiana nawe kimtazamo tu lakini siwajibiki kubadilisha malezi yako, kwa maana hata mtaani tunaona ME wenye mavazi ya kike ambao bila shaka ni matokeo ya malezi ya namna yako.

Torati 22:5
Mtu mume asivae mavazi yampasayo mtu mke wala mtu mke asivae mavazi yampasayo mtu mume.
Mchungaji wa kike na mchungaji wa kiume wanavamaa mavazi tofauti? Au wote wanavaa kanzu ndefu?

Hakuna mavazi ya kike Wala mavazi ya kiume yanayotoka kwa Mungu, watoto wote wanazaliwa wakiwa uchi kabisa, jamii ndiyo iliyowaamilia nguo gani wavae. Bahati mbaya jamii imewachagulia wanawake nguo dhaifu sana kama kanga, kitenge, shumizi, sketi, gauni na vichupi laini zinavyoweza kumuweka uchi wakati wowote kukiwa na kurupushani hata kidogo. Siku moja askari wa kike aliwekwa uchi na mhalifu wakigombea kukabidhi lisensi ya udereva, sketi ilifunuka wakati wa kurupushani. Watoto wa kike wanawekewa vioo chini na watoto wa kiume ili kuona viungo au nguo za ndani za msichana aliyevaa gauni. Tuwape watoto wa kike nguo zinazowatia ujasiri sio zile zinazowadhoofisha
 
Wewe mkuu ni jasusi?? Unajua kuna ule irojorojo mtoto wa kike anao, kwahiyo hao wako ni nga nga nga.
Wanangu wa kike wanafahamu ni wapi mwanaume ukmminya au kimpiga atakuachia kwa urahisi. Wafanye watoto wa kike wasimiohope baba Yao, kaka zake na watoto wa kiume, mwambie ukweli kuwa mwanamke na mwanaume maana yake nini, uzuri na ubaya uko wapi na tofauti ni nini
 
Sio chupi tu kuna sidiria pia ndgu.
Na hata hivo watoto wa kike wanajitahidi mno kwenye matumizi zaidi ya wakiume.

Pamoja na yote hayo bado wa kike wanahitaji pesa zaidi ya wa kiume hicho ndicho ninachokiamini na kukifanya.

Unalea kwa ubaguzi na kuamini kuwa wa kiume ataweza kujitafutia, au kwamba unamwepusha wa kike na vishawishi.

Unasahau kwamba wa kike hupokea na wa kiume hutoa, kijana wa kiume atatoa fungu kadhaa kumpa zawadi binti fulani. Binti atapokea na kusevu alizopewa home.

Kama wazazi hatuwezi kufundisha hilo lakini haiondoi ukweli kwamba ni mambo yanayoendelea, wote tunapitia hatua hizo.

Binafsi naamini katika usawa, hivyo nitawapa bajeti sawa na kuwafundisha namna ya kutumia kiasi hicho kulingana na vipaumbele vyao.
 
haya mambo ya super woman na upuuzi yamechachamaa miaka hiii - nadhani ni sababu ya kule juu
 
Sio kule juu, hata yeye aliyakuta, anayatimiliza na kuyakoleza tu
 
Unalea kwa ubaguzi na kuamini kuwa wa kiume ataweza kujitafutia, au kwamba unamwepusha wa kike na vishawishi.

Unasahau kwamba wa kike hupokea na wa kiume hutoa, kijana wa kiume atatoa fungu kadhaa kumpa zawadi binti fulani. Binti atapokea na kusevu alizopewa home.

Kama wazazi hatuwezi kufundisha hilo lakini haiondoi ukweli kwamba ni mambo yanayoendelea, wote tunapitia hatua hizo.

Binafsi naamini katika usawa, hivyo nitawapa bajeti sawa na kuwafundisha namna ya kutumia kiasi hicho kulingana na vipaumbele vyao.
Wala sio ubaguzi mkuu, ni gender equity.

Nampa kinachostahili na sio sawa na mwenzie.
 
Wanangu wa kike wanafahamu ni wapi mwanaume ukmminya au kimpiga atakuachia kwa urahisi. Wafanye watoto wa kike wasimiohope baba Yao, kaka zake na watoto wa kiume, mwambie ukweli kuwa mwanamke na mwanaume maana yake nini, uzuri na ubaya uko wapi na tofauti ni nini
Aisee unawafunza mpaka mapigano we noma.

Binafsi level hizo sijafika na wala aifikirii kuzifanya. Nadhani kujitambua tu inatosha.
Kuna mambo atatakiwa kuyafanya yeye kwa kupenda yeye mwenyewe.
 
Kuna mambo ambayo wanawake wamepewa na wanaume bila wao wenyewe kuyapenda. Mfano, aliyeamua wanawake wavae magauni na sketi na kilinda na wanaume wavae kaptula na suluali waliangalia urahisi wa wanawake na wanaume wakati wa kujisaidia haja ndogo na kubwa basi wakadharau uwezo wa wanawake kujihifadhi wa mavazi hayo. Ndiyo maana wanawake baada ya kuliona hilo siku hizi wakaja na chupi, skin tight na suruali. Na hatujaona mwanamke aliye jikojolea au kujinyea eti kwasababu amevaa chupi, skin tight au suruali. Malengo yao ni mwanamke awahi kuvua na kuchuchumaa kwa urahisi wakati wa kujisaidia, shame upon them.
 
Sio chupi tu kuna sidiria pia ndgu.
Na hata hivo watoto wa kike wanajitahidi mno kwenye matumizi zaidi ya wakiume.

Pamoja na yote hayo bado wa kike wanahitaji pesa zaidi ya wa kiume hicho ndicho ninachokiamini na kukifanya.
Kumbuka kuwa mume wa kwanza wa mwanamke ni baba yake mzazi, watoto wa kike kwa asili wanapenda baba zao zaidi kuliko mama zao na wale wa kiume wake zao wa kwanza ni mama zao. Baba atakavyomlea na kumhandle binti yake ndiyo binti yake hivyo atakavyotaka afanyiwe na wanaume wengine wote hata akiwa mkubwa. Na mtoto wa kiume atakavyofanyiwa na mama yake ndivyo atapenda hata mkewe na wanawake wengine. Mfano, kama mtoto wa kike akilia baba yake anamtuliza na kumliwaza kwa kumpa kitu au kumletea zawadi basi mtoto huyo hata ukubwani atapenda apewe zawadi akikasirishwa au akiwa na huzuni na kama baba anamliwaza binti yake mdogo kwa kumkumbatia na kumshumu shavuni mtoto huyo hata ukubwani atapenda afanyiwe hivyo na mwanaume huko uumbwani kwake. MTOTO WA KIUME hivyohivyo kwa mama yake pia.

Ndiyo maana ya umleavyo ndivyo akuavyo
 
🤔🤔 its true theoretically.
 
Back
Top Bottom