Kakaaa, tofauti kubwa sana iliyoko kati ya mwanaume na mwanamke iko kwenye viungo vyao vya uzazi tu ( uke, uume, korodani, ovale, uterus, nk) basi na wote wanazaliwa wakiwa uchi, hizi nguo, bangili, heleni, magauni, suluali na mishono ya nguo waliwapa sisi (social constructions). Wazazi ndio wanaowanunulia watoto wa kiume matoi ya bastola na magari na watoto wa kike midoli ya mwana sesele, vitu vya kujipikilisha na vitambaa vya kuvalisha watoto. Mimi watoto wangu wote niliwanunulia midoli inayofanana (bastola, magari, mwanasesele, nk) wachezee wote. Watoto wangu wa kike ndo walikuwa wa kwanza kuendesha magari yangu, na wote walikuwa na uwezo wa kukamua ng'ombe na kulisha na kufunga mbwa bandani. wote walijisikia wako sawa ila wote walijua kwanini wanatofautiana kwenye namna kukojoa; kuchuchumaa na kukojoa wima.