Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Zote ziko chini ya Mkandarasi anaitwa CHICO. Sharti ni kwamba mkandarasi akikabidhiwa Barabara lazima ahakikishe inapitika bila kikwazo, ni mbaya yes!

Unachosema ni kweli Kasulu to Kibondo kuna mkandarasi, nilivyohamishiwa huku kikazi barabara ilinikatisha tamaa as kulikuwa hakuna mkandarasi..ilikuwa vumbi kuanzia Nyakanazi till Kasulu, you can imagine
 
Unachosema ni kweli Kasulu to Kibondo kuna mkandarasi, nilivyohamishiwa huku kikazi barabara ilinikatisha tamaa as kulikuwa hakuna mkandarasi..ilikuwa vumbi kuanzia Nyakanazi till Kasulu, you can imagine
Nasikia kuja Wakandarasi CHICO, SINOHYDRO, ZCCC na STECOL
 
Ni kweli Mkuu. Hats Mimi naunga mkono. Kutembea usiku in hatari sana.
Anza safari walau saa moja asubuhi, maximum mpaka saa mbili usiku, lengo kutafuta sehemu ya kulala.
Na ni kweli, mchana unainjoi sana.
Na pia usiwe na haraka. Nenda mdogomdogo.
 
Asante kwa kunipa kumbukizi amazing

Picha ya kwa kwanza nimeitambua...ni daraja la mto malagarasi njia ya kasulu - kibondo ukitoka kijiji cha mvugwe

Hiyo sehemu ni mtihani kwa kweli nyakati za usiku
 
Umeni-inspire sana japo sipendi safari kabisa

Binafsi kama safari inaepukika huwa sisafiri, naonaga kero tu
 
Hiyo route ya majimoto hadi kamsamba sio mchezo!!cjajua kwa sasa hivi ila 2019, nilipita huko, daa sio kwa ubovu ule wa barabara hasa madaraja!!ni mengi mno halafu una kuta baadhi ya maeneo ina bidi upite tu kwani daraja hakuna limeshasombwa na maji, sema ilikuwa kipindi cha kiangazi, na gari ilikuwa ni hizi za kazi toyota pick up!!kama ni ist kule unaiacha kabisa!!!kamsamba hadi mlowo kuna msitu mzito pale unajulikana kama (BOT)sehemu ya wazee (majambazi)kuchukulia pesa zao!!!
 
Nyie wakazi wa Kigoma na Wale wa Kagera kueni wapole mpo karibu na nchi Tata kiusalama hatuwezi kuweka lami sehemu zote isije kikanuka siku1 jamaa wakatuingilia mpk ndani kirahisi rahisi(Na ndio maana Congo barabara zake Ni mbaya ili kupunguza kasi ya waasi walitaka kuja kuteka jiji Lao).

Mlevi akiwa anakunywa komoni alisikika akitoa mawazo yake hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…