Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Mkuu Bwana PGO
Safari yako ulitumia muda gani na kama hautajali ukiweka gharama ulizotumia aidha kwa ujumla au kwa mchanganuo

Je unafahamu organisers wanaofanya utalii huu wa road trip in groups
Shukrani sana, nilitumia takribani siku kumi, sio za kusafiri. Nazungumzia safari nzima, Kuna sehemu nilikua napumzika kidogo na kuonana na wadau.

Mafuta Nina baadhi ya risiti haifiki 700,000....kwa Mafuta.

Njiani nilikua nakula matunda zaidi Ili kubalance tumbo, ndizi, maepo (apples) 🍎🍏 za Makete, Karanga etc . Gharama halisi Sina ila haikuzidi 1.2m.
 
Ni kweli Mkuu. Hats Mimi naunga mkono. Kutembea usiku in hatari sana.
Anza safari walau saa moja asubuhi, maximum mpaka saa mbili usiku, lengo kutafuta sehemu ya kulala.
Na ni kweli, mchana unainjoi sana.
Na pia usiwe na haraka. Nenda mdogomdogo.
Usiku Wala hakuna hatari yoyote, hakikisha tu huna uchovu, gari Ina taa zenye mwanga wa kutosha na acha ku-overtake kijinga
 
Niliwaza kutumia Nissan Xtrail nikahofia kama nikipata breakdown, zile gari ni umeme 100% na mafundi wetu wa mkoani hawa
Umeme 100%! Sasa ulikuwa unaichaji wapi? Sijui kama tayari tunavyo vituo vya kuchaji magari au ulikuwa unaichaji mwenyewe hotelini!
 
Ni kweli Mkuu. Hats Mimi naunga mkono. Kutembea usiku in hatari sana.
Anza safari walau saa moja asubuhi, maximum mpaka saa mbili usiku, lengo kutafuta sehemu ya kulala.
Na ni kweli, mchana unainjoi sana.
Na pia usiwe na haraka. Nenda mdogomdogo.
Ukiwa na 4x4 na silaha usiku ni muda mzuri kusafiri. Hamna traffic wala magari mengi unatumia muda mfupi kufika eneo husika.
 
Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.

Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.

Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.

Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.

Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.

Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.

Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.

Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.

Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....

Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.

Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.

Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.

Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.

Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.

View attachment 2050099

View attachment 2050102

View attachment 2050103

View attachment 2050106

View attachment 2050107

View attachment 2050109

View attachment 2050110

View attachment 2050112

View attachment 2050113

View attachment 2050114

View attachment 2050115

View attachment 2050116

View attachment 2050118

View attachment 2050121
You deserve my salute
 
Back
Top Bottom