Safari yangu ya Elimu ilivyokuwa ngumu na kupata Zero mara tatu katika mtihani wa Kidato cha Nne

Safari yangu ya Elimu ilivyokuwa ngumu na kupata Zero mara tatu katika mtihani wa Kidato cha Nne

Safari yangu ya Elimu ya Secondary niliianza Mwaka 2011 katika Shule moja Maarufu pale Bukoba Mjini ikiitwa Lake View hakika Maisha ya Pale yalikuwa mazuri tulisoma na wahindi huku shule hipo beach yaani kila kitu nilikuwa Safi ,hasa ukizingatia nilisoma shule za kawaida katika Elimu ya msingi.


Baada ya kusoma na kufika kidato Cha Tatu kuelekea Cha nne nilikwama Ada na hivyo kushindwa kuendelea na Masomo hakika Jambo hili lilini-Affect kiakili Sana.


Basi baada ya kukaa Nyumbani muda Mrefu niliwaza kusoma Qt na hapo nyota yangu ya Kupata division zero ndipo ilipoanza kuwaka..

Hivyo mwaka 2014 nikafanikiwa kufanya mtihani wa kidato Cha nne Kama mtahiniwa wa Kujitegemea na hapo Ndipo napata zero yangu ya 35 kwa mara ya kwanza.


Baada ya Kupata zero ya kwanza nikapata Ushauri kuwa Ni re-sit tena Mwaka 2015 nikpata tena zero na hapo safari yangu ya Kumiliki cheti Cha kidato Cha nne ikakwama .


Tena mwaka 2016 nilifanya paper la form four na nikapata tena zero hivyo nikawa jumla nime-score zero 3 ndani ya miaka 03. Mfululizo.


Je ilikuaje nikapata degree na hapa ndo ntaleta funzo kuwa Imposssible is possible

ITAENDELEA

Uzi unasema ulipata 0x3. Itaendelea kwenda wapi sasa
 
Ulipata zero Mara tatu maana yake ulipewa taarifa tumia kipaji achana na elimu ili uwe tajiri!
Wakati mwingine unafeli ili ufanikiwe kupitia kipaji au kilimo
Sema watu huwa tuna kariri njia moja ndiyo maana hatuwi matajili

I bet kama una digrii itakuwa ya mchongo na kamwe haitakupa utajili zaidi utapata hela ya kula tu
Sio kila mtu anahitaji utajiri mkuu, wengine huitaji aman tu.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Uje uchukue zero yako nyingine huku
 
Mleta mada muombe hata rafiki/mumeo akusaidie uandike hadithi ndefu na iishe kwa haraka.
 
2017 form 4
2022 degree holder

Kajamaa haka huwa ni kaongo balaa
Afu ni kabishi noooma

Afu kukimbia uzi kamebadili jina toka
Haya land to tushome
 
Back
Top Bottom