Safari yangu ya jana imenisaidia kuitafakari imani yangu kwa dakika kadhaa

Dada umenitisha sana sana nikajua umeamua kwenda CCM! Achana na hao watu usiogope, Shika sana ulichonacho asije mtu akaichukua taji yako....Revelation 3:....
 
Hao achana nao wewe gonga injili tu, binafsi mimi nimeziona nguvu za Yesu Kristo na ukizilitea mchezo tu unapata adhabu kali sana.
Yesu Kristo ndio njia ya kweli na uzima,

Hakuna mwingine kama yeye, nguvu za Yesu Kristo zipo ndani ya Biblia soma Biblia kwa kuelewa na kuyashika Yale maneno utaziona nguvu zinakuja zenyewe.
 
Yesu anatupenda kweli!ila usiwekeze imani ya kristo kwa hzi taasisi za kiroho hasa makanisa!usije ukavunjika moyo kabisa!!nimeamua kuishi maisha yangu mwenyewe !!makanisa hayaaminiki kama taasisi kimbilio kwa waliovunjika moyo!!watakufinyanga wakukamue zaidi!!!yesu awe wako mwenyewe wala usichanganywe na mtu!!!
 




Safari ya masaa 4 (a 4 hrs journey???), kutoka wapi hadi wapi??, au SGR imeanza kazi??.

Juu ya yote ni Mungu pekee ndiye ukimuomba kwa dhati anaweza kukuongoza katika njia yake sahihi, usifuate njia uliyorithi kutoka kwa wazazi wako kwani siku ya hukumu kila mmoja ataulizwa kile alichofanya, pia kumbuka hao wazazi wako pia nao wana wazazi wao (Bibi na babu yako), sasa kama kila mtu atamtegemea mzazi wake kwa wema au ubaya aliofanya utakuta kwamba wale wazazi wa kwanza kuumbwa ndio watakuwa "responsible".

Kuna bwana mmoja ambaye alifanya maombi haya kwa Mungu akitafuta njia ya haki alisema: " Ewe Mungu wangu nakuomba unionyeshe njia ya haki usiponionyesha basi mimi nitakulaumu siku ya kiyama"---- huyo baadaye aliona njia ya haki na akakiri kwamba Mungu alisikia maombi yake.
 
Wanawake huwa ni wepesi sana kuaminishwa...
vitu vipya kirahisi rahisi....
ndivyo mlivyo that is nature.....
unaanzaje kuabudu jua....
unaacha kumuabudu aliyeumba hilo jua!!?
 
Akili kubwa km yako,bht mbaya wengi HAWANA....
 
Uzuri wa kuzaliwa kwenye imani unakuwa na watu wanaoielewa na kukupa muingozo pale unapokuwa na maswali. Kutokana na mafunzo na kuamini u Kristu ndiyo maana bado Nina imani yangu.

Wazazi wangu ninawaheshimu na hawawezi kunipeleka kwenye kitu kisicho bora lakini na mimi mwenyewe nimefahamu kuwa ni kitu bora.
 
mimi mwenyewe nimefahamu kuwa ni kitu bora

Hiyo hasa ndiyo point, sasa kwa index ipi unaweza kujua kwamba kitu/ jambo hili ni bora au siyo bora???--- mfano haiwezekani mbwa au kuku aliyedokoa nyama jikoni akahukumiwa tofauti na mtu akidokoa hiyo nyama, maana yangu ni hii kwamba kudokoa ni wizi na ni huyohuyo Mungu ametuambia tusiibe, tusizini, tusiseme uongo nk, sasa tunashindwaje kumuomba yeye atupe Muongozo kwa yale tusiyoyajua yale ambayo wazazi wetu wameshindwa kutufundisha kwa kutokuyajua kwani mwadadamu ni limited na Mungu ni unlimited.

Juu ya yote Mungu bado ni mtegemewa kwetu kwa kila hali, yeye ndiye aliyeweka index na yard sticks za sisi kuzifuata na binadamu atake asitake anahitaji muongozo na msaada kutoka kwake, no short cuts.

Omba msaada kwa Mungu akuongoze katika njia sahihi, kama umeridhika na njia hiyo basi utahukumiwa katika njia hiyo.
 
Kwanini huwa mnatishana kuhusu hukumu?! Mnasema Mungu ni mwema, na anasamehe bila kujali ukubwa wa dhambi,
Lakini waooga.
Mimi naamini hakuna hukumu zaidi ya hii tuipatayo humu duniani.
Imani ni imani, inategemea umezaliwa wapi na ukapokea nini, hakuna aliyesawa kuliko mwingine.
Ingekuwa wote tunaimani moja ningekuwa na mtizamo tofauti, lakini kwa hivi ilivyo wote tuko sawa.
Hakuna imani inayofundisha uovu, zote zinakataza uovu,hivyo zote ziko sawa kabisa.
 
Habari sky, nakushauri tafakari zaidi na pia muombe sana muumba wako akuonyeshe njia sahihi ya kumwabudia, kuwa huru uitafute haki ya kweli.
Wewe pia tafakari vizuri, kwa viashiria vichache tu, upo katika dini ya wanadamu, iliyojaa uongo, hadaa na vitisho. Karibu katika ile dini ya kweli na uweze kuipata ile nuru.
 
Yesu ni Njia, Kweli na Uzima!

Huyo kidume ulimpa namba ya simu?
 
Msema kwel mpenz wangu,,,,wengi tunaishi kwa kukaririshwa
Ila kwa Yesu ni kugumu wadau.Tuwe wakwel.Mi mwenyewe nimeokoka na namuamini Mungu ila dah kuna time unajikuta tu ushachanganya "makaratee" mengine ya "kimaghumashi" ilimradi life lisonge.
Ila naamin Mungu ananipenda hivyo hivyo.
Ntafanyaje sasa????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…