Safari za mabasi kwenda mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ni za hovyo sana

Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono, Hata hizo hoteli mbovu zilizopo zina chakula duni mno na cha hovyo sana na bei mbaya mno
 
Msafiri kafiri
 
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono, Hata hizo hoteli mbovu zilizopo zina chakula duni mno na cha hovyo sana na bei mbaya mn
Aibu sana!
Kwanini matajiri msiwekeze hii njia?
 
Hata wakiwekeza hakuna wateja,,,, abiria wa huko wanatoka na viporo vyao kabisa, nani akale chips kuku/samaki kwa 10k ? Au nyama choma na vindiz kadhaa atoe 10k ? Miaka flani nikiwa advance nilikuwa nasafiri sana kwenye hio kanda, unashangaa umekaa na mtu anatofoa kontena lake lina makande anaanza kula,,, mpaka maji ya kunywa wanatoka nayo home
 
🀣🀣🀣🀣
Shida wenye Hotel wanauzwa vyakula bei ghali!
 
Ushamba, eti pesa zao wanatunza benki. Halafu hawajui kupika, Iringa pa hovyo sana kwa chakula, pale Igumbilo kuna kahoteli mabasi huingia chakula kinakuwa kimeusu. Kaskazini mpaka wilayani kwa chakula ni next level
 
Ushamba, eti pesa zao wanatunza benki. Halafu hawajui kupika, Iringa pa hovyo sana kwa chakula, pale Igumbilo kuna kahoteli mabasi huingia chakula kinakuwa kimeusu. Kaskazini mpaka wilayani kwa chakula ni next level
Siyo Iringa pekee mkuu!..

Ni njia nzima hadi unafika Mbeya hamna sehemu ya maana ya kula
 
Wenyewe wamesha zoea, ukiona ni wagumu kubadilika badilika wewe uwe kama wao
njaa ya siku moja aiui, nunua soda au juisi, biskuti au vitafunwa vyovyote upoze njaa ukiwa safarini
 
Aisee. Kumbe bado wapo watu wanasafiri na viporo kwenye mabasi karne hii?
 
Vyakula vibaya halafu bei ndefu, wauzaji wanajua tu kuwa lazima abiria watanunua.

Abiria wengine kwao kusafiri ni kama tafrija, bei ya vyakula hawazingatii wanachofurahia ni kula tu wakiwa safarini kwao burudani

Ukiona unapigwa nunua biskuti na soda kabla haujaanza safari
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…