Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais kula bata hadi kuku waone wivu ......
Prezidee ongeza speed kwani dakika za mwisho hizi, utazikumbuka hizo safari, kuna Bembea na wasanii kibao wa mamtoni bado hujapiga nao picha! Kula bata mtoto wa kikwere si unajua sisi mabumbula hatuna uchungu na fedha zetu!
Wow hongera ccm hongera jk zidumu fikra za mwenyekiti tunaomba By 2015 safaris zisipungue 500 pls jk cover the rest zitimie 500 bado muda kidogo tuu pls
Iwekwe ktk katiba kuwa raisi asiwe amewahi kuwa waziri wa mambo ya NJE!
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.
Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.
Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.
Duuh.. so kwa wiki 2 Tanzania hakutakuwa na raisi..! Na we see nothing wrong with this..!
Aliyeanzisha huu uzi tulisha mkanya zamani, lakini naona bado kuna viherehere mmebaki.....Ok
jk na diamond wanapenda sana show za nje ya nchi kuliko za ndani, mwacheni JK WETU afaidi ujana.