Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Prezidee ongeza speed kwani dakika za mwisho hizi, utazikumbuka hizo safari, kuna Bembea na wasanii kibao wa mamtoni bado hujapiga nao picha! Kula bata mtoto wa kikwere si unajua sisi mabumbula hatuna uchungu na fedha zetu!
 
Wow hongera ccm hongera jk zidumu fikra za mwenyekiti tunaomba By 2015 safaris zisipungue 500 pls jk cover the rest zitimie 500 bado muda kidogo tuu pls
 
Prezidee ongeza speed kwani dakika za mwisho hizi, utazikumbuka hizo safari, kuna Bembea na wasanii kibao wa mamtoni bado hujapiga nao picha! Kula bata mtoto wa kikwere si unajua sisi mabumbula hatuna uchungu na fedha zetu!

:thumbup::thumbup::thumbup::thumbup:
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA




DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS





Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu
Fax: 255-22-2113425





PRESIDENT'S OFFICE,

STATE HOUSE,

1 BARACK OBAMA ROAD,

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.







TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.

Sijui hii itakuwa ni safari ya ngapi kwa ujumla na kwa nini ziara nyingi ni USA?
 
Kuna yeyote ana data za safari za marais waliopita yaani Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Nia ni kuzilinganisha jumla safari za marais hao waliomtangulia na za Mr.Vasco da Gama. Nina wasiwasi kuwa za JK zitakuwa ni nyingi kuliko ujumla wa safari zote zilizofanywa na marais hao 3.
 
Duuh.. so kwa wiki 2 Tanzania hakutakuwa na raisi..! Na we see nothing wrong with this..!
 
Aliyeanzisha huu uzi tulisha mkanya zamani, lakini naona bado kuna viherehere mmebaki.....Ok
 
Aliyeanzisha huu uzi tulisha mkanya zamani, lakini naona bado kuna viherehere mmebaki.....Ok

Acha kutisha watu mkuu.. Wana haki ya kulalamikia matumizi mabovu ya pesa zao kwa ajili ya kiongozi mmoja kutimiza hobby yake ya travelling.. Mwezi uliopita ametoka huko alikokaa zaidi ya 5 days.. leo tena huko huko for 2 weeks..
Kama unanufaika ni wewe na ndo maana kutwa uko humu kutetea uozo..
 
wakuu kama hamjajua ndo njia anayotumia kuchepuka hiyo na kutafuta wengine... kuna mtu katoa majina ya watoto wake na mamaa zao ni hatari tupu wanafika 25 (wanaofahamika)... NYERERE alishasema mkiingiza mhuni ikulu mtapata shida tukasahau kauli hiyo sasa tunajuta..!
 
Nna uhakika Hayati Michael Jackson angekuwa hai, Prezdaa JK angeenda kulala kwenye Mansion yake hata kwa siku mbili.
Hii ni Laana.
 
jk na diamond wanapenda sana show za nje ya nchi kuliko za ndani, mwacheni JK WETU afaidi ujana.
 
Back
Top Bottom