Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

kaka kama inawezaekana..nauomba ui-poat hii kitu kitabusura kule(facebook) ...ama atleast iwe posted katika kila thread ya jukwaa la siasa..hii itasaidia...tafadhali sana Jason Bourne
 
Ni muhimu kwa Rais kufanya safari nyingi kwa kipindi hiki alichokuwepo madarakani ili kuiunganisha Tanzania na mataifa. Taifa limegundua kwamba Katka East Africa na Afrika kwa ujumla Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho kwa kutofahamika kimataifa. Kwa mfano Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa (Eneo, idadi ya watu, maliasili n.k) lakini huwezi kuamini kuwa utafiti ulipofanyika katika nchi za Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Saudi Arabia, India, China na New Zealand, Tanzania ilishika mkia kwa wananchi wa nchi hizo kuifahamu (miongoni mwa Kenya, Uganda, Somali, Burundi, Rwanda, Zambia, Msumbiji, Sudan, Ethiopia, Eritrea, na djibout.) ispokuwa huko China na India ambako ilishika nafasi ya Tatu.

Uhusiano wa kimataifa ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Uchumi na Siasa ni vitu vinavyoenda pamoja na nyakati za Ujamaa tulielekeza macho yetu sana katika nchi za Kikomunist kama Rusia , Korea ya Kaskazini, kuba na China. Leo nchi hizo zote zenyewe zipo katika hali ngumu na kimsingi hatufaidiki sana na nchi hizo pengine China tu. Na si vizuri katika kipindi hiki kwa nchi moja kuwa na monopoli katika nchi nyingine, kwa sababu nchi zinozopenda kufanya biashara nasi lazima ziwe katika ushindani. Na mtazamo wa Tanzania kwa muda huu ni kuzichanganya kati ya nchi zilizoendelea na nchi na zile za kati kama Turky, Iran, Brazil, Mexico, Venuzuela, korea ya kusini, uhispania, Poland. Uzuri wa nchi hizi za kati ni kwamba, ziko tayari zaidi kuuza Teknlojia yaondogo waliyokuwa nayo kuliko nchi zilizoendelea. Leo hii Turky, Korea kaskazini, Brazil na Iran ndio wauzaji wakubwa wa Teknolojia ya kati kuliko nchi zilizoendelea. Na demand yake katika nchi za Afrika ni kubwa sana, na ni lazima kuifuata huko huko iliko.

Tatizo la Thread hii haijazingatia ni nini kinachopatikana katika safari za Rais bali imezingatia Idadi ya safari alizozifanya kwa kipindi alichokuwepo madarakani. Hili ni Tatizo la kutokuona mbali, na ni moja kati ya tatizo kubwa la Wana JF. Hii inanikumbusha filamu ya Senior Bachelor pale mke wa Erick alipomlaumu kwa kutokaa nyumbani. Erick alimuomba achague moja kati ya mawili, Au yeye akae siku nzima nyumbani na waishi katika umasikini ule wa zamani au amruhusu akachachalike huko nje na kurudi nyumbani na chochote. Mke wake hakuwa mjinga, alikaa kimya ndipo Erick alipopata jibu kuwa umasikini hautaki, na akaendelea kuchachalika nje. Na wanaJF wanamawili ya kuchagua kati ya... na ....

Populist Thread hazitatusaidia hapa JF wala kwa maendeleo ya nchi yetu. Kwa sababu watanzania wengi hapa JF WAMELALAMIKA KUWA TANZANIA HAIFAHAMIKI HUKO NJE. Leo juhudi mbali mbali zinafanyika ikiwa pamoja na kuisuka timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Kukuza Viwango vya Filamu zetu, leo zinaangaliwa na nchi nyingi Afrika n.k. Zote hizi ni katika juhudi za za kuipandisha chati Tanzania.

Kwa machache haya na kwa tathmini ya yale tuliyoyapata kwa safari za Rais, ninaziunga mkono safari zake zote na rais ajaye mwaka 2015 aendeleze uhusiano na nchi hizo na ikibidi naye asafiri.

kama nchi haina hata shirika la ndege utegemee nini
 
kaka kama inawezaekana..nauomba ui-poat hii kitu kitabusura kule(facebook) ...ama atleast iwe posted katika kila thread ya jukwaa la siasa..hii itasaidia...tafadhali sana Jason Bourne

Hii ni rahisi tu mkuu, mtu yeyote anaweza kuposti popote tu!

Nitajitahidi kuutumia ushauri wako!
 
hivi na hizi safari za hapo rwanda tunazihesabu?


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
kama nchi haina hata shirika la ndege utegemee nini

Umenena vyema mkuu,mchangiaji ameongelea kufahamika naye amekosea KUTOJIULIZA HAO WAMEFAHAMIKAJE? Sithani kwa SAFARI ILA KWA KUFANYA MAMBO YAKAONEKANA,JUZI NILIKUTANA NA MCANADA PALE MJINI AKANIULIZA HIVI MLIMA KILIMANJARO UPO KENYA AU TZ DAH? Wakenya sio hao wanakimbia wanafahamika sisi je?
 
Mungu wangu, yani kumbe ile hotuba hakuwepo nchini, katoka Rwanda na kwenda Burundi huku mgomo unaendelea??
 
Hivi hakuna mtu wa ikulu mwana JF atupe data kamili za namba za safari za nje na matumizi yake. Itatufaa sana hasa wengine tunaofikiria kuwa ikulu. Mwalimu aliuza ikulu pana nini pale, ningemjibu leo ningesema pana safari nyingi za nje!
 
nadhani kabla ya mtu kuingia ikulu, apitie mirembe kwanza! kwani vasco hana ratiba ya kwenda kwa baloteli kumpa poleeeee?? yaani PATHETIC kwa kweli!
 
UPDATES

Safari ya 330:

Hivi punde tumewasili nchini Uingereza,

Msafara wa mh rais Jakaya Kikwete umewasili Hyatt Regency London-The Churchill

Ziara hii imetufikisha hapa kwaajili ya mh rais kuhudhuria mkuta unaohusu mambo ya Family plan!
 
da jamaa ni travella kwelikweli, kawazd mabaharia wote wazaman i.e marcopolo
 
kuna mtu atusaidie rais gan ametembea sana dunian kama mr.dhaifu...hivi obama amesafir mara ngap nje ya nchi yake? thabo mbeki amesafir mara ngap? pia hadi mkewe analipwa posho? kwa kaz gan hasa? nchi hii ya kijiiinga....pumbafu
 
kuna mtu atusaidie rais gan ametembea sana dunian kama mr.dhaifu...hivi obama amesafir mara ngap nje ya nchi yake? thabo mbeki amesafir mara ngap? pia hadi mkewe salma analipwa posho? kwa kaz gan hasa? nchi hii ya kijiiinga....pumbafu nisaidien ktk maswal yangu yan cielewi mpk akiondoka itakuaje fisad nyangumi huyu..
 
Duh, safari ya 330?????. Mungu wangu. Jason, nasikia Obama ndiye anangoza kwa safari nyingi kama raisi wa merekani kwa safari 8..!?. Alafu..unaweza kutupa statistics ya comparison ya safari na maraisi wengine?.
 
Mkuu hii ni thread ya great thinker, updated, kweli hii ndiyo JF. Kitakwimu kama JK amesafiri mara 330, na kama kwa wastani alikaa ugeneni kwa siku mbili achilia mbali zile amekaa siku 5, 8, atakuwa nje ya ofisi kwa siku 660 almost 2 years out of 7 ambayo ni asilimia karibu 30 (30%) ya muda wake hayupo Tanzani plus an error term!! Sasa kama 30% ya time yaani miaka miwili kati ya 7, ukijumlisha na semina elekezi na safari za ndani atakuwa labda miaka mitano kati ya saba hayupo ofisini, labda ofisini siyo muhimu! sasa ili kufanya thered hii iwe nzuri zaidi, hebu tupige kwa wastani kila safari inagharimu kiasi gani kwa wastani, including acting allowances ambazo wanaokaimu hulipwa wakubwa wakisafiri na rais, halafu tuone hizo pesa ni kiasi gani. Mungu ibariki tanzania.
 
kuna mtu atusaidie rais gan ametembea sana dunian kama mr.dhaifu...hivi obama amesafir mara ngap nje ya nchi yake? thabo mbeki amesafir mara ngap? pia hadi mkewe salma analipwa posho? kwa kaz gan hasa? nchi hii ya kijiiinga....pumbafu nisaidien ktk maswal yangu yan cielewi mpk akiondoka itakuaje fisad nyangumi huyu..

Hivi kwani Kagame hawamwaliki?wakati yaonyesha wanafanya vema kwenye uchumi wao?
 
kaka jason kwa ushujaa wako wa kuvumbua mambo nakufananisha characters wa zile movie za james bond 007.tofauti ni ni ndogo,wao hutumia HITECH-divices kukamilisha malengo yao.hongera sana bro. 😛eace:
 
Back
Top Bottom