Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni muhimu kwa Rais kufanya safari nyingi kwa kipindi hiki alichokuwepo madarakani ili kuiunganisha Tanzania na mataifa. Taifa limegundua kwamba Katka East Africa na Afrika kwa ujumla Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho kwa kutofahamika kimataifa. Kwa mfano Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa (Eneo, idadi ya watu, maliasili n.k) lakini huwezi kuamini kuwa utafiti ulipofanyika katika nchi za Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Saudi Arabia, India, China na New Zealand, Tanzania ilishika mkia kwa wananchi wa nchi hizo kuifahamu (miongoni mwa Kenya, Uganda, Somali, Burundi, Rwanda, Zambia, Msumbiji, Sudan, Ethiopia, Eritrea, na djibout.) ispokuwa huko China na India ambako ilishika nafasi ya Tatu.
Uhusiano wa kimataifa ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Uchumi na Siasa ni vitu vinavyoenda pamoja na nyakati za Ujamaa tulielekeza macho yetu sana katika nchi za Kikomunist kama Rusia , Korea ya Kaskazini, kuba na China. Leo nchi hizo zote zenyewe zipo katika hali ngumu na kimsingi hatufaidiki sana na nchi hizo pengine China tu. Na si vizuri katika kipindi hiki kwa nchi moja kuwa na monopoli katika nchi nyingine, kwa sababu nchi zinozopenda kufanya biashara nasi lazima ziwe katika ushindani. Na mtazamo wa Tanzania kwa muda huu ni kuzichanganya kati ya nchi zilizoendelea na nchi na zile za kati kama Turky, Iran, Brazil, Mexico, Venuzuela, korea ya kusini, uhispania, Poland. Uzuri wa nchi hizi za kati ni kwamba, ziko tayari zaidi kuuza Teknlojia yaondogo waliyokuwa nayo kuliko nchi zilizoendelea. Leo hii Turky, Korea kaskazini, Brazil na Iran ndio wauzaji wakubwa wa Teknolojia ya kati kuliko nchi zilizoendelea. Na demand yake katika nchi za Afrika ni kubwa sana, na ni lazima kuifuata huko huko iliko.
Tatizo la Thread hii haijazingatia ni nini kinachopatikana katika safari za Rais bali imezingatia Idadi ya safari alizozifanya kwa kipindi alichokuwepo madarakani. Hili ni Tatizo la kutokuona mbali, na ni moja kati ya tatizo kubwa la Wana JF. Hii inanikumbusha filamu ya Senior Bachelor pale mke wa Erick alipomlaumu kwa kutokaa nyumbani. Erick alimuomba achague moja kati ya mawili, Au yeye akae siku nzima nyumbani na waishi katika umasikini ule wa zamani au amruhusu akachachalike huko nje na kurudi nyumbani na chochote. Mke wake hakuwa mjinga, alikaa kimya ndipo Erick alipopata jibu kuwa umasikini hautaki, na akaendelea kuchachalika nje. Na wanaJF wanamawili ya kuchagua kati ya... na ....
Populist Thread hazitatusaidia hapa JF wala kwa maendeleo ya nchi yetu. Kwa sababu watanzania wengi hapa JF WAMELALAMIKA KUWA TANZANIA HAIFAHAMIKI HUKO NJE. Leo juhudi mbali mbali zinafanyika ikiwa pamoja na kuisuka timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Kukuza Viwango vya Filamu zetu, leo zinaangaliwa na nchi nyingi Afrika n.k. Zote hizi ni katika juhudi za za kuipandisha chati Tanzania.
Kwa machache haya na kwa tathmini ya yale tuliyoyapata kwa safari za Rais, ninaziunga mkono safari zake zote na rais ajaye mwaka 2015 aendeleze uhusiano na nchi hizo na ikibidi naye asafiri.
kaka kama inawezaekana..nauomba ui-poat hii kitu kitabusura kule(facebook) ...ama atleast iwe posted katika kila thread ya jukwaa la siasa..hii itasaidia...tafadhali sana Jason Bourne
kama nchi haina hata shirika la ndege utegemee nini
kuna mtu atusaidie rais gan ametembea sana dunian kama mr.dhaifu...hivi obama amesafir mara ngap nje ya nchi yake? thabo mbeki amesafir mara ngap? pia hadi mkewe salma analipwa posho? kwa kaz gan hasa? nchi hii ya kijiiinga....pumbafu nisaidien ktk maswal yangu yan cielewi mpk akiondoka itakuaje fisad nyangumi huyu..