Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Alishasema yeye ni mzee wa kuhemea vibaba ili tusife njaa. Sasa akikaa ikulu atahemea saa ngapi? Ikulu anapita tu kuoga na kubadilisha nguo. Alisha maliza kuonana na marais wa marekani huko marekani na hapa Tz sasa ameanza kutembelea majimbo ya marekani kama waziri mkuu wa marekani mpaka amalize yote
 
Huu ni wizi tu na mwandishi wa habari hii ni kanjanja.

Mtu alikuwa anatoka zake Magomeni anaenda kuomba Viza na kupewa the same day, leo hii unaletwa utaratibu wa siku tano halafu mwandishi anaandika utaratibu umerahisishwa!!! Hawa waandishi wa gazeti la Tanzania Daima ni SIFURI kabisa.

Utaratibu wa viza Uingereza ni mbovu na UK wenyewe washaona kuwa watu hawaendi na wameanza kuhisi kuwa kumbe wanahitaji watu wetu nao waende UK so wanajifanya kulegeza masharti kwa kisingizio cha kurahisisha!
 
"Mimi nakwenda kule (Ulaya na Marekani) kuhemea. Nikirudi narudi na kibaba”, - Jakaya Mrisho Kikwete
 
Huyu ni wazir wa mambo ya nje na analiua taifa....
 
Nampenda sana rais wa Botswana Lieuternant Khama Ian Khama hasafiri safari zaid ya 10 kwa mwaka. Jk alienda mwaka flan kusherekea miaka 40ya chama tawala, Khama hajawahi gusa hapa tz huwa anatuma vijana wake na hapendi kusafiri nchi yake 1$=6Pulla na inazid kuimarika nchi ya watu milion 3

Tz tumerogwa
 
View attachment 112776
Na alituroga kama kafa.View attachment 112777View attachment 112778View attachment 112779
Na haya ndio tunayoyaweza 1379682228002.jpg
 
Binafsi nimefurahishwa sana na matokeo ya safari za Mh. Kikwete nje ya nchi, zimekua na manufaa makubwa kisiasa , kiuchumi na kujenga mahusiano mema na chanya kwa nchi yetu na nchi nyingi Kimataifa.

Ingawa wapinzani na wananchi wengine wanaweza tazama safari za Rais wetu, kama kupoteza rasilimali nyingi, lakini badala yake zimekua chachu, na nchanzo cha kujenga nchi yetu katika siasa za kimataifa.

Kwa ufupi na wote tumeona na kushuhudia, ujio wa viongozi wakubwa duniani, akiwemo Rais wa Marekani Barak Obama, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, mawaziri wakuu wa nchi mbali mbali, na marais wengine ambao wote wameleta neema kubwa ya kiuchumi.

Ujio wa marais hao na viongozi mbali mbali wa dunia, umeifungua Tanzania kiuchumi, na kua kiongozi katika nchi za Afrika mashariki kwa uchumi bora, tukiwa na faida ya amani inayotufanya tuwe sehemu bora ya kuwekeza Afrika mashariki.

Bila shaka na haipingiki, kwa sasa Tanzania inakua sana kiuchumi, kuliko nchi nyingine afrika mashariki jambo lililozifanya mataifa makubwa duniani kuichukulia kama mshirika mkubwa wa kiuchumi.

Kwa kuzingatia hilo, Rais wa marekani kwa kuona umuhimu wa Tanzania, kwa siasa za sasa na baadae, kutokana na nguvu ya uchumi ambayo inayo na itakayokuja kuwepo, akambadili balozi wa Marekani Tanzania, na kumleta mshauri wake wa karibu katika ikulu yake kuwa balozi wa Tanzania, hili ni jambo la kujipongeza kwa kukubalika.

Safari za Rais wetu zimetujenga katika siasa za kimataifa na si jambo la kupingika kua kwa sasa Tanzania ni moja wapo ya nchi zinazokubalika kimataifa na kutazamwa kama super power siku zijazo.

Safari za rais wetu, zikienda sambaba na ukuaji wa uchumi na kufunguliwa milango kwa miradi mbali mbali mikubwa, zimeibua mengi yaliyojificha nyuma ya pazia katika mahusiano yetu na majirani wetu.

Bila shaka kila mmoja anafahamu ni kwa jinsi gani nchi nyingine za maziwa makuu zinavyoendelea na kampeni za kuitenga tanzania katika shirikisho la kisiasa, hii ni baada ya kuona kua ukuaji wake ni mkubwa na hatarishi kwa mataifa mengine ya maeneo haya.

Kwa mtazamo wangu kutengwa huku, ni matokeo ya wivu na woga wa ukuaji wa kiuchumi wa Tanzania, pamoja na mbinu mbadala ya kuilazimisha Tanzania kuingia katika shirikisho hilo la kisiasa ili hatimae nchi hizo zifaidike moja kwa moja na neema iliyopo ndani ya Tanzania.

Watanzania , tunapaswa kushukuru kutokana na matokeo haya ya ziara hizi, kwani zisingekuwepo, ingetuchukua muda kutambua agenda ya siri ya marafiki zetu juu ya neema za taifa hili.


Binafsi naziunga mkono safari za Rais wetu na nina mtakia kila la heri katika kuikuza nchi yetu kiuchumi, kisiasa, kulinda amani ya nchi, rasilimali zake, mipaka na Raia kwa ujumla.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mdau,

Stroke.

kugawa urithi wa wajukuu zetu kwa wachina!
 
:hungry: Mhhh......."Baba anahemea chakula" kwa ajili wananchi wake!! teh..tehee
 
Nampenda sana rais wa Botswana Lieuternant Khama Ian Khama hasafiri safari zaid ya 10 kwa mwaka. Jk alienda mwaka flan kusherekea miaka 40ya chama tawala, Khama hajawahi gusa hapa tz huwa anatuma vijana wake na hapendi kusafiri nchi yake 1$=6Pulla na inazid kuimarika nchi ya watu milion 3

Tz tumerogwa
Sijaelewa point yako hapa!.

Kwa hiyo unataka kusema nini?.

Kwa hiyo Unataka kusema Rais wa Botswana kwa vile hasafiri mara kwa mara atakuwa nni mtendaji mzuri na hatumii pesa za walipa kodi vibaya?.
 
Nimejaribu kuzitafakari kwa kina safari 357 ambazo mpaka sasa Mkuu wa Kaya amezifanya nje ya nchi ,nimeassume kila safari moja amekaa siku 3 tu,ina maana ametumia siku 1,071 (357 x 3) ambazo ni sawa na miaka 3 (1071/365),so nimepata jibu kuwa ndani ya miaka 8 aliyokaa ikulu yetu,ikulu imelala wazi miaka 3. Ni tafakari tu wadau!

Hivi mtu anayependelea kula miguu ya kuku utotoni anakuwa mzururaji sana??
 
wakuu hapa kuna siku zaidi ya 25 Rais hatakuwa nchini, karibia mwezi mzima! Ama kweli Rais tunaye!!


SAFARI YA 356

Tarehe 13/09/2013

Rais Jakaya Kikwete anawasili Windhock Nambia kwa ziara ya kiserikali,

UPDATES:

SAFARI YA 357

Tarehe 16/09/2013

Rais Jakaya Kikwete anawasili Marekani kwa ziara ya kiserikali itakayo mchukua hadi Canada na tarehe 26/09/2013 atahudhuri mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York,,
 
Back
Top Bottom